Jumatano, 1 Agosti 2018

Ufunuo wa Yesu Kuhusu Kuzimu. Sura ya 1



Ufunuo wa Yesu Kuhusu Kuzimu
na Mary K Baxter

Translated to Swahili by Ambakisye Mtawa, ambamtawa@gmail.com
Sikiliza ushuhuda wa moja kwa moja juu ya
uwepo Halisi wa Kuzimu. Mary Katherine
Baxter alichaguliwa na Mungu ili kuujulisha
ulimwengu juu wa UHALISI wa Kuzimu. Yesu
Kristo alimtokea Mary Baxter wakati wa usiku
siku 40 mfululizo na kumtembeza kuzimu na
Mbinguni. Alitembea, na Yesu, na kuona
mambo ya kutisha ya Kuzimu na alizungumza
na watu wengi.Yesu alimwonyesha ni kitu gani
kinatokea roho zinapokufa na mambo gani
yanatokea kwa wasioamini na watumishi wa
Mungu ambao hawatii wito walioitiwa.
Neno la Awali
Wakfu
Sura ya 9 – Vitisho vya Kuzimu Sura ya 19 – Mdomo wa Kuzimu
Utangulizi Sura ya 10 – Moyo wa Kuzimu Sura ya 20 - Mbinguni
Sura ya 1-Kwenda Kuzimu Sura ya 11 – Giza la Nje Sura ya 21 – Dini ya Uongo
Sura ya 2 - Mguu wa Kushoto wa
Kuzimu
Sura ya 12 - Pembe Sura ya 22 – Alama ya Mnyama
Sura ya 3 - Mguu wa Kulia wa
Kuzimu
Sura ya 13 – Mkono wa Kulia wa
Kuzimu
Sura ya 23 – Kurudi kwa Kristo
Sura ya 4 - Mashimo Zaidi
Sura ya 14 – Mkono wa Kushoto wa
Kuzimu
Sura ya 24 – Ombi la Mwisho la
Mungu
Sura ya 5 – Pango la Hofu Sura ya 15 – Siku za Yoeli Sura ya 25 – Maono ya Mbingu
Sura ya 6 - Matendo Katika Kuzimu Sura ya 16 – Kitovu cha Kuzimu
Sura ya 26 –Unabii Kutoka kwa
Yesu
Sura ya 7 – Tumbo la Kuzimu Sura ya 17 – Vita Katika Mbingu Maneno ya Kufungia
Sura ya 8 – Selo za Kuzimu
Sura ya 18 – Maono ya Wazi Kutoka
Kuzimu
Kuhusu Mwandishi
Mwaliko wa huduma
2

Neno la Awali
Marcus Bach alisema kwamba mara nyingi vitabu ni kama watoto wa akili, wala hakukosea. Sio
kama watoto wa nyama na damu, watoto hawa, wanaozaliwa kwa kupanga au kwa bahati
wamepangiwa maisha yao wenyewe. Kuishi kwao katika ulimwengu huu kunafanana na watoto
wengine. Hisia zote za kibinadamu ni zao. Si ajabu hofu yao ya siri ni kwamba siku moja watawekwa
kando na kusaulika moja kwa moja.
Tofauti na vitabu vingine, ninaamini kwamba Roho Mtakatifu amefanya maandishi haya kuwepo kwa
muda na milele. Ushuhuda na ujumbe huu ni wa muhimu sana kwa mwili wa Kristo. Ninaamini
kwamba upako wa Mungu utakuwa juu ya kitabu hiki na kumhudumia kila mtu asomaye yaliyomo.

Wakfu
Kazi hii imewekwa wakfu kwa utukufu wa Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu,
bila Yeye kitabu hiki kisingewezekana kuwepo.

Utangulizi
Ninatambua kwamba bila nguvu za Bwana Yesu Kristo, kitabu hiki au kingine
kinachoshughulikia na maisha baada ya kifo kisingeandikwa.Yesu peke yake ndiye aliye
na funguo za Kuzimu na amelipa gharama za kutuingiza mbinguni.
Niligundua kwamba kuandika kitabu hiki ilikuwa ni kazi ndefu, ya upweke, na ngumu.
Kwa kweli kitabu hiki kimesubiri miaka mingi kufunuliwa. Ufunuo kutoka kwa Bwana
ulinijia mwaka 1976. Ilinichukua miezi minane kuuandika katika karatasi. Uandikaji wa
rasimu ulichukua miaka mingi na uwekaji wa vifungu vya Maandiko hatua kwa hatua
ilinichukua mwaka mwingine zaidi. Kukamilisha kitabu kulichukua msimu wa baridi wa
1982 na mwaka 1983. Vile vile kwa muda wa siku thelathini, Yesu alinichukua hadi
Kuzimu wakati wa usiku, zikafuata siku kumi za kutembelea mbinguni wakati wa usiku.
Sasa naona kwamba Bwana alikuwa ananiandaa kuandika kitabu hiki tangu nilipokuwa
mtoto mdogo nilipokuwa naota mambo ya Mungu. Baada ya kuzaliwa mara ya pili,
nilikuwa na mapenzi sana kwa waliopotea na nilikuwa natamani kuona roho zikiokolewa.
Baadaye Bwana alinitokea mwaka 1976 na kuniambia kwamba nilikuwa nimechaguliwa
kwa ajili ya kazi maalum, Aliniambia,
Mwanangu, nitajithibitisha kwako na kuwatoa watu kutoka gizani na kuwaleta nuruni.
Kwa maana Bwana Mungu amekuchagua kwa kusudi, kuandika na kuweka kumbukumbu
ya mambo nitakayokuonyesha na kukuambia.
3
"Nitakufunulia uhalisi wa kuzimu, ili wengi waokolewe, wengi watatubu njia zao mbaya
kabla hawajachelewa.
"Roho yako itachukuliwa kutoka kwenye mwili wako, na mimi, Bwana Yesu Kristo, na
kupelekwa kuzimu na sehemu nyingine nitakazopenda kukuonyesha. Vile vile
nitakuonyesha maono ya mbinguni na mahali pengine na kukupa mafunuo mengi.”
Mary Kathryn Baxter

Kwa Kathryn kutoka kwa Yesu
Kwa kusudi hili ulizaliwa, kuandika na kueleza mambo niliyokuonyesha na kukuambia.
Maana mambo haya ni uaminifu na kweli. Wito wako ni kuufanya ulimwengu ujue kwamba
kuna kuzimu, na kwamba Mimi, Yesu, nilitumwa na Baba ili kuwaokoa kwenye mateso
haya.

Sura ya 1
Kwenda Kuzimu
Mwezi Machi 1976 nilipokuwa naomba nyumbani, nilitembelewa na Bwana Yesu. Nilikuwa
nikiomba katika Roho kwa siku kadhaa ambapo mara nilihisi uwepo halisi wa Mungu.
Nguvu yake na utukufu wake uliijaza nyumba. Mwanga mkali ulikijaza chumba nilimokuwa
naomba, na hali ya kujisikia vizuri ilinijia.
Mwanga ulikuja kama mvuke, ukiviringika na kujikunja na kujikunjurua tena. Lilikuwa
jambo la ajabu. Ndipo sauti ya Bwana ikaanza kuzungumza nami.
Alisema, "Mimi ni Yesu Kristo, Bwana wako, nataka kukupa ufunuo wa kuwaandaa
watakatifu kwa ajili ya kurudi kwangu na kuwageuza wengi kuelekea kwenye haki.
Nguvu za giza ni halisi na hukumu zangu ni halisi.
"Mwanangu, nitakupeleka kuzimu kwa Roho Yangu, na nitakuonyesha mambo
mengi ambayo nataka ulimwengu uyajue. Nitaonekana kwako mara nyingi;
nitaichukua roho yako nje ya mwili wako na nitakupeleka kuzimu kihalisi.
"Nataka uandike kitabu na ueleze maono yote na mambo yote nitakayofunulia. Mimi
na wewe tutatembea kuzimu pamoja. Andika mambo haya yaliyopo na
yatakayokuja. Maneno yangu ni hakika, kweli, aminifu. Mimi Ndimi, wala hakuna
mwingine badala yangu.
4
"Bwana wangu,” nililia, “Unataka nifanye nini?” Kila kitu ndani yangu kilitaka kumlilia Yesu,
kukiri uwepo wake. Nikijitahidi sana kueleza niseme kwamba upendo ulinifunika. Ulikuwa
ni upendo mzuri, wa amani, wa furaha, wenye nguvu, kuliko nilivyowahi kuhisi wakati
wowote.
Sifa za Mungu zilianza kunimiminika. Pale pale nilitamani kumpa maisha yangu yote
ayatumie, kusaidia kuwakoa watu katika dhambi. Nilijua, kwa Roho wake, kwamba
alikuwa Yesu Mwana wa Mungu aliyekuwa chumbani pamoja nami. Sipati maneno ya
kuelezea uwepo wake. Lakini najua kwamba najua kwamba alikuwa ni Bwana.
"Angalia , mwanangu,Yesu alisema, Ninakuchukua kwa roho wangu hadi kuzimu ili
uweze kuelezea uhalisi wake, kuiambia dunia nzima kwamba kuzimu ni halisi, na
kuwatoa waliopotea kutoka gizani kuingia kwenye nuru ya injili ya Yesu Kristo.
Mara ile ile, roho yangu ilitolewa ndani ya mwili. Nilitoka na Yesu kutoka ndani ya chumba
changu tukaingia hewani. Nilikuwa na ufahamu wa mambo yote yaliyokuwa
yananizunguka. Nilimuona mume wangu na watoto wamelala pale chini nyumbani.
Ilikuwa kama nimekufa na mwili wangu umeachwa nyuma kwenye kitanda wakati roho
yangu inapanda juu na Yesu kupitia paa la nyumba. Ilikuwa kama paa lote limeezuliwa, na
niliona familia yangu imelala vitandani.
Niliona Yesu akinigusa na kuniambia, “Usiogope. Watakuwa salama.Alitambua
mawazo yangu.
Nitajihidi kwa kadri ya uwezo wangu kueleza hatua kwa hatua niliyoyaona na nilivyojisikia.
Mambo mengine sikuelewa. Bwana Yesu alinieleza maana ya mambo mengi, lakini
mambo mengine hakuniambia.
Nilifahamu wakati ule, na sasa nafahamu, kwamba mambo haya yalikuwa yanatokea
kihalisi na Mungu mwenyewe ndiye angeweza kunionyesha. Litukuzwe Jina lake. Jamani,
niamini, kuzimu ni halisi.Nilipelekwa kule na Roho mara nyingi wakati wa kuandaa taarifa
hii.
Mara tulikuwa katika anga za juu. Niligeuka na kumtazama Yesu. Alikuwa amejaa utukufu
na nguvu, na amani ya ajabu ilifurika kutoka kwake. Alichukua mkono wangu na kusema,
Nakupenda. Usiogope, maana niko pamoja nawe.”
Baada ya hayo, tulianza kupaa juu zaidi mawinguni, na sasa niliweza kuiona dunia kwa
chini. Katika sehemu nyingi kulikuwa na mashimo (faneli) yaliyokuwa yanajizungusha
kueleka mahali fulani, na kurudi tena yalikotoka.. Haya yalikuwa yanatembea juu sana ya
dunia na yalikuwa kama kitu fulani kikubwa, kichafu na kinachoteleza kinazunguka wakati
5
wote. Vilikuwa vinajitokeza duniani pote. Vitu gani hivi?” Nilimuuliza Bwana Yesu
tulipokuwa tunakikaribia kimojawapo.
"Haya ni malango ya kuzimu, Aliniambia. Tutaingia kwenye mojawapo.
Mara tuliingia mojawapo ya mashimo haya. Ndani lilionekana kama tanuru, likizunguka na
kuzunguka kama pia.
Giza nene ilituangukia, na pamoja na giza hilo ilikuja harufu mbaya sana kiasi cha
kwamba ilikausha pumzi yangu. Kwenye kuta za shimo hili kulikuwa na viumbe vimeganda
kwenye kuta. Vilikuwa na rangi ya zambarau, viumbe hivi vilitembea na kupiga kelele
tulipopita. Nilijua bila kuambiwa kwamba vilikuwa viovu.
Viumbe hivi vingeweza kutembea lakini viliganda kwenye kuta. Vilitoa harufu mbaya sana,
na vilitupigia kelele zenye kukera kweli. Nilihisi nguvu fulani ya giza, isiyoonekana,
ikitembea ndani ya mapango.
Wakati fulani, katika giza, niliweza kuona maumbile. Chura mchafu alijaza kuta za pango.
Bwana vitu gani hivi?” Niliuliza huku nikishika mkono wa Yesu kwa nguvu.
Alisema, "Hizi ni roho chafu ambazo ziko tayari kumwagwa duniani pindi Shetani
atakapotoa amri."
Tulipokuwa tunashuka kwenye pango, viumbe hivyo viovu vilicheka na kutuita. Vilijaribu
kutugusa, lakini havikuweza kwa sababu ya nguvu ya Yesu. Hewa yenyewe ilikuwa chafu,
ni uwepo wa Yesu tu ulionizuia kupiga kelele kwa utisho mkubwa uliokuwepo.
Oh, ndio, nilikuwa na fahamu zangu zote – niliweza kusikia, kunusa, kuona, kugusa na
hata kuonja uovu wa mahali hapa. Zaidi ya hapo fahamu zangu zilikuwa makini zaidi,
harufu na uchafu vilinitia kichefuchefu.
Mayowe yalijaza hewa tulipokaribia mwanzo wa shimo. Vilio vikali vilipanda juu na
kutulaki. Sauti za kila namna ziliijaza hewa. Nilisikia hofu, mauti na dhambi vikinizunguka.
Harufu mbaya ambayo sijawahi kunusa iliijaza hewa. Ilikuwa harufu ya mzoga unaooza,
na ilielekea kutoka kila upande. Kamwe hapa duniani nilikuwa sijawahi kuhisi kiasi hiki cha
ouvu au kusikia sauti za namna hii za kukata tamaa. Muda si muda ningeligundua
kwamba mayowe haya yalikuwa ya wafu na kwamba kuzimu kulijaa mayowe yao.
Nilisikia mvumo wa upepo mbaya na mvuto mdogo mbele yetu. Mwanga kama wa radi
ulipenyeza kwenye giza nene na kutupa vivuli vyeusi vyeusi kwenye kuta. Niliweza kuona
umbile la kitu fulani mbele yangu. Nililishtuka nilipotambua kwamba joka kubwa lilikuwa
linatambaa mbele yetu. Nilipoendelea kutazama niliona nyoka wengi wabaya
wanatambaa kila mahali.
6
Yesu aliniambia "Muda si mrefu tutaingia kwenye mguu wa kushoto wa kuzimu. Huko
mbele utaona huzuni kubwa, masikitiko ya kutisha na vitisho visivyoelezeka. Kaa
karibu na Mimi, nami nitakupa nguvu na ulinzi tunapopita kuzimu. Mambo ambayo
utayaona ni tahadhari, Aliniambia. "Kitabu utakachokiandika kitaziokoa roho
nyingi zisiende kuzimu. Unayoyaona ni halisi. Usiogope, kwa maana nitakuwa
pamoja nawe
Hatimaye, Bwana Yesu namimi tulifika chini ya shimo. Tuliingia kuzimu. Nitajitahidi kwa
uwezo wangu wote kukueleza niliyoyaona, na nitasimulia kwa ule mpangilio ambao
Mungu alinipa.
Mbele yetu, kwa kadri nilivyoweza kuona, kulikuwa na vitu vinaruka huku na kule. Sauti za
kukoroma na vilio vya huzuni viliijaza hewa. Juu niliona mwanga hafifu, na tulianza
kuufuata. Njia ilikuwa kavu na yenye mavumbi. Mara tulifika kwenye mlango wa kuelekea
kwenye shimo dogo lenye giza.
Mambo mengine siwezi kuyaandika kwenye karatasi; yalikuwa yanatisha mno kuyaeleza.
Kuzimu hofu unaisikia hasa, na nilijua kwamba kama nisingelikuwa na Yesu nisingeweza
kurudi. Katika kuandika haya, baadhi ya mambo niliyoyaona sikuyaelewa, lakini Bwana
anajua yote, na alinisaidia kuelewa mambo mengi niliyoyona.
Nakuonya, usiende mahali kule. Ni mahali penye mateso ya ajabu, maumivu makubwa,
na huzuni ya milele. Roho yako itakuwa hai wakati wote. Roho inaishi milele.Roho ndio
wewe, na roho yako itakwenda mbinguni au kuzimu.
Kwa wale mnaodhani kwamba kuzimu ipo hapa duniani – sawa, ipo hapa. Kuzimu ipo
katikati ya dunia, na kule kuna roho ziko kwenye mateso usiku na mchana. Kuzimu
hakuna sherehe. Hakuna upendo, hakuna kuhurumiana. Hakuna kupumzika. Ila ni mahali
penye masikitiko zaidi ya unavyoweza kudhani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni