Alhamisi, 1 Machi 2018

Notes za FONETIKI NA FONOLOJIA



CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA ELIMU MKWAWA
   KITIVO CHA SAYANSI ZA JAMII
IDARA YA LUGHA NA FASIHI
   KI 208: FONOLOJIA YA KISWAHILI


© PENDO MWASHOTA: B. A (ED (Hons), M.A (Kiswahili) Dar, PhD Candidate (UDSM)
2017.

MODULI YA 1: FONETIKI NA FONOLOJIA
FONOLOJIA NI NINI?
Fonolojia ni taaluma ya isimu inayochunguza mifumo ya sauti za kutamkwa zinazotumika katika lugha asilia mahususi za binadamu. Inapolinganishwa na fonetiki, inasisitizwa kuwa fonolojia ni tawi la isimu linalochunguza mifumo ya sauti za lugha mahsusi  tu, kama vile sauti za Kiswahili, Kiingereza, Kigogo, n.k. Hata hivyo, wapo wanaisimu wanaoelekea kukubaliana kuwa kuna fonetiki ya lugha mahsusi pia, na kuna fonolojia ya jumla, na fonetiki ya lugha mahususi. Mathalani, Massamba (1996) licha ya kufasili fonolojia kuwa ni taaluma ya isimu inayochunguza mfumo wa sauti za lugha mahsusi, anaenda mbele zaidi na kudai kuwa fonolojia inaweza kuchunguza sauti kwa ujumla wake bila kuzihusisha na lugha mahsusi.
Akmajian na wenzake (2001), nao wanadokeza msimamo kama wa Massamba (1996) wanapodai kwamba fonolojia inaweza kuchunguzwa kwa mitazamo miwili tofauti. Kwanza, fonolojia kama tawi dogo la isimu linalochunguza mfumo na ruwaza za sauti za lugha mahsusi ya binadamu; na pili, fonolojia kama sehemu ya nadharia ya jumla ya lugha ya binadamu inayohusika na tabia za jumla za mfumo wa sauti za lugha asilia za binadamu.
Massamba (2012:3) anasema kuwa fonolojia ni tawi la isimu linalojishughulisha na kuchunguza mifumo ya lugha mbalimbali za binadamu: Kila lugha ya binadamu ina mfumo wake wa sauti ambao huongoza ujenzi wa maneno ya lugha hiyo.
-          Taaluma hii hujishughulisha na jinsi sauti za lugha zinavyotumika katika kujenga maneno ambayo huwakilisha maana.
-          Hujishughulisha na muundo, mjengo na kazi ya sauti za lugha mbalimbali za binadamu.
-          Fonolojia ni taaluma inayotuambia ni sauti zipi zinatumika katika lugha fualni na zipi hazitumiki katika lugha hiyo. Pia taaluma hii hutuelekeza uwezekano wa mfuatano wa sauti katika lugha hiyo, na  ni sauti zipi zinaweza kutokea katika mazingira yapi; hutuelekeza ni sauti zipi zinaweza kuungana na kuna mashartizuizi gani.
-          Kwa kuwa lugha zote za binadamu ni asilia na zote hutumia sauti kutoka katika BOHARI KUU lilelile la sauti bila shaka zitakuwa zinachangia sifa za msingi. Hata hivyo, kwa kuwa kila lugha ina mfumo wake tofauti wa sauti haitawezekana kuwa na lugha mbili zenye mfumo uleule mmoja wa sauti.
RUWAZA ZA SAUTI KATIKA LUGHA HUONEKANA KUTOFAUTIANA KWA NAMNA MBALIMBALI
-          Kwa kuwa kila lugha asilia huchagua kutoka bohari kuu la sauti, sauti chache tu, orodha ya sauti zitumikazo katika lugha zote haiwezi kuwa sawa.
-          Kila lugha inaweza kuwa na namna tofauti ya utokeaji wa sauti zake. Yaani kila lugha inaweza ikawa na mashartizuizi ya mfuatano wa sauti zake. Kwa mfano; embryo katika lugha ya Kiingereza ni kubalifu lakini katika lugha ya Kiswahili si kubalifu.
-          Michakato inayoleta mabadiliko katika lugha moja si lazima ilete mabadiliko katika lugha nyingine. Hali hii inatokea hata katika lugha zinazotoka katika mbari kuu moja.
-          Pia, sifa ambayo ni pambanuzi katika lugha moja si lazima iwe pambanuzi katika lugha nyingine.
-          Kila lugha ina uziada bileshi tofauti na lugha nyingine. Yaani sifa ambayo si muhimu katika lugha moja inaweza kuwa muhimu sana katika lugha nyingine.
-          Kila lugha inaweza kuwa na mfumo wake wa irabu. Baadhi ya lugha zina irabu saba, nyingine zina irabu tano na nyingine zina irabu tatu. Pia kila lugha ina mfumo wake wa konsonanti, kwani kila lugha huchota konsonanti chache tu kutoka katika BOHARI KUU LA SAUTI.
 Katika mhadhara huu, hata hivyo, tutakuwa wafuasi wa mtazamo unaoona kuwa fonolojia ni tawi la isimu linaloshughulikia mfumo wa sauti za lugha mahususi, hivyo tuna, kwa mfano, fonolojia ya Kiswahili, fonolojia ya Kiingereza, fonolojia ya Kiha, fonolojia ya Kihehe, na fonolojia ya Kibena.
1.1 USULI WA TAALUMA YA FONOLOJIA
Neno fonolojia linatokana na maneno mawili ya Kigiriki phone-sauti za kusemwa na logos- taaluma/mtalaa.
Masimulizi yanadai kuwa taaluma hii ilianza zamani sana kati ya mwaka 520460 kabla ya Masihia) huko India ya kale, ambapo mtu aliyeitwa Panini, na ambaye huaminika kuwa ni baba wa isimu aliandika kuhusu fonolojia ya Kisansikriti katika matini aliyoiita Shiva Sutras. Ni katika andiko hili ndipo alipobainisha kuwepo kwa dhana ambazo leo zinajulikana kama fonimu, mofimu na mzizi.
Baada ya andiko hilo, habari za taaluma ya fonolojia ni kama zilipotea kabisa katika uwanja wa isimu hadi ilipofika karne ya 19 ambapo wanaisimu wengine waliibuka na kuzungumzia upya masuala ya fonolojia. Miongoni mwa wanaisimu wa mwanzo wanaotajwa kujihusisha na fonolojia ni Mpolandi Jan Baudouin de Courtenay (pamoja na mwanafunzi wake wa zamani Nikołaj Kruszewski) alipobuni neno fonimu mnamo mwaka 1876, na kazi yake, ijapokuwa hairejelewi sana, inachukuliwa kuwa ni mwanzo wa fonolojia mamboleo. Mwanaisimu huyu si tu alishughulikia nadharia ya fonimu, bali pia vighairi vya kifonetiki (ambavyo leo huitwa alofoni na mofofonolojia). Maandishi ya Panini (Sarufi ya Kisanskriti) pamoja na Jan Baudouin de Courtenay yalikuja kuwa na athari kubwa kwa anayeaminika kuwa baba wa nadharia ya Umuundo Mamboleo, Ferdinand de Saussure, ambaye pia alikuwa ni profesa wa Sansikriti.
Wanaisimu wote hawa walikuwa wanajaribu kulinganisha sauti za lugha za Asia Mashariki  na za Ulaya, lengo lao likiwa ni kujua mizizi ya lugha zilizoitwa India-Ulaya. Kutokana na mkabala huo, katika kipindi hicho isimu ilikuwa Isimu-linganishi tu. Kutokana na utafiti wao huo waliweza kupata maneno yenye sauti na maana zilizolingana, kufanana au kukaribiana. Utafiti huo uliweza kugundua jamii mbili za lugha ambazo ni jamii ya lugha za Kirumi na jamii ya lugha za Kijerumani. Baadhi ya wanaisimu mahususi kabisa wanaokumbukwa kuchangia katika maendeleo ya fonolojia ni pamoja na:
(i) Jan Baudouin de Courtenay (1845-1929)
Kama ilivyoelezwa hapo awali, huyu ni mwanaisimu aliyebuni dhana za foni na fonimu. Katika nadharia yake, alidai kuwa sauti za mwanadamu ni za aina mbili—foni na fonimu.  Alisema kuwa foni ni sauti za kutamkwa tu lakini fonimu ni sauti za lugha. Hata hivyo, Jan Baudouin de Courtenay hakutumia istilahi za foni na fonimu (kama zinavyotajwa sasa) bali alitumia istilahi za anthrophonics—foni na psychophonics—fonimu. Yeye alidai kuwa foni zipo karibu sana na taaluma ya kumuelewa binadamu pamoja na alasauti zake ambazo kwa hakika hutofautiana sana na za wanyama wengine. Na kuhusu fonimu, alidai kuwa zinahusu kumwelewa binadamu pamoja na akili zake na namna anavyofikiri katika akili yake. Alidai kuwa, mara nyingi, binadamu hupokea kinachotamkwa na kufasiliwa.

(ii) Ferdinand de Saussure (1887-1913)
Ni mwanaisimu wa Kiswisi anayejulikana kama baba wa isimu kutokana na mchango wake alioutoa katika taaluma hii. Yeye anakumbukwa zaidi kutokana na uwezo wake wa kutofautisha dhana alizoziita langue—mfumo wa lugha mahsusi na parole—matamshi ya mzungumzaji wa lugha husika. Langage hufafanuliwa kuwa ni uwezo alionao mzungumzaji wa lugha mahususi wa kuzungumza na kuelewa matamshi ya mzungumzaji mwingine wa lugha hiyohiyo. Ni sehemu ya lugha inayowakilisha maarifa kati ya sauti na alama. Ni mfumo wa alama kwa maana ya kiufundi tu. Dai lake la msingi ni kuwa alama inategemea vitu viwili—kitaja na kitajwa—hivyo ili mawasiliano yafanyike, mfumo wa ishara lazima ufahamike na ukubaliwe na wanajamii wote.
Kwa upande wa parole, anadai kuwa ni matendo uneni. Ni namna lugha inavyotamkwa katika hali halisi na mtu mmoja mmoja. Dhana ya parole inalingana na dhana ya performance (utendi) ya Noam Chomsky. Katika lugha, parole ni matamshi tofauti ya sauti moja—alofoni. Wanaisimu wanaonekana kukubaliana na madai ya Saussure kwakuwa inaelekea kuthibitika kuwa hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya kitaja na kitajwa (alama na kinachowakilishwa), bali makubaliano baina ya wazungumzaji wa lugha moja husika ndiyo hutawala.

(iii) Nikolai Trubetzkoy (1890-1939)
Ni miongoni mwa waanzilishi wa taaluma ya fonolojia akichota mizizi ya taaluma ya isimu kutoka katika Skuli ya Prague. Mwanaisimu huyu aliandika misingi ya fonolojia kwa kutumia maarifa yaliyoibuliwa na Ferdinand de Saussure. Ni mtaalamu wa kwanza kufasili dhana ya fonimu. Aliandika vitabu vingi kwa lugha ya Kijerumani, miongoni mwake ni Grundzüge der Phonologie (Principles of Phonology, 1939), ambapo ni katika kitabu hicho ndimo alimotoa fasili ya fonimu pamoja na kubainisha tofauti baina ya fonetiki na fonolojia.
(iv) Noam Chomsky
Huyu ni mwanaisimu wa Kimarekani anayevuma sana kwa mchango wake katika taaluma ya isimu kwa ujumla. Dhana za competence (umilisi) na perfomance (utendi) zimemfanya awe maarufu ulimwenguni. Dhana hizi zinaelezea tofauti baina ya maarifa na udhihirishaji wa maarifa ya mtumiaji wa lugha. Katika fonolojia, Chomsky anakumbukwa kwa ufafanuzi wake wa dhana ya fonimu kwa mtazamo wa kisaikolojia, ambapo anadai kuwa fonimu ni tukio la kisaikolojia, hivyo lipo kichwani mwa mzungumzaji wa lugha.


(v) Daniel Jones (1881-1967)
Ni mwanafonetiki maarufu kabisa wa karne ya ishirini. Ni Mwingereza msomi ambaye alikuwa na shahada ya kwanza ya hisabati na shahada ya mahiri ya sheria, shahada ambazo hata hivyo, hakuwahi kuzitumia. Baadae, alisomea lugha na kuhitimu shahada ya azamivu. Daniel Jones alifunzwa fonetiki na maprofesa mbalimbali, japokuwa aliathiriwa zaidi na Paul Passy na Henry Sweet. Hamu yake kuu ilikua kwenye nadharia ya fonetiki. Anafahamika zaidi kwa ufafanuzi wa dhana ya fonimu kwa mtazamo wa kifonetiki.   
UJITOKEZAJI WA FONOLOJIA
Fonolojia hujitokeza kwa namna mbili:
  1. Fonolojia kama kiwango cha lugha, kinachoshirikiana na viwango vingine vya lugha (isimu maumbo, isimu miundo, isimu maana katika kuijenga lugha husika.
  2. Fonolojia kama taaluma ambayo huchunguza sauti (fonimu) katika lugha mahsusi.
MALENGO YA FONOLOJIA
1.      Kutambua na kuorodhesha sauti (fonimu) za lugha mahususi.
2.      Kuchunguza mfuatano wa sauti (fonimu) unaokubalika katika lugha. Kwa mfano katika Kiswahili (KI, KKI) n.k.
3.      Kuchunguza mifanyiko ya kifonolojia inayotokana na sauti kuathiriana na nyingine zinapokaribiana katika kuunda vipashio vikubwa hususan, maneno.
4.      Kuchunguza sifa za kiarudhi zinazoathiri vipashio vya lugha ambavyo ni vikubwa kuliko fonimu.
MATAWI YA TAALUMA YA FONOLOJIA
1.      Fonolojia Vipande Sauti (segmental phonology)
2.      Fonolojia Arudhi (prosodic phonology)
3.      Fonolojia asilia zalishi (natural generative phonology)
4.      Fonolojia atomiki (atomic phonology)
5.      Fonolojia leksika (lexical phonology)
6.      Fonolojia mizani (metrical phonology)
7.      Fonolojia umbo upeo (optimality phonology)
8.      Fonolojia vipambasauti (prosodic phonology)
9.      Fonolojia vipandesauti huru (autosegmental phonology)
10.  Fonolojia zalishi (genarative phonology)

1.      FONOLOJIA VIPANDE SAUTI
Ni tawi linalochunguza vitamkwa (sauti) katika lugha husika. Mambo yanayoshughulikiwa katika tawi hili la fonolojia
-          Uainishaji wa sauti katika lugha fulani (fonimu na alofoni zake)
-          Ufafanuzi wa sauti hizo kwa kutumia sifa bainifu.
-          Kueleza jinsi sauti hizo zinavyoathiriana wakati zinapokaribiana na sauti nyingine katika uundaji wa maneno. Massamba (2016) anaeleza maana ya fonolojia vipandesauti kuwa ni mtazamo wa kinadharia katika uchunguzi na uchanganuzi wa mfumo wa sauti za lugha asilia ambao huchambua taratibu za usemaji kwa kuzingatia sauti dhahiri na pambanuzi, k.m fonimu.

3

2.      FONOLOJIA ARUDHI
Hili ni tawi linalochunguza sifa za kiarudhi ambazo huathiri vipashio vikubwa kuliko fonimu na alofoni zake. Baadhi ya sifa za kiarudhi ambazo huchunguzwa na tawi hili ni: mkazo, kidatu, kiimbo, toni na wakaa.
3.      FONOLOJIA ASILIA (natural phonology)
Ni mtazamo wa kinadharia katika uchanganuzi wa mfumo wa sauti za lugha ambao husisitiza umuhimu wa kuzingatia taratibu asilia za usemaji wa lugha. Lengo ni kuchunguza sheria, kanuni, michakato na taratibu mbalimbali zinazojitokeza katika lugha zote za ulimwengu na ambazo hazinabudi kufuatwa katika uchanganuzi wa fonolojia ya lugha.
4.      Fonolojia asilia Zalishi (natural generative phonology)
Mtazamo wa kinadharia katika uchanganuzi wa mfumo wa sauti za lugha asilia ambao unasisitiza kuwepo kwa uhusiano wa moja kwa moja baina ya uwakilishwaji wa maumbo mbalimbali ya ndani (pamoja na sheria zinazoendana nayo) na yale ya nje.

5.      Fonolojia Atomiki (atomic phonology)
Mtazamo wa kinadharia katika uchanganuzi wa mfumo wa sauti za lugha asilia ambao unalenga kuonyesha masharti ambayo hayawezi kukiukwa katika matumizi ya sheria. Masharti hayo huchukuliwa kuwa sheria atomiki zinazotumika katika michakato ya kifonolojia.
6.      Fonolojia leksika (lexical phonology)
Mtazamo wa kinadharia katika uchanganuzi wa mfumo wa sauti za lugha ambao kwao baadhi ya sheria za kifonolojia huhamishiwa katika sehemu ya leksika na kuwa sehemu ya mofolojia.


7.      Fonolojia Mizani (Metrical Phonology)
Mtazamo wa kinadharia katika uchanganuzi wa mfumo wa sauti za lugha ambao umekitwa katika mfumo wa sauti za lugha kama kitu ambacho kimejengeka kimsonge kwa kufuata msingi wa silabi lakini chenye uhusiano wa viwango tofauti kati ya vipengele vyake.
8.      Fonolojia umbo upeo (optimality theory)
Mtazamo wa kinadharia katika uchanganuzi wa mfumo wa sauti za lugha ambao umekitwa kwenye madai kwamba miundo mbalimbali ya lugha hutokana na mashartizuizi ya kimajumui yaliyomo katika lugha za binadamu. Madai haya nayo yamekitwa kwenye mtazamo kwamba tofauti zinazojitokeza katika lugha za binadamu hutokana na tofauti za uthamini wa mashartizuizi hayo.
9.      Fonolojia Vipambasauti
Mtazamo wa kinadharia katika uchanganuzi wa sauti za lugha asilia wa vipengele ambavyo huvuka mipaka ya vipandesauti; yaani vipashio kama toni, mpandoshuko, lafudhi, kidatu, mkazo na tempo.
10.  Fonolojia vipandesauti huru (autosegmental phonology)
Mtazamo wa kinadharia katika uchanganuzi wa mfumo wa sauti za lugha asilia ambao umekitwa katika msingi kwamba kila kipandesauti (kitamkwa, mkazo, toni, n.k.) hujitegemea na huwa katika rusu yake chenyewe (si sehemu ya kingine).
11.  Fonolojia Zalishi (generative phonology)
Mtazamo wa kinadharia katika uchanganuzi wa mfumo wa sauti za lugha asilia ambao nia na lengo lake ni kujaribu kubainisha sheria na kanuni za kimajumui zinazohusisha umbo ndani na umbo nje la mfumo wa sauti.


12.  Fonolojia zalishi asilia (natural generative phonology)
Ni mtazamo wa kinadharia katika uchanganuzi wa mfumo wa sauti za lugha asilia ambao unaamini kwamba wasemaji wa lugha yoyote iwayo, katika usemaji wao huwa wanajikita katika majumuisho ambayo yanadhihirika katika  kinahosemwa na kuleta uangavu wa kilichokusudiwa.
FONETIKI NA FONOLOJIA
Fasili ya taaluma ya fonolojia haiwezi kukamilika, na pengine kueleweka, iwapo hakuna linalosemwa kuhusiana na taaluma ya fonetiki. Hali hii inatokana na ukweli kuwa kuna uhusiano wa kinasaba kati ya fonolojia na fonetiki. Massamba na wenzake (2004:5) wananeneleza ukweli huu kwamba:
fonetiki na fonolojia ni matawi mawili tofauti ya isimu lakini yenye kuhusiana sana. Uhusiano wa matawi haya unatokana na ukweli kwamba yote mawili yanajihusisha na uchunguzi na uchambuzi unaohusu sauti za lugha za binadamu.

Kutokana na ukweli huu, jitihada za kufasili dhana ya fonolojia inaelekea kuwa nyepesi, dhana hizi mbili zinapofasiliwa kwa mlinganyo. Tuanze na fonetiki:
1.1   FONETIKI NI NINI?
Kwa mujibu wa Hyman (1975) fonetiki ni taaluma ambayo huchunguza sauti ambazo hutumiwa na wanadamu wakati wanapowasiliana kwa kutumia lugha. Uchunguzi wa kifonetiki huwa hauhusishwi na lugha yoyote mahususi na kutokana na hali hiyo kipashio cha msingi cha fonetiki ni foni. Hyman anaendelea kueleza kuwa foni ni kipande kidogo kabisa cha sauti kisichohusishwa na lugha yoyote.
Kindija (2012:2) anaeleza maana ya fonetiki kuwa ni neno lenye asili ya lugha ya Kigiriki. Limeingia katika Kiswahili kutokana na neno la Kiingereza ‘phonetics’ na likichambuliwa linaonesha kuwa lina maneno mawili, yaani fon-etiki. ‘Fon –“sauti” na ‘etiki---- ina maana ya taaluma ya” Hivyo basi fonetiki ni taaluma ya sauti za lugha za binadamu.
Matinde (2012: 43) anafafanua kuwa neno “fonetiki” hutokana na neno la Kigiriki “phonetica” ambalo limeundwa na  maneno mawili “phone” (sauti) na “tic” (uchunguzi). Hivyo basi, fonetiki ni taaluma ya isimu inayochunguza foni (sauti zote zinazotamkwa na binadamu ambazo hazihusishwi na lugha maalumu). Fonetiki huchunguza mifanyiko ya kifizikia inayoambatana na utamkaji wa sauti mbalimbali katika upekee wake au mfululizo wake. Anaendelea kufafanua kuwa fonetiki kwa upekee wake huchunguza sifa za kifonetiki za kila sauti inayojitokeza katika lugha za binadamu.
Naye Massamba na wenzake (2013:5) wanafafanua maana ya fonetiki kuwa ni tawi ambalo hujishughulisha na uchambuzi wa taratibu zote zinazohusiana na utoaji, utamkaji, usafirishaji, usikiaji na ufasili wa sauti za lugha za binadamu kwa ujumla. Kinachozingatiwa hapa ni kuchunguza maumbo mbalimbali ya sauti zinazoweza kutolewa na alasauti, namna maumbo hayo yanavyoweza kutolewa, yanavyoweza kumfikia msikilizaji na yanavyofasiliwa na ubongo; bila kujali sauti hizo zinatumika katika lugha gani.
Massamba (2016:16) anaeleza maana ya fonetiki kuwa ni tawi la isimu ambalo hujishughulisha na uchambuzi na uchanganuzi wa sauti za lugha za binadamu, usikiaji na utamkaji wake.
Hata hivyo ni jambo la wazi kuwa sauti tunayoifikiria katika fonetiki siyo cheko, wala kohozi, kwikwi, chafya n.k pamoja na kuwa mambo haya huingia katika mazungumzo, huwa hayatumiki kwa kuwasilisha ujumbe (mbali na ule ujumbe wa kwamba mtu ana furaha, mafua n.k.) Ni kwamba tunaposikiliza mazungumzo, siyo tu kwamba tunaweza kutenganisha maneno yanayosemwa, bali kila neno tunaweza kuligawa katika silabi zake, na kila silabi tukaigawa katika “vitamkwa/ sauti zake. Kwa mfano, maneno “≠k/a$mb/a ≠y/a$/ng/u”≠. Aidha, kumbuka kwamba neno hujengwa na vitamkwa na siyo herufi. Herufi ni mwakilisho tu wa vitamkwa. Kitamkwa kilekile kinaweza kuwakilishwa na herufi tofauti katika lugha mbalimbali.
Vitamkwa ndivyo vinavyoshughulikiwa na taaluma ya sauti (fonetiki). Katika taaluma hii, tunajadili masuala kama vile; Ni ala zipi katika maungo ya binadamu hutumika katika utoaji wa vitamkwa? Je, vitamkwa hivyo ni vya aina ngapi na vinatolewaje? Kwa kusisitiza fonetiki hushughulikia kila aina ya vitamkwa vinavyoweza kutolewa na ala za matamshi za mwanadamu, hata kama baadhi ya vitamkwa hivyo havitumiki katika lugha fulani, kama vile katika Kiswahili. Ukweli ni kwamba, kitamkwa kisichopatikana katika Kiswahili huweza kupatikana katika lugha nyingine. Sauti zinazoshughulikiwa katika fonetiki huitwa FONI.
Fonetiki ni taaluma pana na imejigawa katika nyanja kadhaa. Zifuatazo ni baadhi tu ya Nyanja hizo.
(a)    Fonetiki matamshi
(b)   Fonetiki akustika
(c)    Fonetiki majaribio
(d)   Fonetiki masikizi na
(e)    Fonetiki tibamatamshi
(i)                 FONETIKI MATAMSHI (articulatory phonetics)

Massamba na wenzake (2004, 2007, 2013) wanaeleza maana ya fonetiki matamshi kuwa ni tawi linalojishughulisha na jinsi sauti mbalimbali zinavyotamkwa kwa kutumia zile alasauti.  Hivyo basi, kinachoangaliwa hapa ni jinsi ya utamkaji wa sauti hizo (kama vile sauti za vikwamizi), mahali pa matamshi pa sauti hizo (kama ni ufizi) na hali ya mkondo hewa (kama ni ghuna au sighuna). Mgullu (2008) anaeleza kuwa tawi la fonetiki matamshi linajishughulisha na ala za matamshi, mahali pa kutamkia, namna ya kutamka, mikondo hewa, aina za vitamkwa (foni), sifa bainifu za foni na unukuzi wa foni.  Kindija (2012:31) kama anavyomnukuu Crystal (1989) anasema kuwa tawi hili hujulikana pia kama ‘fonetiki fiziolojia’ “fiziolojia ni sayansi inayuhusu utendaji kazi wa viumbe.  Anaendelea kueleza kuwa katika fonetiki matamshi, sauti zinaainishwa kufuatana na vigezo vikuu viwili
-          Mahali zinapotamkiwa- yaani ni ala zipi zinatumika katika utoaji wa sauti hizo.
-          Jinsi sauti hizo zinavyotamkwa- yaani kunatokea nini wakati hewa inatoka mapafuni kupitia kwenye bomba la hewa, kupitia kwenye glota, mpaka kufikia kwenye mkondo sauti.
-           

(ii)                  FONETIKI AKUSTIKA (Acoustic phonetics)
Matinde (2012) anasema kuwa fonetiki akustika (pia fonetiki mawimbi) ni tawi la fonetiki ambalo huchunguza na kufafanua sifa za kifonetiki za sauti baada ya kutamkwa na kabla ya kuingia masikioni mwa msikilizaji. Tawi hili huchunguza na kubainisha jinsi mawimbi ya sauti za lugha yanavyosafiri kutoka kinywa cha msemaji hadi sikio la msikilizaji.

Kwa upande wa Massamba (2016:16) fonetiki akustika ni tawi la fonetiki ambalo hujishughulisha na uchunguzi wa namna sauti za lugha zinavyosafiri kutoka kwa msemaji hadi kwenye sikio la msikilizaji. Aghalabu uchunguzi na uchanganuzi huu huhitaji matumizi ya vifaa vya kielektroniki.

(iii)                FONETIKI MASIKIZI (auditory phonetics)
Kindija (2012: 19) anaeleza kuwa fonetiki masikizi ni tawi dogo la fonetiki linalohusu uchunguzi na uchanganuzi wa namna sauti za lugha zinavyokamatwa na sikio zikasafirishwa kwenda kwenye ubongo kupitia neva zinazohusika na usikiaji. Anaendelea kufafanua kuwa mawasiliano kwa njia ya lugha ni upitishaji wa mawazo au hisia kutoka katika akili ya msemaji hadi katika akili ya msikilizaji. Hili ni tawi la fonetiki linaloshughulikia jinsi mawimbi sauti yanavyoingia katika sikio la msikilizaji na kutafsiriwa na ubongo wake hata kupata maana.

Kwa upande wa Massamba (2016:16) fonetiki masikizi ni tawi dogo la fonetiki linalohusu uchunguzi na uchanganuzi wa namna sauti za lugha zinavyokamatwa na sikio zikasafirishwa kwenda katika ubongo kupitia neva zinazohusika na usikiaji. Kwa ujumla, fonetiki masikizi ni tawi la fonetiki ambalo hujishughulisha na jinsi utambuzi wa sauti mbalimbali za lugha unavyofanywa, na uhusiano uliopo baina ya sikio, neva masikizi (yaani neva zinazohusika na usikiaji wa sauti) na ubongo.


(iv)               FONETIKI TIBA MATAMSHI (speech pathology)
Tawi hili linaitwa hivyo kwa mujibu wa Massamba na wenzake (2004) wakati Mgullu (1999) analiita fonetiki majaribio, nalo linashughulikia matatizo yanayoambatana na usemaji na jinsi ya kuyatatua.  Massamba (2016:17) anaeleza kuwa fonetiki tibamatamshi ni tawi linalohusu uchunguzi na uchanganuzi wa matatizo ya utamkaji wa sauti za lugha za binadamu na jinsi ya kuyarekebisha. Tawi hili ni jipya na limeibuka hivi karibuni. Katika kozi yetu tutajikita zaidi na tawi moja tu la fonetiki ambalo ni fonetiki matamshi.


FONETIKI MATAMSHI.
► Kwa ujumla, fonetiki si taaluma ya kinadharia, ni taaluma ya ‘utendaji’, na hivyo ni lazima mafunzo yake yaandamane na mazoezi ya utamkaji na usikilizaji.

ALA ZA SAUTI NA MFUMO WA SAUTI
Fonetiki matamshi ni tawi linaloshughulikia jinsi sauti zinavyotolewa na ala za sauti/matamshi.
ALA ZA SAUTI/ ALA ZA MATAMSHI
Kindija (2012:33) anaeleza kuwa sauti hutamkwa wakati ambapo viungo mbalimbali vya mwili vinaathiri mkondohewa unaoingia au kutoka mapafuni kupitia kinywani au puani au kote kuwili kinywani na puani. Anaendelea kueleza kuwa viungo vya mwili vinapofanya kazi ya utoaji wa sauti huitwa ala za matamshi au alasauti. Ala hizi ni kama vile mapafu, kongomeo, koo, ulimi, paa la kinywa (na sehemu zake kama vile kilimi, kaakaa, na ufizi), meno, midomo, na pua.

Mgullu (2010) anaeleza maana ya ala sauti kuwa ni viungo vya mwili wa mwanadamu ambavyo huhusika katika utamkaji. Kuhusika huku kunaweza kuwa kwa moja kwa moja au usio wa moja kwa moja. Mwanadamu anapozungumza hutumia viungo vya mwili ambavyo ndivyo uitwa ala za sauti au ala za matamshi.



UTAMKAJI WA SAUTI ZA LUGHA
Sauti za lugha ya mwanadamu hutamkwa pale ambapo viungo mbalimbali vya mwili wa binadamu hutatiza hewa inayoingia na kutoka mapafuni kupitia ama chemba ya pua au chemba ya kinywa. Viungo hivi vya mwili wa binadamu huitwa ala za sauti.

AINA ZA ALA ZA SAUTI


Ala za sauti zimegawanyika katika makundi makuu mawili ambayo ni:
(a)    ALA TULI (Passive  speech organs)
Hizi ni zile ambazo huwa zimetulia tu hazisogeisogei wakati mtu anapozungumza. Kwa mfano, ufizi, kaakaa gumu, kaakaa laini, meno n.k.

(b)    ALA SOGEZI (Active speech organs)
Hizi ni zile alasauti ambazo husogeasogea wakati mtu anapozungumza. Kwa mfano, ulimi na midomo n.k.

(i)      MIDOMO:
Mwanadamu wa kawaida ana midomo miwili, yaani mdomo wa juu na mdomo wa chini. Midomo hushiriki kiasi cha kutosha katika utamkaji wa vitamkwa vya lugha. Miongoni mwa sauti za midomo ni: [m], [p], [b], [β] n.k.

(i)                 MDOMO-MENO-
Sauti zinazotamkwa hapa zinahusisha mdomo wa chini na meno ya juu. Mdomo wa chini huwa ala sogezi na husonga kuelekea meno ya juu ambayo ni ala tuli. Mfano, [f], [v] n.k.

(ii)               MENO:
 Meno ni miongoni mwa ala tuli nayo huhusika wakati wa kutamka sauti fulani fulani. Aidha, vitamkwa vinavyotamkiwa kwenye meno huitwa foni za meno. Wakati wa kutamka foni hizi ulimi huwekwa katikati ya meno ya chini na ya juu na hususani huwa umeyagusa meno ya juu. Mfano wa foni hizi ni kama vile: [θ] na [ dh ].

(iii)             UFIZI:
Hizi ni ala ambazo zinashikilia meno ya juu na ya chini.  Wakati wa utamkaji wa sauti hizi ncha ya ulimi hugusa ufizi. Baadhi ya sauti za ufizi ni: [f], [v], [θ], [dh], [š] n.k.


(iv)             KAAKAA GUMU:
Hii ni sehemu inayopakana na ufizi. Wakati wa utamkaji wa sauti hizi sehemu ya kati ya ulimi hugusa kaakaa gumu. Mfano wa sauti zinazotamkwa katika kaakaa gumu ni: [ch] [j] na [J].

(v)               KAAKAA LAINI:
Hii ni sehemu tuli inayopakana na kaakaa gumu. Wakati wa kutamka sauti hizi sehemu ya kati ya ulimi huinuliwa hadi kukaribia kugusa kaakaa laini. Baadhi ya sauti zinazotakwa katika kaakaa laini ni: [γ], [k], [g], [η], [X] N.K.

(vi)             ULIMI:
Hii ni ala ya msingi sana ya sauti na husaidia utamkaji wa sauti nyingi sana. Irabu zote hutegemea ala hii ya sauti katika utamkaji wake. Kwa mfano [i], [u], [a], [e] na [o]. Sehemu mbalimbali za ulimi zinaweza kutumika kutoa aina mbalimbali za sauti za lugha. Sehemu hiyo inaweza kuwa ni sehemu ya mbele ya ulimi, sehemu ya kati ya ulimi au sehemu ya nyuma ya ulimi. Sauti hizi zinaweza kuzalishwa wakati ulimi ukiwa umeinuliwa juu, upo kati au upo chini.
(vii)           NYUZI ZA SAUTI:
Nyuzi sauti pia zina mchango mkubwa sana katika utoaji wa sauti. Zinapotikiswa hutoa mghuno na hivyo hutoa sauti ziitwazo ghuna na zisipotikiswa hazitoi mghuno na hivyo hutoa sauti ziitwazo sighuna. Baadhi ya sauti ghuna ni kama vile: [b], [m], [g], [d], [r] n.k. na baadhi ya sauti sighuna katika lugha ya Kiswahili ni: [p], [s], [k] n.k
(viii)         CHEMBA YA PUA:
 Alasauti hii hutoa sauti ziitwazo nazali. Wakati wa utamkaji wa sauti hizo hewa hupitia katika chemba ya pua. Sauti hizo ni kama [m], [n], [η], [ny] n.k.
(ix)              KOROMEO:
Ni chemba iliyo kati ya kilimi na kongomeo. Sauti zinazotamkiwa hapa hutolewa kwa kulivuta shina la ulimi nyuma na kulielekeza kwenye ukuta wa nyuma ya koo. Hakuna sauti za lugha ya Kiswahili zinazotamkiwa katika sehemu hii. Mfano, [ћ] [ћamma:m] ‘oga’ (Kiarabu).


(x)               SAUTI ZA GLOTA:
 Hii ni sehemu ya mwisho kabisa ambayo ni uwazi uliopo kati ya nyuzi sauti zilizopo katika kongomeo. Uwazi huu hubadilika kutegemea na kinachotamkwa (hubadilikabadilika katika utamkaji wa sauti mbalimbali). Mfano wa sauti ya glota ni [h].

UTAMKAJI NA UBAINISHAJI WA MAKUNDI ASILIA YA SAUTI
Katika utamkaji kwa kawaida huwa tunatumia vitamkwa. Vitamkwa hivi huwakilishwa na herufi kama vile; l, m, b, p n.k. Herufi hizi huwa ni viwakilishi tu vya sauti halisi zinazotolewa na ala za sauti. Aidha, herufi hizi ni za kinasibu tu na wala hazina uhusiano wa moja kwa moja na pale tunapoona aina tofautitofauti ya herufi zinazotumiwa na lugha mbalimbali duniani kuwakilisha sauti hizo, kwa mfano, herufi za Kichina, Kiswahili, Kihindi na Kijapani n.k. Hivyo basi, kitu cha muhimu hapa si herufi bali ni sifa zinazojenga vitamkwa husika. Sifa hizo zimegawanywa katika makundi matatu kama wanavyoainisha Chomsky na Halle (1968) katika SPE. Sifa hizo ni irabu, konsonanti na viyeyusho.
A.    IRABU
Hii ni sauti ambayo wakati wa utamkaji wake, mkondohewa hauzuiwi na pia nyuzi sauti hurindima. Hii ina maana ya kwamba irabu zote ni ghuna. Kuna irabu za aina nyingi sana duniani lakini katika kozi hii tutajikita zaidi na irabu za Kiswahili na za lugha za Kibantu. Kimsingi kuna makundi mawili ya irabu katika lugha ambazo tutazivinjari. Lugha zenye irabu saba na kundi la pili ni lile la lugha zenye irabu tano
LUGHA ZENYE IRABU SABA
Kundi hili lina lugha nyingi sana za Kibantu kama vile; Kisukuma, Kinyakyusa, Kihaya na Kinyambo, Kimatengo, Kindendeule.
Maandishi ya kawaida                                                          Maandishi ya kifonetiki
i                                                                                   [i]
e                                                                                  [I]
e                                                                                  [ε]
a                                                                                  [a]
o                                                                                  [ )]
o                                                                                  [u]
u                                                                                  [u]
LUGHA ZENYE IRABU TANO
Kundi hili lina lugha chache sana kwa mfano, Kiswahili, Kizigula, Kilugulu n.k.
Maandishi ya kawaida                                    Maandishi ya kifonetiki
i                                                                   [i]
e                                                                  [ε]
a                                                                  [a]
o                                                                  [)]
u                                                                  [u]
MWAINISHO WA IRABU
Irabu huainishwa kwa kutumia vigezo vikuu vitatu: mahali pa matamshi, mwinuko wa ulimi na hali ya mdomo.
MAHALI PA MATAMSHI/KUTAMKIA
Irabu zinaweza kutamkwa katika sehemu tatu za ulimi: sehemu ya mbele ya ulimi, sehemu ya kati ya ulimi na sehemu ya nyuma ya ulimi.


UHUSIANO KATI YA FONETIKI NA FONOLOJIA
Na
Fonetiki
Fonolojia
1.
Huchunguza sauti za kutamkwa na binadamu
Huchunguza sauti za kutamkwa na binadamu
2.
Ni pana (huchunguza sauti nyingi)
Ni finyu (huchunguza sauti chache tu)
3.
Ni kongwe
Ni changa
4.
Huchunguza sauti pekepeke
Huchunguza sauti katika mfumo
5.
Huchunguza sauti kwa ujumla
Huchunguza sauti za lugha mahususi, k.m. Kiswahili, Kiha, na Kinyiramba.
6.
Kipashio cha msingi ni foni
Kipashio cha msingi ni fonimu

UHUSIANO WA FONOLOJIA NA MATAWI MENGINE YA ISIMU
Fonolojia kama tawi mojawapo la isimu fafanuzi ina uhusiano na matawi mengine ya isimu, kwa mfano fonolojia na fonetiki zote zinahusika na sauti za lugha. Pia kimbile chao ni kimoja yaani zote hufafanua sauti za lugha. Tofauti yake ipo katika mkabala.
TOFAUTI KATI YA FONOLOJIA NA FONETIKI
► Fonolojia inategemea uchunguzi uliofanywa na fonetiki wakati fonetiki haitegemei sana fonolojia.
► Fonetiki inachunguza sauti kama zilivyo.
► Fonolojia inachunguza sauti na maathiriano katika lugha fulani.
► Fonetiki ina seti kubwa ya sauti wakati fonolojia ina seti ndogo ya sauti ambayo ni sehemu ya seti ya fonetiki.
► Seti ya fonolojia ina kikomo wakati seti ya fonetiki haina kikomo. Inasemekana kuwa lugha nyingi duniani hutumia wastani wa sauti kati ya ishirini na arobaini tu. Kwa mfano lugha ya Kiswahili ina sauti 31.
► Fonetiki ipo moja lakini fonolojia ni nyingi  kama lugha zilivyo nyingi. Hivyo kila lugha ina fonolojia yake ambayo ni tofauti na fonolojia ya lugha nyingine
► Kipashio cha msingi katika fonetiki ni FONI wakati katika fonolojia ni FONIMU.
► Katika fonetiki sifa bainifu za foni hubainishwa wakati katika fonolojia tunabainisha sifa bainifu za FONIMU.
● Kwa ujumla fonetiki na fonolojia hutegemeana na kukamilishana.Uchunguzi na uchambuzi wa kifonetiki husaidia sana uchambuzi wa kifonolojia na vilevile uchambuzi wa kifonolojia husaidia uchambuzi wa kifonetiki. Hata hivyo fonetiki ni msingi imara ambao husaidia katika uchambuzi wa kifonolojia. Kwa upande mwingine fonetiki huzipata foni zote kutoka lugha mbalimbali, yaani kutoka fonolojia za lugha mbalimbali. Kwa maneno mengine tunaweza kusema kwamba kama hapangekuwepo hizo fonolojia za lugha mbalimbali basi wanafonetiki hawangekuwa na kitu cha kuchunguza.
UHUSIANO KATI YA FONOLOJIA NA MOFOLOJIA
MOFOLOJIA
► Ni taaluma inayochunguza maumbo ya maneno katika lugha yaani namna neno linavyoundwa.
Kipashio chake cha msingi ni MOFIMU ambacho hakiwezi kugawanyika mara mbili na kuleta maana ya kileksika ama kisintaksia, kwa mfano
Mama
●Mofimu leksika/huru
m/toto
●m- ni kiambishi cha idadi
●toto mofimu ya mzizi
UHUSIANO
►Taaluma zinahusika na lugha mahsusi/maalumu
► Mofimu ambazo ni vipashio vya msingi huundwa na fonimu.
► Mofimu moja inaweza kuwa na maumbo mbalimbali→ALOMOFU
Kwa mfano
Mtoto, muuguzi, mwalimu
Kuna m, mu, mw ambazo ni mofimu za umoja nazo ni alomofu za mofimu  ngeli ya kwanza umoja. (YUAWA).
►Fonimu ni kipande tu cha sauti yaani umbo la kitamkwa kimoja wakati mofimu yaweza kuwa umbo la silabi, mofimu au neno.
UHUSIANO KATI YA FONOLOJIA NA SINTAKSIA
Sintaksia ni taaluma ihusikayo na mpangilio wa maneno katika tungo. Kipashio cha msingi katika sintaksia ni neno. Kipashio cha juu katika sintaksia ni SENTENSI. Aidha sentensi huundwa kwa maneno yaliyoundwa na mofimu. Maneno hayo pia huunda kirai+kishazi+sentensi.
Kuna kanuni za kifonolojia zinazotawala miundo ya tungo hizo.
  1. Neno lazima likubaliane na mpangilio wa silabi na fonimu
  2. Kuna kanuni fulani zitumikazo ili kupata muundo fulani wa maneno, kwa mfano
Mke wake mkewe. Uunganishaji na udondoshaji ni kanuni za kifonolojia.


UHUSIANO KATI YA FONOLOJIA NA SEMANTIKI
Semantiki ni taaluma inayohusika na maana.
Fonimu ni vipande vya sauti msingi katika fonolojia ambavyo maana zake lazima zitumike katika mfumo mzima wa lugha . Na ndizo zinazobadili maana nzima ya maneno katika lugha kwa mfano kata, kaba ndizo zinazotuletelea kupata maana tofauti za maneno hayo kwa kuzingatia mpangilio fulani ulio maalumu. Hivyo basi tukijua maana za maneno katika lugha ni rahisi kutambua fonimu za maneno katika lugha husika.
UHUSIANO KATI YA FONOLOJIA NA MATAWI MENGINE YA ISIMU
ISIMU JAMII
► Tawi hili huangalia matumizi ya lugha na jamii zinavyohusiana, kujua hisia utamaduni wa jamii na kubalidi msimbo kwa mfano kwa nini lugha inakufa. Uhusiano wake na fonolojia upo katika utofauti kati ya wazungumzaji wa eneo katika matamshi.
ISIMU HISTORIA
► Tawi hili huangalia mabadiliko ya sauti yaani sauti fulani ilivyobadilika toka awali na kuendelea.
ISIMU SAIKOLOJIA
► Huangalia jinsi mtu apatavyo (aamiliavyo) lugha, jinsi motto anavyoanza kuamili lugha. Pia inaangalia kuwa lugha ipo kwenye ubongo . Sauti za kwanza ambazo ni msingi katika lugha husika. Vilevile huonesha mambo yanayoweza kumzuia au kumkabili mtu kutoa sauti fulani.
NADHARIA YA FONIMU
Fonimu ni kipande kidogo kabisa katika mfumo wa sauti za lugha ambacho hutofautisha vitamkwa vinavyokinzana. Dhana ya fonimu ilitokana na nadharia ya wanamuundo “nadharia ya fonimu”. Kwa mujibu wa Jones (1957) istilahi ya fonimu iliundwa na Baudouin de Courtenay ambaye alitumia neno Ki-Rusi ‘fonema’ kama istilahi. Lakini Firth (1957:1) anadai kwamba de Courtenay aliiazima istilahi hiyo ya ‘fonema’ kwa mwanafunzi wake Kruszewiski ambaye aliitumia katika insha yake iliyokuwa na mada “Athari ya mkazo katika ubadilishanaji wa irabu (guna) katika Rig-Veda iliyoandikwa huko Kazan 1879. Wafuatao ni waasisi wa nadharia ya fonimu:
A.    JAN NIECISLAW BAUDOUIN DE COURTENAY (1845-1929)
Alizaliwa Radzymin huko Poland, alianza kujishughulisha na nadharia ya fonimu 1868. Kwa mujibu wa de Courtenay dhima ya sauti ‘kwa namna lugha ilivyojengwa, katika hisia za watu, haitokei kwa namna sawa na umbo lake linalotamkwa; na kwa kuwa haya yanaelekea kuwa maumbo mawili yanayojitegemea kutofautisha fonimu na sauti za usemaji. Hii ina maana kwamba de Courtenay anaweka wazi tofauti baina ya sauti kama zinavyobainishwa na wasemaji wa lugha (yaani, katika bongo zao) na sauti kama vitu halisi vinavyotamkwa. Naye anadai kuwa kuna mambo mawili yanayochunguzwa katika uchunguzi na uchanganuzi wa mfumo wa lugha kileo: kuchunguza kile kitamkwacho na kuchunguza kile kilichokusudiwa ubongoni mwa msemaji.
Kwa mujibu wa de Courtenay ule uwanja unaoshughulikia sauti za lugha zinazotamkwa na msemaji (uwanja ujulikanao hii leo kama fonetiki) unaitwa ANTHROPOFONIKI na ule uwanja unaoshughulikia sauti kama zinavyokusudiwa katika ubongo wa msemaji (uwanja ujulikanao hii leo kama fonolojia )unaitwa SAIKOFONETIKI. Kutokana na maoni ya de Courtenay SAIKOFONETIKI inahusiana na uwanja wa saikolojia kwa ujumla kwa kusema kuwa ni kipengele kilichokitwa katika uchanganuzi wa sauti katika mtazamo wa mofolojia na uundaji wa maneno. Hii inaelekea kutuambia kuwa saikolojia ni kipengele muhimu sana katika kutofautisha maneno. Kwa namna nyingine hii ni sawa na kusema kuwa de Courtenay alitambua kwamba dhana ya SAIKOFONETIKI ilikuwa imekitwa katika upambanuzi wa sauti. Kwa ujumla de Courtenay alibainisha viwango viwili vya uwakilishi wa sauti: kiwango cha fonetiki (ANTHROPOFONIKI) na kiwango cha fonolojia, ambacho alikiita SAIKOFONETIKI). Alitambua kwamba fonimu zilikuwa na dhima pambanuzi lakini hazikuwa zinawakilisha maana yoyote ile zikiwa peke yake. Aliamini kwamba fonimu, kama kipengele cha kisaikolojia, ilikuwa dhana tata na changamani sana.
B.     FERDINAND DE SAUSSURE
Alizaliwa tarehe 26 Novemba 1857 huko GENEVA, SWITZERLAND na kufariki 22 Februari 1913. Alikuwa mwanafalsafa wa karne ya 19 wa Ki-Swiss aliyejishughulisha sana na isimu zaidi kwenye isimu muundo na semiotiki baadhi ya wanazuoni humwita baba wa isimu ya kileo kutokana na mchango wake mkubwa katika taaluma ambayo hujulikana leo hii kama ISIMU KILEO.
MICHANGO YAKE
-          Kuweka wazi tofauti iliyopo baina ya LANGUE (lugha) na PAROLE (utendaji).
-          Langue ni ile sehemu inayowakilisha welewa wetu wa uhusiano uliopo kati ya sauti na maana. Anaeleza kwamba lugha ni mfumo wa alama. Kwa mujibu wa de Saussure alama ina pande mbili yaani: mtajo/ kitu kinachotaja (significant) na kitajwa (signifie- dhana). Mfumo wa alama ndio ujengao maarifa ya pamoja ya jamiilugha moja ukicha tofauti ndogondogo za watu binafsi katika jamii hiyo.
-          Parole (utendaji katika lugha huhusu usemaji kwa ujumla. Yaani jinsi lugha inavyotumiwa na watu, siyo inavyotumiwa na jamiilugha yote bali inavyotumiwa na msemaji mmojammoja. Aidha, kwa mujibu wa de Saussure dhana ya lugha na utendaji inavuka mipaka ya kifonetiki na kifonolojia. Kwake yeye lugha ni mfumo wa vipengele vyote vinavyohusiana, yaani vipengele vya kileksika, kisarufi na kifonolojia.  Kuhusu fonolojia de Saussure anasema kuwa mwanaisimu anapaswa kujishughulisha zaidi na lugha siyo utendaji. Hivyo basi mwanaisimu kazi yake ni kuchunguza faridi mbalimbali za sauti na sheria zinazotumika katika kuziunganisha ili kujenga mfumo wa lugha.

C.    PRINCE NIKOLAJ TRUBETZKOY (1890-1939)

Wanazuoni wengi, hasa kutoka Shule ya Mawazo  ya Prague, walivutiwa sana na mawazo ya de Saussure, na wakajitahidi sana na mawazo ya de Courtenay na de Saussure na wakajitahidi sana kujaribu kuyaendeleza. Ragba yao kubwa ilikuwa kuiendeleza nadharia ya fonolojia. Alikuwa ni profesa wa filolojia huko Viena Austria. Alibainisha matawi mawili yaliyoshughulikia sauti. Tawi la kwanza ni fonetiki kama sayansi inayoshughulikia sauti katika uumbwaji wake halisi kifiziolojia, kiakustika na kimasikizi.  Tawi la pili ni la fonolojia – sayansi inayoshughulikia uamilifu na utofautishaji wa sauti katika mfumo wa lugha. Lengo kuu la Trubetzkoy ilikuwa ni kutumia nadharia ya de Saussure ya sauti kama mfumo wa alama ili kuiweka wazi zaidi dhana ya fonimu. Isipokuwa kwa namna ya tofauti kidogo na de Saussure, Trubetzkoy aliamini kwamba fonetiki na fonolojia si nyanja zilizotengana kabisa, kwani zilikuwa zinarejeleana. Wanazuoni wa shule ya Mawazo ya Prague ni kwamba wao hawakuichukulia fonimu kama kategoria au kikundi cha sauti tu. Kwao fonimu ilikuwa faridi ya kifonolojia iliyokuwa changamani sana na iliyoweza kujitokeza tu katika mfumo wa sauti. Fonimu ilichukuliwa kuwa faridi iliyokuwa na sifa kadhaa pambanuzi; na kwamba sifa pambanuzi hizo ndizo zilizoipa utambulisho wake kama kipengele muhimu cha lugha. Trubetzkoy anadai kuwa dhana ya upambanuzi inakwenda sambamba na dhana ya ukinzani, kwa maana ya kwamba fonimu inaweza tu kutofautishwa na fonimu nyingine iwapo, na iwapo tu, kuna uhusiano wa kiukinzani baina ya fonimu hiyo na fonimu nyingine.  Ukinzani unachukulia sifa zile, ambazo memba wa ukinzani hutofautiana na zile ambazo memba wake wa ukinzani huchangia. Ukinzani ndicho kiini cha fonimu. Katika mtazamo wake anadai kuwa fonimu zote zina uhusiano wa kiukinzani. Kwa mfano, /p/ inakinzana /b/ pia /k/ na /g/. n.k. Ukinzani unaweza kuainishwa kutegemea na idadi na aina ya sifa pambanuzi ambazo kwazo ukinzani huo umeegemezwa. Fonimu zenye uhusiano wa karibu mara nyingi huunda makundi asilia wakati zile ambazo hazina uhusiano wa karibu haziundi makundi kama hayo.

D.    DANIEL JONES (1881-1967)
Alizaliwa London 1881. Alijifunza ma kuweza kusema lugha kadhaa. Digrii yake ya kwanza ilikuwa katika Hisabati, Digrii ya Umahiri alisomea sheria. Naye alisoma Fonetiki, chini ya maprofesa mbalimbali katika nyakati mbalimbali. Mwanazuoni huyu anaitazama fonimu kama kipengele chenye sura mbili, sura ya kudhihirika kimatamshi na sura ya kudhihirika kisaikolojia. Katika sura ya kisaikolojia fonimu zinaweza kutazamwa kama vijenzi vya kisaikolojia. Fonimu inachukuliwa kuwa ni sauti ya usemaji ambayo taswira yake inaonekana akilini na ambayo imekusudiwa kutolewa katika mchakato wa usemaji. Katika sura ya kudhihirika kimatamshi fonimu ni familia ya sauti zitamkwazo ambazo huhesabiwa kama kitu kimoja. Hata hivyo baadaye Jones alifasili upya fonimu kwa kusema kuwa “fonimu ni familia ya sauti, katika lugha yoyote iwayo, ambazo zinahusiana katika kuumbwa kwake na ambazo hutumika kwa namna ambayo hairuhusu memba yeyote aliyemo katika familia hiyo kutokea katika neno katika mazingira yaleyale ya kifonetiki ambamo memba mwingine hutokea. Kutokana na fasili ya Jones tunapata mtazamo mwingine wa kuifasili fonimu kuwa ‘fonimu ni familia ya sauti tu. Memba wa familia hudhihirika wazi kimatamshi; ila fonimu ndicho kitu pekee yake ambacho hakidhihiriki wazi kimatamshi.  Umoja uwawekao memba katika familia moja ndio ujengao dhana ya fonimu. Katika familia hii ya sauti hakuna memba ambaye anaweza kutokea katika mazingira yaleyale ya kifonetiki ambamo memba mwingine hutokea. Kwa ujumla, memba wa familia ya sauti ni lazima watokee katika msambao kamilishani, ambao unajulikana sana kama Mgawanyo wa kimtoano.

E.     JOHN RUPERT FIRTH (1890-1960)
Alisoma Historia katika Chuo Kikuu cha Leeds. Baadaye alianza kusoma mambo ya lugha. Mwanzoni Firth akiwa chini ya Jones aliikabili nadharia ya fonimu kwa mtazamo karibu sawa na ule wa Jones. Baadaye alibadili mtazamo wake, akaachana na kukazia uamilifu wa fonimu kama kipengele cha kipeke yake; akasisitiza uhusishaji wa uamilifu wa fonimu katika miktadha mbalimbali. Kwa mujibu wa Firth, kuna aina kuu mbili za uamilifu wa vipengele vya fonimu: Uamilifu mdogo na uamilifu mkubwa. Katika uamilifu mdogo kipengele kinajitokeza katika upambanuzi wake kama kitu pekee kikijitofautisha na vipengele vingine, lakini katika uamilifu mkubwa kipengele hicho kinafanya kazi kama kiwakilishi cha kategoria ya kimofolojia.  Firth anadai kwamba katika maneno kama breed [brid] na bred [bred] ukinzani baina ya [i] na [e] hufanya kazi ya kuonyesha upambanuzi wa irabu zote mbili (uamilifu mdogo) na hufanya kazi ya kuonyesha njeo baina ya wakati wa sasa na wakati uliopita (uamilifu mkubwa). Utofauti unaojitokeza kati ya Firth na wanafonolojia tangulizi ni kwamba yeye anaingiza masuala ya kisarufi (mofolojia) katika ufafanuzi wa muundo wa sauti za lugha. Mkabala huu ulipata mashiko katika kazi za wanafonolojia wa miaka ya 1980. Nadharia za Fonolojia Leksika, Fonolojia Vipandesauti Huru na Fonolojia Mizani zimeegemea sana katika mtazamo huu. Lakini, baadaye, Firth hakujaribu kuifuatilia sana nadharia ya fonimu. Badala yake alianzisha nadharia yake mwenyewe ambayo baadaye ilijulikana kama Nadharia ya Arudhi (au Uchanganuzi wa Kiarudhi).
F.     EDWARD SAPIR (1884-1939)
Alizaliwa Ujerumani 1884, lakini wazazi wake wakahamia Marekani alipokuwa na umri wa miaka mitano tu na wakachukua uraia wa Marekani. Sapir alikuwa Mmarekani wa kwanza kuelezea kwa ufasaha kabisa dhana ya fonimu. Naye anasema kuwa kwa kawaida msemaji huhisi kwamba lugha yake imejengeka kwenye idadi ndogo ya sauti pambanuzi; kwamba tukiacha sauti chache, sauti zinazotumika katika lugha za kigeni ni zilezile ambazo yeye naye anazijua, ingawa anazitumia kwa namna tofauti.
MAMBO YA MSINGI YANAYOZUNGUMZWA NA SAPIR
-           Lugha zote huelekea kutumia sauti zilezile
-          Lugha zote zina ukomo wa idadi ya sauti pambanuzi. Hali hii inaashiria kuwa Sapir alitambua kuwako kwa fonimu ingawa kwa namna tofauti. Sapir anatambua kuwa sauti zitumikazo katika usemi ndizo zibebazo fonimu kwa maana ya kwamba fonimu hujitokeza ndani mwake, lakini asili ya fonimu ni ndani ya akili ya wasemaji wa lugha. Kwa mujibu wa Sapir tukiuchunguza mfumo wa ndani wa sauti katika lugha tutagundua kwamba  katika akili zetu, kama wasemaji wazawa wa lugha, kuna mfumo ‘halisi’ au ‘wa ndani’ ambao msemaji anaweza  kuuona (au mtu yeyote anayejifunza lugha) katika umbo la ruwaza kamilifu; mfumo wa kisaikolojia.  Kwa ujumla kwa upande wa Sapir lugha ni kitu cha kisaikolojia; na hivyo basi fonimu ni kipengele cha kisaikolojia.
-          Ingawa Sapir anaiona fonimu kama kipengele cha kisaikolojia hazipuuzi sifa zake za kifonetiki. Katika mtazamo wake Sapir fonimu si kitu kinachofikiriwa tu kama kimejengeka kwenye seti ndogo ya sifa za kifonetiki za sauti, bali pia ni kipengele cha kifonetiki kinachojitosheleza, ambacho kina thamani ya kisaikolojia kutokana na maumbo mengine, nyuma ya vitamkwa halisi vya kifonetiki katika mfumo wa lugha. Kwa hiyo Sapir anaiona fonimu kuwa ni ukweli unaoonekana akilini mwa msemaji wa lugha.
-          Kwa ujumla, Sapir anatambua kuwapo kwa viwango viwili vya sauti
(i)                 Kiwango cha kifonetiki na
(ii)               Kiwango cha kisaikolojia
                                 
Kwa mujibu wa mtazamo wake fonimu ni kitu kinachojikamilisha chenyewe na kinatokana na vitamkwa ambavyo kwa hakika hutokea katika lugha, si kitu cha kubahatisha tu. Kwa maneno mengine twaweza kusema kuwa Sapir anaweka msisitizo katika tabia ya kijamii katika lugha yaani lugha kama shughuli ya kijamii. Mtu anapozaliwa au anapoanza kujifunza lugha huwa ameikuta katika jamii, na anapoondoka, ama kwa kwenda katika jamii nyingine au anapokufa, huiacha katika jamii alimoikuta. Kama angekuwa amezaliwa nayo asingelazimika kujifunza lugha hiyo.

G.    LEONARD BLOOMFIELD (1887-1949)
Alizaliwa Chicago, Marekani. Mkabala wake katika mitaala ya lugha ulikuwa mkali, wa kisayansi na wa kutegemea mashine. Bloomfield anasema kuwa kwa kuwa tunaweza kutambua sifa pambanuzi za usemaji kwa kuangalia maana tu, hatuwezi kuzitambua [sifa hizo] kwa kutumia vigezo vya kifonetiki peke yake”. Hii ina maana kwamba ni ile sehemu maanifu ya sauti katika usemaji inayotufanya tuitambue sauti ya usemi kama fonimu.
Aidha, tofauti baina ya sifa pambanuzi na sifa zisopambanuzi za sauti inategemea tabia ya wasemaji. Maana ya madai haya ni kwamba kitakachoamua kwamba sauti fulani ni pambanuzi au la ni namna sauti hiyo inatakavyotumiwa na wasemaji wa lugha inayohusika.  Ikumbukwe kwamba sifa ambayo ni pambanuzi katika lugha moja inaweza isiwe pambanuzi katika lugha nyingine.
-          Fonimu inaweza kugunduliwa tu kwa kutambua sauti za lugha na jinsi zinavyofanya kazi kama mfumo mmoja; yaani kwa kuangalia jinsi zinavyotumiwa na wasemaji wa lugha inayohusika katika kuwasilisha maana.
Kwa mujibu wa Bloomfield fonimu ni kipande kidogo kabisa cha sifa pambanuzi katika sauti.
Uchanganuzi wa Bloomfield wa sifa pambanuzi na zisopambanuzi umeelezwa kwa ufupi na Dinneen.
-          Sifa pambanuzi hutokea katika mafungu; kila moja ya mafungu hayo huitwa fonimu.
-          Haiwezekani kupata sifa pambanuzi pasi na kuwepo sifa zisopambanuzi.
-          Fonimu za lugha si sauti bali ni sifa za sauti, ambazo wasemaji wa lugha wamejifunza kutambua na kutoa.
-          Upeo wa sifa zisopambanuzi ni mkubwa lakini ule wa sifa pambanuzi ni mfinyu, si badilifu sana.
-          Wasemaji wa lugha wa kigeni ambao huweza kutoa sifa pambanuzi za lugha hueleweka, lakini mara nyingi husema kwa lafudhi tofauti kutokana na mgawanyo usio sahihi wa sifa zisopambanuzi.
-          Sifa zisopambanuzi hutokea katika namna zote za mgawanyiko lakini siku zote huwa kuna kiwango ukomo cha kusigana kwake.
-          Kwa kuwa kila lugha ina fonimu zake ambazo hutokana na sifa pambanuzi mbalimbali, mara nyingi wasemaji wa lugha wageni hutumia fonimu fonimu za lugha zao za awali, ambazo zinaweza kuonekana zinafanana na zile za lugha ngeni lakini mara nyingi huangukia nje ya kiwango kinachokubalika cha fonimu za lugha ya kigeni ambazo wanajaribu kutamka.
-          Kinachofanya mawasiliano yawepo baina ya msemaji mzawa wa lugha na msemaji mgeni ni zile jitihada za msemaji mzawa za kujaribu kufidia matamshi yenye makosa ya msemaji mgeni wa lugha.
-          Matatizo huongezeka inapokuwa fonimu mbili au tatu za lugha za kigeni zinafanana na fonimu za lugha lengwa.
-          Matatizo huzidi kuwa makubwa pale ambapo lugha ya kigeni huingiza matumizi makubwa ya sifa ambazo hazifanyi kazi katika lugha yetu.

FONIMU TOFAUTITOFAUTI KAMA ZILIVYOJADILIWA NA BLOOMFIELD.

(I)                Fonimu sahili za msingi kama vile /p/, /k/, /z/ n.k
(II)             Fonimu changamani ambazo hutokana na muungano wa fonimu sahili ambazo hufanya kazi kama kitu kimoja kwa mfano, irabu unganifu.
(III)          Fonimu za upili ambazo hujitokeza kama muungano wa fonimu mbili au zaidi (kwa mujibu wa Bloomfield, vipambasauti vyote huangukia katika kundi hili).
Bloomfield anajadili pia sauti nyingine ambazo anaziita makundi maalumu ya fonimu, kwa mfano, anatofautisha fonimu zenye ukulele (vizuio, vimadende na vikwamizi) na zile zenye mlio wa kimuziki kama vile nazali, vitambaza, irabu n.k.)
Bloomfield anasema kuwa fonimu zinaweza kubainishwa kwa upambanuzi wa fonimu ujitokezao katika tabia yake ya kutofautisha maana na jinsi inavyoweza kuungana na vipashio vingine kuunda vipashio vikubwa zaidi. Naye anahimiza kuwa sifa za kifonetiki ni muhimu kwa sababu ndizo ziipazo fonimu utambulisho wake.
Kwa ujumla, Bloomfield anasema kuwa fonimu haiwezi kutazamwa katika upeke wake bali hutazamwa katika uamilifu wake katika lugha inayohusika. Kwa hakika dhana ya fonimu ya Bloomfield inashahabiana sana na dhana ya fonimu ya Trubetzkoy.
H.    MORRIS SWADESH
Mwanisimu huyu anaifasili fonimu kama kipashio kidogo kabisa kinachoweza kuleta tofauti kati ya maneno yanayofanana ambayo hutambuliwa na msemaji mzawa wa lugha kuwa ni tofauti. Swadesh kama Bloomfield naye anazichukulia fonimu za lugha kuwa vitu ambavyo vinatambuliwa na msemaji mzawa wa lugha. Lengo la Swadesh ni kujaribu kuonesha njia tofautitofauti ambazo tungeweza kuzitumia kugundua fonimu za lugha maalumu. Njia hizo ni kama zifuatazo:
(i)                 Kigezo cha kutobadilika kwa maneno: “Iwapo tutakuta tofauti za matamshi za neno lilelile moja [pasipo tofauti ya maana], basi ichukuliwe kuwa zinaonesha namna kadhaa tu za mkengeuko (unaokubalika) wa vijenzi vya fonimu
(ii)               Kigezo cha mlandano kiasi: Ukilinganisha seti zote za maneno ambayo yanafanana kifonetiki, utafikia mahala ambapo utakuta kuna sauti kadhaa muhimu zinazojitokeza kwa mfano, jozi mlinganuo finyu katika maneno kama vile; dada-data, punga-bunga, koti-goti.
(iii)             Kigezo cha uhusiano usiobadilifu. “Tuchukulie kuwa tuna kipashio cha kifonimu ambacho ni changamani, ambacho moja ya elementi zake au zote hujitokeza katika kipashio kingine changamani bila kuharibu muungano wa uchangamani wake. Katika hali kama hiyo tunaweza kusema sauti zote zenye elementi hiyo huunda darajia moja ya kifonimu.
(iv)             Kigezo cha mgawanyo wa kimtoano: Kigezo hiki kina maana kwamba   “Sauti za fonimu moja hazitaweza kutokea katika mazingira mamoja ya kifonimu. Lakini ili nguvu ya kigezo hiki iweze kufanya kazi, shurti iendane na kigezo cha mlandano wa kifonetiki”
(v)               Kigezo cha mlandano wa ruwaza: “Maumbo fulani maalumu shurti yakubaliane na ruwaza ya jumla ya kifonimu ya lugha inayohusika” Kigezo hiki kinaendana na kigezo (iv). Sauti mbili zinaweza kutokea katika mazingira ya kimtoano lakini kama hazikukaribiana sana kiumbo kiasi cha kuzifanya zionekane kuwa katika darajia asilia moja, kwa mujibu wa ruwaza ya lugha inayohusika, haziwezi kuwa ni sauti za fonimu moja.
(vi)             Kigezo cha jaribio la mbadilishano: Hiki ni kigezo kitumikacho kuonesha kama kubadilisha sauti moja kwa nyingine bado kutaiacha sauti katika mkengeuko unaokubalika.
Kwa ujumla, mambo yanayojitokeza hapa ni kama vile; utaratibu wa kujaribu kuibaini fonimu na fasili ya  tabia ya fonimu.
1.2.2.1 Fonimu
Ni kipashio kidogo kabisa cha kifonolojia kinachoweza kubadili maana ya neno. Hivyo basi, fonimu ina maana, kwakuwa inaweza kubadili maana ya neno inapobadilishwa nafasi katika neno husika. Foni chache zilizoteuliwa kutoka katika bohari la sauti ili zitumike kwenye mfumo wa sauti za lugha mahsusi ndiyo fonimu. Hivyo, fonimu ni chache ikilinganishwa na foni. Idadi ya fonimu za lugha hutofautiana kati ya lugha moja na nyingine. Mathalani, Kiarabu kina fonimu ishirini na nane (28), Kiswahili kina fonimu thelathini (30), Kifaransa kina fonimu thelathini na tatu (33), na Kiingereza kina fonimu arobaini na nne (44). Sauti ambayo huweza kubadilishwa nafasi yake katika neno lakini maana ikabaki ileile huitwa alofoni.

Alofoni ni kipashio cha kifonolojia kinachotaja hali ambapo fonimu moja hutamkwa na kuandikwa tofautitofauti bila kubadili maana ya neno. Mfano:
  • Fedha na feza
  • Sasa na thatha
  • Heri na kheri
Kwa kifupi, alofoni ni matamshi tofautitofauti ya fonimu (sauti) moja.

UHUSIANO ULIOPO BAINA YA FONIMU NA ALOFONI
Fonimu za lugha huweza kupata sura tofautitofauti kulingana na mazingira ambamo hutokea. Hii ina maana ya kwamba fonimu inaweza kubadilika ikachukua umbo moja kutokana na kutokea kwake katika mazingira fulani na ikaweza pia kubadilika ikachukua umbo jingine kutokana na kutokea kwake katika mazingira mengine tofauti. Hizi sura au maumbo mbalimbali ya fonimu moja hujulikana katika lugha ya kitaalamu kama alofoni.


1.2.2.2 Mitazamo juu ya Dhana ya Fonimu
Juhudi za kufasili dhana ya fonimu zilizofanywa wa wanaisimu mbalimbali zimezua mitazamo mbalimbali ya namna ya kuchambua dhana hii. Hadi sasa, mitazamo mitatu ifuatayo ndiyo hujulikana zaidi.
(i)        Fonimu ni Tukio la Kisaikolojia
Huu ni mtazamo uliokuzwa na kutetewa na wanasarufi geuzi-zalishi, mwanzilishi wake akiwa ni Noam Chomksy. Kwa mujibu wa mtazamo huu, fonimu ni dhana iliyo katika akili ya mzungumzaji wa lugha. Mtazamo huu unadai kuwa kila mzungumzaji wa lugha ana maarifa bubu ya idadi na jinsi ya kutamka fonimu za lugha yake. Chomsky anayaita maarifa haya kuwa ni umilisi (competence). Anadai kuwa maarifa haya ya fonimu hufanana kwa kiasi kikubwa miongoni mwa wazungumzaji wa lugha moja husika. Kinachotofautiana ni jinsi ya kudhihirisha (kutamka)  fonimu hizo, yaani utendi (perfomance). Chomsky anabainisha kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kuhitilafiana baina ya umilisi na utendi kutokana na matatizo mbalimbali ambayo mzungumzaji hukabiliana nayo. Matatizo hayo ni kama vile uchovu, ulemavu wa viungo vya matamshi, athari za mazingira, ulevi, na maradhi. Hivyo, kutokana na hali hii, fonimu hubaki kuwa tukio la kisaikolojia tu.
(ii)         Fonimu kama Tukio la Kifonetiki
Wafuasi wa mtazamo huu wanaongozwa na Daniel Jones. Daniel Jones anaiona fonimu kuwa ni [umbo] halisi linalojibainisha kwa sifa zake bainifu. Anadai kuwa fonimu huwakilisha umbo halisi la kifonetiki na inapotokea kukawa na fungu la sauti katika fonimu moja, sauti hizo huwa na sifa muhimu za kifonetiki zinazofanana. Hivyo, fonimu ya Kiswahili ni kitita cha sauti za msingi pamoja na alofoni zake.
(iii) Fonimu kama Tukio la Kifonolojia
Huu ni mtazamo wa kidhahania, ambapo huaminika kuwa fonimu ni kipashio cha kimfumo, yaani fonimu huwa na maana pale tu inapokuwa katika mfumo mahususi. Mwanzilishi wa mtazamo huu ni Nikolai Trubetzkoy. Yeye huamini kuwa fonimu ni dhana ya kiuamilifu na uamilifu huo hujitokeza tu fonimu husika inapokuwa katika mfumo wa sauti wa lugha husika. Kwa mujibu wa mtazamo huu, fonimu ni kipashio kinachobainisha maana ya neno. Mtazamo huu hutumia jozi sahili kudhihirisha dai lake. Mathalani, maneno baba na bata yana maana tofauti kwa sababu ya tofauti ya fonimu /b/ na /t/. Mtazamo huu hujulikana kuwa ni wa kifonolojia. Na kwa hakika, mawazo haya ndiyo yaliyoshika mizizi zaidi katika taaluma ya fonolojia na ndiyo inayofunzwa hivi sasa katika sehemu nyingi ulimwenguni.

Uhusiano kati ya Foni na Fonimu
Na.
Foni
Fonimu
1.
Hazina maana
Zina maana
2.
Ziko pekepeke
Zimo katika mfumo
3.
Nyingi
Chache
4.

Huweza kujitokeza kama alofoni
5.
Zinaponukuliwa, alama ya mabano mraba “[ ]” hutumika.
Zinaponukuliwa, alama ya mabano mshazari “/   /” hutumika

DHANA ZA FONIMU NA ALOFONI
Ingawa dhana ya fonimu imekuwepo kwenye vichwa vya wanaisimu tangu zamani sana lakini istilahi yenyewe ni ya hivi karibuni. Kwa mujibu wa Daniel Jones istilahi hii ya fonimu ilianzishwa na Baudouin de Courtenay. Aidha, naye Robins (1967:204) anamuunga mkono Jones na kusema kuwa ni katika kitabu chake kiitwacho Nadharia ya fonimu ndipo ambapo de Courtenay anatumia neno la Kirusi fonema kama istilahi ya kiisimu. Hata hivyo Firth, J.R (1957:1) anasema kwamba Baudouin de Courtenay pia aliazima istilahi ya fonimu toka kwa mwanafunzi wake aitwaye Kruszewski. Aidha, wapo pia baadhi ya wanazuoni wanaodai kwamba istilahi fonimu ilitolewa na Dufrichesprachlaut, yaani kitamkwa. Kwa ujumla dhana ya lini na nani hasa alianza kuitumia istilahi ya fonimu bado inaleta shida kwa wanaisimu wengi.
Jambo la msingi tu kwa sasa ni kusema kwamba, fonimu ni kipashio kilichobainifu katika lugha fulani mahsusi. Hii ina maana kwamba fonimu huweza kubadilisha maana za maneno. Hata hivyo ikumbukwe kwamba fonimu ya lugha moja yaweza isiwe fonimu ya lugha nyingine. Mfano, katika Kiswahili [b] ni fonimu kwani yaweza kubadili maana; bata, pata lakini kwenye lugha ya Kinyakyusa [b] si fonimu bali ni alofoni. Aidha, wakati ambapo ph ni fonimu katika lahaja ya Kipemba, si fonimu katika lahaja ya Kiunguja.
ALOFONI
Alofoni kietimolojia ni neno linaloundwa na maneno mawili, yaani, alo- maumbo mbalimbali na foni- yaani sauti. Kumbe, alofoni ni maumbo, balimbali au tofauti ya fonimu moja. Hivyo basi, alofoni ni maumbo mbalimbali ya fonimu moja. Kwa maneno mengine, alofoni ni matamshi tofauti ya fonimu moja (Ladefoged, 1962). Fonimu moja yaweza kuwa na maumbo mbalimbali kutokana na mazingira fulani. Kwa mfano, katika data ya maneno yafuatayo:
(i)                 Ki+ti ki+refu                    [kiti kirefu]
(ii)               Ki+ti ki+eusi                     [kiti cheusi]
(iii)              U+limi   m+refu   [ulimi mrefu]
(iv)             N+limi                               n+refu [ndimi ndefu]
(v)               N+buzi                  [mbuzi]
(vi)              N+dama               [ndama]
(vii)           N+gombe  [ng’ombe]
Katika data hii, tunaona mabadiliko ya kifonimu yakijitokeza. Katika mfano (ii) fonimu /k/ inapofuatiwa na irabu e hubadilika na kuwa ch (ki+eusi =cheusi); katika (iv) tunaona wazi kuwa fonimu /l/ inapotanguliwa na nazali n hubadilika na kuwa d (n+limi=ndimi). Hali kadhalika katika mifano ya (v) na (vii) tunaona kwamba nazali n inapofuatiwa na kitamkwa b hubadilika na kuwa m, inapofuatiwa na kitamkwa d hubakia n, na inapofuatiwa na kitamkwa g hubadilika na  kuwa ŋ. Hii ina maana kwamba katika mazingira haya sauti ch ni alofoni ya fonimu /k/; d ni alofoni ya fonimu /l/ na m ni alofoni ya fonimu /N/ (Nazali)
Pia alofoni huweza kutokea katika lugha zingine za kibantu hebu tuangalie mifan ifuatayo:
Mofimu za maneno                       matamshi yake                        maana yake
(i)                 Βirikir+a                            [βirikira]                                  ita
(ii)               n+βirikir+a                                    [mbirikira]                               unite
(iii)             a+ka+βusi                          [akaβusi]                                  mbuzi mdogo
(iv)             i+n+βusi                            [imbusi]                                   mbuzi
(v)               o+gu+βusi                         [oguβusi]                                 buzi kubwa
(vi)             o+ru+rimi                          [orurimi]                                  ulimi
(vii)           ji+n+rimi                           [jindimi]                                  ndimi
(viii)         reer+a                                [reera]                                      refu
(ix)              n+reer+a                           [ndeera]                                   ndefu
(x)               O+ku+lim+a                                  [okulima]                                 kulima
(xi)             i+n+lim+I                          [indima]                                   namna ya kulima
Katika mifano hii ya Kiruuri tunaona pia mabadiliko ya fonimu yakijitokeza. Kwa mfano , katika mfano (ii)- (iv)  fonimu β inapotanguliwa na nazali n hubadilika na kuwa b. Pia katika  mifano ya (vii)-(ix) tunaona kwamba fonimu /r/ inapotanguliwa na nazali n hubadilika na kuwa d. Katika mazingira haya ni wazi kwamba /b/ ni alofomni ya fonimu /β/ na [d] ni alofoni ya fonimu /r/ na /l/.
Hali hii ya mabadiliko ya maumbo ya fonimu kutegemea mahali ambapo fonimu hizo hutokea ni ya kawaida sana katika lugha za ulimwengu; na kwa hakika, hujitokeza sana katika lugha za kibantu. Hata hivyo ifahamike kwamba ili sauti ziwe alofoni za fonimu ileile ni sharti ziwe na mfanano wa kifonetiki. Kwa mfano ni wazi kwamba irabu /a/ na /u/ katika lugha ya Kiswahili haziwezi kuwa alofoni kwa sababu zinatofautiana sana kifonetiki. Hata kama irabu hizo zinapobadilishana nafasi huweza kutobadili maana za maneno. Kwa mfano katika data ifuatayo:
(i)                 /baibui/ na /buibui/
(ii)               /angalau/ na /angalao/
(iii)             /badili/ na /badala/
(iv)              /akhsante/ na /ahsante/
Ni wazi kwamba sauti /u/ na /a/; /u/ na /o/; /i/ na /a/ na /X/ na /h/ haziwezi kuwa alofoni za fonimu moja kwa sababu sauti hizi ni za lahaja  tofauti tofauti au zatokana na vyanzo mbalimbali kama ilivyo kwa /X/ na /h/  kwamba /X/ ni sauti ya Kiarabu wakati /h/ ni sauti ya Kibantu.
MBINU ZA UTAMBUZI WA FONIMU
Ili kuweza kuzibaini fonimu na alofoni za lugha fulani, wanaisimu hutumia mbinu mbalimbali. Miongoni mwa mbinu hizo ni hizi zifuatazo:
(i)                 Mfanano wa Kifonetiki
(ii)               Jozi mlinganuo/ pambanuzi finyu
(iii)              Mgawanyo wa kiutoano
(iv)              Mpishano huru

(I)                MFANANO WA KIFONETIKI
Sauti zinazofanana kifonetiki ni sauti zilizo na sifa bainifu zinazofanana. Kwa mfano irabu zina sifa bainifu zao na konsonanti zina sifa bainifu zao. Sauti zinazofanana sana kifonetiki ni sauti za fonimu moja (alofoni). Kwa mfano, [i] na [u] haziwezi kuwa alofoni za onimu moja kwa sababu sauti hizi zinatofautiana mno kifonetiki. Mfano katika maneno yafuatayo:
(i)                 /Baibui/ na /buibui/
(ii)               /angalau/ na /angalao/
(iii)              /badili/ na /badala/
(iv)              /Akhsante/ na /ahsante/
(v)                /mahali/ na /mahala/
Ni wazi kwamba sauti /u/ na /a/; /u/ na /o/; /i/ na /a/ na /X/ na /h/ kama tulivyosema hapo awali, haziwezi kuwa alofoni za fonimu moja kwani zina tofautiana sana kifonetiki. Labda tunaweza kusema kuwa sauti hizi ni za lahaja tofauti tofauti au zatokana na vyanzo mbalimbali kama ilivyo kwa /X/ na /h/ kwamba /X/ ni sauti ya Kiarabu wakati /h/ ni sauti ya Kibantu. Ukizichunguza irabu /u/ na /a/ kwa mfano, utagundua kuwa mfanano pekee ni kwamba ni irabu lakini hazina mfanano mwingine. Wakati /u/ ni irabu ya juu nyuma viringo, /a/ ni ya irabu ya chini/. Pia /X/ ni konsonanti ya kaakaa laini wakati /h/ ni ya glota. Mfanano pekee unaoonekana ni kwamba zote ni konsonanti na zote ni sighuna.
Daniel Jones (1957) anaeleza kuwa fonimu fulani katika lugha huwa ni ujumuisho na udhahanishaji wa sauti kadhaa au kundi la sauti ambazo kwanza kabisa ni lazima zifanane sana kifonetiki. Anasema ni familia ya sauti (family of sounds); wanafamilia huwa na mfanano fulani kama sura, urefu n.k. Hapa Jones anazungumza kuhusu alofoni
(II)                JOZI MLINGANUO FINYU/ JOZI PAMBANUZI FINYU (minimal pairs)
Fischer (1957) anaeleza kuwa, jozi mlinganuo finyu ni tofauti ndogo kabisa ya kifonolojia iliyopo baina ya maneno fulani.  Mara nyingi maneno hayo huwa na
(i)                 Idadi sawa ya fonimu
(ii)                Fonimu zinazofanana isipokuwa moja
(iii)             Mpangilio wa fonimu ulio sawa
Kwa mfano, katika lugha ya Kiswahili maneno kama /pia/; /tia/ na /lia/ ni jozi mlinganuo finyu kwa sababu zina idadi sawa za fonimu (fonimu tatu), aina za fonimu zilizopo ni sawa isipokuwa moja, yaani /i/ na /a/ ni sawa na tofauti ni /p/, /t/ na /l/. Kigezo hiki ni cha uamilifu. Maneno hayo yote lazima yawe ya lugha inayohusika na pia neno hilo liwe na maana tofauti na neno la awali. Hivyo, sauti /p/, /t/ na /l/ ni fonimu tofauti kwa sababu zinabadili maana ya maneno.
(III)          MGAWANYO WA KIMTOANO/ MTAWANYO MKAMILISHANO (Complementary distribution)
Hyman (1975), anasema, utoano ni dhana ambayo hutumiwa kuelezea uhusiano uliopo baina ya sauti mbili au zaidi za fonimu moja ambazo haziwezi kutokea katika mazingira sawa! Kwa hiyo, kila sauti huwa ina mahala/ mazingira yake maalum ambayo hayawezi kukaliwa na sauti nyingine. Kwa mfano, kutoka katika lugha ya Kiingereza sauti /p/ na /ph/ hutokea katika mazingira tofauti. Wakati /p/ hutokea mahali popote pale, /ph/ hutokea mwanzoni mwa maneno tu kama katika maneno /pin/, /pen/, /put. n.k. Kwa sababu sauti hizo zinafanana kifonetiki na tofauti pekee ni mpumuo tu basi sauti hizo ni alofoni za fonimu moja ambayo ni [p]. Na sauti hizo zipo katika mahusiano ya mgawanyo wa kimtoano.
Katika lugha za Kibantu pia hili hutokea kama inavyojidhihirisha katika data ifuatayo kutoka katika lugha ya Kiruuri.
Mofimu za maneno                       matamshi yake                        maana yake
(xii)           Βirikir+a                            [βirikira]                                  ita
(xiii)         n+βirikir+a                        [mbirikira]                               unite
(xiv)         a+ka+βusi                          [akaβusi]                                  mbuzi mdogo
(xv)           i+n+βusi                            [imbusi]                                   mbuzi
(xvi)         o+gu+βusi                         [oguβusi]                                 buzi kubwa
(xvii)       o+ru+rimi                          [orurimi]                                  ulimi
(xviii)     ji+n+rimi                           [jindimi]                                  ndimi
(xix)         reer+a                                [reera]                                      refu
(xx)            n+reer+a                           [ndeera]                                   ndefu
(xxi)         O+ku+lim+a                      [okulima]                                 kulima
(xxii)       i+n+lim+I                          [indima]                                   namna ya kulima
Utagundua kwamba sauti /b/ na /β/ zinafanana sana kwani zote ni konsonanti za midomo na zote ni ghuna; pia sauti /l/, /r/ na /d/ zote  ni za ulimi; au /s/ na /z/ katika /dogs/ na /cats/ ni sauti za ufizi na tofauti pekee ni +/- ghuna.
[b]/ N-------
/β/      
 [β]/---------
Hii maana yake ni kwamba fonimu /β/ inajitokeza kama [b] inapotanguliwa na nazali na inajitokeza kama [β] mahali penginepo.
(IV)          MPISHANO HURU
Ni uhusiano wa fonimu mbili tofauti kubadilishana nafasi moja katika jozi maalumu ya maneno bila kubadili maana ya maneno hayo. Kwa hiyo, maneno mawili yanaweza kuwa na tofauti ya fonimu moja tu lakini fonimu hizo tofauti ni tofauti sana kifonetiki na hivyo haziwezi kuwa alofoni za fonimu moja.
Pili, fonimu hizo hazipo katika ule uhusiano wa kiutoano, yaani, zote zinaweza kutumika katika mazingira yaleyale kwenye neno lakini fonimu hizo ingawa ni tofauti hazisababishi tofauti za kimaana katika maneno zinamotokea. Kigezo hiki hakipingani na kile cha msingi kuhusu uwezo wa fonimu kuweza kubadili maana. Tofauti kati ya mpishano huru na mgawanyo wa kiutoano ni kwamba:
► Mpishano huru huhusisha fonimu mbili au zaidi zilizo tofauti kabisa, mgawanyo wa kiutoano hazihusishi alofoni mbili au zaidi za fonimu moja zinazofanana sana kifonetiki, za aina moja na zinazotamkiwa sehemu moja.
► Mpishano huru huhusisha fonimu mbili zinazobadilishana/kupishana nafasi moja katika neno wakati mgawanyo wa kiutoano huzihusisha alofoni ambazo zimegawana mahali tofauti pa kutokea. Kila moja ina muktadha wake maalumu ambao ni mwiko kukaliwa na alofoni nyingine.
► Kufanana kwao ni: mpishano huru maana za maneno hazibadiliki na pia katika mgawanyo wa kiutoano maana za maneno hazibadiliki.
Baadhi ya mifano ya mpishano huru katika lugha ya Kiswahili:

MANENO
MPISHANO HURU
Alimradi- ilimradi
/u/ na /i/
Baibui- buibui
/a/ na /u/
Bawabu -bawaba
/u/ na /a/
Angalao- angalau
/o/ na /u/
Amkia- amkua
/i/ na /u/
Banyani- baniani
/ny/ na /n/
Wasia - wosia
/a/ na /o/
Heri- kheri
/h/ na /X/
Mtelemko- mteremko
/l/ na /r/

Sababu zinazosababisha mpishano huru:
► Tofauti za kimtindo
► Tofauti za kilahaja
► Tofauti za kijiografia
FONIMU ZA KISWAHILI
Kuna mgawanyo bayana wa fonimu za lugha ya  Kiswahili. Kuna makundi mawili yaliyojikita katika kuangalia namna sauti hizo zitolewavyo
  1. Irabu/vokali, nazo zipo 5
  2. Konsonanti, zipo 26
IRABU
Tofauti iliyopo kati ya utamkaji wa irabu na ule wa konsonanti ni kuwa utamkaji wa irabu hauandamani na mzuio wowote wa mkondo-hewa, yaani hewa hupita kwa urahisi bila kuzuiliwa. Hivyo basi, migawanyo ya irabu haitegemei mzuio wa hewa, bali hutegemea sana mkao wa ulimi katika kinywa wakati wa utamkaji, vilevile mkao wa midomo wakati huo. Irabu hupangwa kufuatana na vigezo vitatu: ulimi uko juu kiasi gani kinywani (ujuu); ni sehemu gani ya ulimi inainuliwa au kushushwa (umbele); na midomo ikoje wakati huo (uviringo).
(i)                 UJUU
Wakati wa kutamka irabu-juu ulimi unakuwa umeinuliwa juu katika kinywa, ambapo irabu-chini hutolewa wakati ulimi umeteremshwa chini. Irabu-juu ni kama [i,u] na irabu-chini ni kama [a]. Ulimi ukiwa katikati ya kinywa, irabu zinazotolewa huitwa irabu-kati, nazo ni kama [e,o].
(ii)               UMBELE
Wakati ulimi unainuliwa kinywani, unaweza kupelekwa mbele katika kinywa, na hivyo kutolewa irabu-mbele kama [i,e]. Ikiwa ulimi utarudishwa nyuma, basi irabu zitolewazo zitakuwa irabu- nyuma kama [u,o]. Irabu [a] kama ya Kiswahili hutolewa ambapo ulimi hauko mbele au nyuma, bali uko katikati.
(iii)             UVIRINGO
Wakati wa utamkaji wa irabu, midomo inaweza kuviringwa, na irabu zitakazotolewa zitakuwa  viringo, kama [u,o]. Midomo inaweza kusambazwa au kupanuliwa na hivyo kutoa irabu siviringo, kama [i,e,a].
KIELELEZO CHA IRABU ZA KISWAHILI
[i] irabu juu mbele siviringo
[u] irabu juu nyuma viringo
[e] irabu kati mbele siviringo
[o] irabu kati nyuma viringo
[a] irabu chini siviringo
VIYEYUSHO
Ni aina ya vitamkwa/fonimu  ambavyo si konsonanti na wala si irabu; yaani ni vitamkwa ambavyo huchukuliwa kuwa viko katikati ya irabu na konsonanti. Kwa vile vitamkwa hivi havina sifa kamili ya ukonsonanti na pia havina difa kamili ya uirabu lakini vinaelekea zaidi kufanana na irabu wakati mwingine hupewa jina la nusuirabu. Katika lugha nyingi za Kibantu viyeyusho huwa ni vya aina mbili:
[y] na [w].
KONSONANTI
Konsonanti ni aina ya sauti ambazo hutamkwa kwa kuzuia mkondohewa kutoka mapafuni, ukipitia chemba ya kinywa na chemba ya pua kwenda nje. Uzuiaji wa mkondo huo wa hewa unaweza  kuwa wa kubana kabisa na kuachiwa ghafla, kama tunapotamka sauti [p]; unaweza kuwa wa kubana kabisa na kisha kuachiwa taratibu, kama tunapotamks sauti [ch]; unaweza kuwa wa kubana kiasi na kuruhusu hewa hiyo ipite katika nafasi nyembamba  na wakati huohuo midomo ikiwa katika hali ya kuviringwa  kiasi, kama tunapotamka sauti [f] au [v]; unaweza kuwa wa kubana hewa lakini ukiwa unaruhusu hewa ipite pembeni mwa ulimi, kama tunapotamka sauti [l]; unaweza kuwa wa kubana hewa kinywani na kuiruhusu ipitie puani kama tunavyotamka sauti [m],  [n], an ng’ [ŋ]. Kila konsonanti za lugha huwa na sifa mahsusi zinazozitambulisha.
SIFA KUU ZA KONSONANTI
Sifa hizi zinazingatia mambo makuu matatu
1.      Jinsi konsonanti zinzvyotamkwa
2.      Mahali ambapo konsonanti hutamkiwa
3.      Hali ya nyuzi sauti
SIFA ZA JINSI YA MATAMSHI
Katika sifa hii konsonanti hugawika katika makundi sita
A.    VIPASUO/VIZUIWA
Wakati wa utamkaji wa konsonanti hizi huwa kuna mzuio wa mkondohewa na kuachiwa ghafula. Konsonanti hizi zimepewa jina hilo kutokana na kwamba katioka kuachiwa ghafla kwa mkondohewa sauti itokeayo huwa kidogo kama ina mlio wa kupasua. Kwa mfano konsonanti /p/, /b/, /t/, /d/, /k/ na /g/.
/p/  kipasuo sighuna cha midomo
/b/ kipasuo ghuna cha midomo
/t/ kipasuo sighuna cha ufizi
/d/ kipasuo ghuna chaa ufizi
/k/ kipasuo sighuna cha kaakaa laini
/g/ kipasuo ghuna cha kaakaa laini
B.     VIZUIO/VIPASUO KWAMIZA
Konsonanti hizi zinapotamkwa hewa husukumwa nje kwa nguvu na kuzuiwa halafu nafasi ndogo huachwa ili hewa ipite ikiwa na mkwaruzo. Kwa mfano, /č/ na ŧ/
C.     VIKWAMIZI
Katika utoaji wa sauti hizi mkondohewa unazuiliwa nusu tu, na hivyo hewa           inapita kwa kujisukuma kupitia katika nafasi au uwazi mdogo uliopo, na hivyo          kusababisha kukwamakwama. Kwa mfano, /f/, /v/, /ө/, /ð/, /s/, /z/,  na /š/.
D.    NAZALI
Ni aina ya konsonanti ambazo hutamkwa kwa kukishusha kimio kwa namna ambayo kiasi kikubwa cha hewa kutoka mapafuni huelekezwa kupitia kwenye chemba cha pua. Kwa mfano, /n/, /m/, /ŋ/ n.k.
E.     VITAMBAZA
Hutamkwa kwa hewa kusukumwa nje na kuzuiwa halafu kuruhusiwa kupita pembeni mwa kizuizi bila mkwaruzo mkubwa sana. Kwa mfano, /l/.


F.     VIMADENDE
Hutamkwa ncha ya ulimi ikiwa imeugusa ufizi lakini kutokana na nguvu ya hewa inayopita kati ya ncha ya hiyo na ufizi ncha ya ulimi hupigapiga kwa harakaharaka kwenye ufizi. Kwa mfano, /r/.
SIFA ZA KONSONANTI ZA MAHALI PA MATAMSHI
Sifa hii inahusu sehemu mbalimbali za chemba ya kinywa ambapo alasogezi na altuli hugusana au hukaribiana katika utamkaji  wa sauti tofautitofauti za lugha. Kuna sifa saba za mahali pa matamshi:
    1. SAUTI ZA  MIDOMO
Wakati wa kutamka sauti hizi midomo huwekwa pamoja. Kwa mfano, /p/, /b/ na /m/
  1. SAUTI ZA MDOMO-MENO
Wakati wa kutamka sauti hizi mdomo na meno ya juu hugusana. Kwa mfano, /f/, na /v/.
3. SAUTI ZA MENO
Wakati wa kutamka sauti hizi ncha ya ulimi hugusana na meno ya juu. Mfano wa sauti hizi ni kama vile /ө/,  / ð,
4. SAUTI ZA UFIZI
Sauti hizi zinapotolewa ncha ya ulimi hugusana na ufizi. Mfano wa sauti hizi ni /t/, /d/, /n/, /s/, /z/, /l/, na /r/
5. SAUTI ZA KAAKAA GUMU
Sauti hizi hutolewa wakati sehemu ya nyuma ya ulimi inapogusana na kaakaa gumu. Kwa mfano /č/, /š/, /ј/, n.k.

6. SAUTI ZA KAAKAA LAINI
Sauti hizi hutolewa wakati sehemu ya nyuma ya ulimi inapogusana na kaakaa laini. Kwa mfano /k/, na /g/.
7. SAUTI ZA GLOTA
Sauti hizi hutokea wakatii nyuzi sauti zinapokutanishwa kwa muda mfupi. Katika lugha sauti hizi ni chache sana. Kwa mfano /h/.
HALI YA NYUZI SAUTI.
Katika kongomeo kuna nyuzi-sauti ambazo zinakuwa katika nafasi za aina mbili wakati hewa inapopita. Ikiwa nyuzi-sauti ziko pamoja yaani zimekaribiana au kusogeana karibu hewa inapotoka kwenye mapafu huzisukuma na kuzitenganisha wakati wa kupia, na hivyo kusababisha msukumo. Sauti zinazotolewa wakati huu zinakuwa na mghuno na huitwa sauti ghuna. Ikiwa nyuzi-sauti hizi zimeachana, hewa hupita kwa urahisi bila kuzuiliwa, na hivyo bila kusababisha msukumo. Sauti zinazotolewa wakati huu huwa hazina mghuno, na huitwa sighuna.
SIFA BAINIFU/ SIFA PAMBANUZI
Sifa katika isimu ni vitu au mambo ambayo yanakibainisha kipengele chochote cha kisarufi au cha kiisimu (Massamba 2004:80).
Sifa bainifu ni nduni zitumikazo kutofautisha kipashio kimoja cha isimu na kipashio kingine cha aina yake. Katika kubainisha vipashio mbalimbali kuna vigezo viwili:
A.    KIGEZO CHA KIFONETIKI
Kigezo hiki huangalia jinsi, mahali, hali ya nyuzi sauti, mwinuko wa ulimi na umbo la midomo katika utamkaji wa sauti mbalimbali za lugha tofauti tofauti.
B.     KIGEZO CHA KIFONOLOJIA
Hiki ni kile kinachoangalia maathiriano ya lugha. Fonolojia nyambulishi ya lugha mahsusi. Hapa sifa za lugha inayochambuliwa huangaliwa zaidi. Kwa mfano, kuna baadhi ya fonimu hupata sifa ya usilabi katika lugha mojawapo na siyo nyingineyo. Mfano, mtu, /m/ inapata sifa ya usilabi. Pia katika nne, /n/ hupata sifa ya usilabi. Aidha, hali hii inalingana na mfumo wa lugha husika.
Wanafonolojia wengi wanakubaliana kwamba wazo la sifa pambanuzi lilianzishwa na shule ya “Mawazo ya Prague”. Hata hivyo mwanazuoni wa kwanza kulibabadua suala la sifa pambanuzi alikuwa ni NIKOLAJ TRUBETZKOY, naye ni mmojawapo kati ya waanzilishi wa Shule ya Mawazo ya Prague. Mwanazuoni huyu alianzisha nadharia ya Upambanuzi (Trubetzkoy 1969:31-83). Madai ya msingi katika nadharia hii ya Trubetzkoy ni kwamba pakiwapo na upambanuzi basi lazima patakuwapo ‘ukinzani’. Naye anauainisha ukinzani pambanuzi katika seti kuu tatu.
SETI YA KWANZA
(a)    Ukinzani uwili
(b)   Ukinzani kiwingi
(c)    Ukinzani kiwiani na
(d)   Ukinzani kipeke
(a)   UKINZANI KIUWILI (Bilateral Opposition)
Ni ukinzani wa sauti ambapo jumla ya sifa bainifu zinazochangiwa na sauti mbili kinzani hupatikana katika sauti hizo mbili peke yake na si kwingineko. Mfano, vipasuo vya midomo [p] na [b] katika Kiswahili ambavyo vinachangia sifa ya kuwa vipasuo vya kinywa vya midomo, hakuna vipasuo vingine vinachongia sifa hiyo.
(b)   UKINZANI KIWINGI (Multilateral Opposition)
Huu ni ukinzani wa sauti ambapo jumla ya sifa bainifu zinazochangiwa na sauti hizo kupatikana katika seti ya sauti nyingine pia. Mfano P na R (herufi) zote zinachangia mkunjo upinde unaoelekea kulia. Lakini haziwezi kuhesabiwa kuwa na ukinzani kiuwili, kwa sababu sizo herufi pekee zenye mkunjo kama huo herufi B nayo inao. Hivyo, ukinzani unaopatikana katika sauti ambazo jumla ya sifa zinazochangiwa nazo hupatikana pia katika ukinzani mwingine na ndio ujulikanao kama ukinzani kiwingi
(c)    UKINZANI KIWIANI (Proportional opposition)
Ni ukinzani wa sauti mbili ambao unawiana na ukinzani wa sauti mbili ambao unawiana na ukinzani wa sauti nyingine mbili. Mfano, ukinzani baina ya [f] na [v] na ukinzani baina ya [s] na [z] katika Kiswahili.
(d)   UKINZANI KIPEKE (Isolated opposition)
Ni ukinzani ambao ni wa kipekee kabisa. Mfano, ukinzani baina ya sauti [r] na [l] katika lugha ya Kiingereza. Katika lugha hii hakuna memba wengine walio na uhusiano wa namna hiyo.
SETI YA PILI
(a)    Ukinzani kibinafsi
(b)   Ukinzani kimwachano taratibu
(c)    Ukinzani kisawa

(a)   UKINZANI KIBINAFSI (Private opposition)
Huu ni ule ukinzani ambapo sauti moja inakuwa na alama za ziada (sifa ya ziada) na sauti nyingine inakuwa haina, mfano kama sauti moja inakuwa na mghuno nyingine inakuwa haina n.k.
(b)   UKINZANI KIMWACHANO TARATIBU (Gradual opposition)
Ni ule ukinzani ambapo memba wa seti wanapishana kwa viwango tofauti vya sifa ileile. Mfano, tofauti iliyopo baina ya irabu [o] na [u].
(c)    UKINZANI KISAWA (Equipollent opposition)
Ukinzani ambapo ukinzani baina ya memba wa kundi moja ni sawa na ukinzani baina ya memba wa kundi jingine, kimantiki; kwa maana ya kwamba ukinzani wao si wa kupishana kwa viwango vya sifa ileile wala hawawezi kuchukuliwa kwamba kama memba mmoja wa kundi ana sifa ya ziada basi mwingine hana. Kwa mfano, sauti [p] na [t] na [f] na [k] katika Kijerumani.
SETI YA TATU
(A) Ukinzani imara (ukinzani usobadilifu)
(B)  Ukinzani usoimara (ukinzani ulobadilifu)
Trubetzkoy pia anaziainisha sifa pambanuzi kwa kuangalia kiasi cha ubainifu wa upambanuzi wa sifa. Mfano, ukinzani baina ya /t, d, l/ katika Kiswahili. /t/ siku zote inakuwa /t/ lakini /l/ inaweza kugeuka na kuwa /d/ mfano, katika u-limi------ n-dimi. Hivyo ukinzani wa /t/ ni imara lakini ule wa /d,l/ si imara (badilifu).
SIFA PAMBANUZI ZA ROMAN JAKOBSON
Huyu ni miongoni mwa wanazuoni waliotumia sifa pambanuzi katika uwakilishi wa vipengele vya kifonolojia na kifonetiki (1952). Aidha, ni mwanzilishi mwingine wa Shule ya Mawazo ya Prague. Katika nadharia yake ya sifa pambanuzi, alianza kwa kubanisha sifa za kimatamshi dhidi ya sifa za kiakustika. Kisha akabainisha sifa za uwili dhidi ya sifa zisouwili. Pia Jakobson na Halle (1956) wakabainisha sifa pambanuzi katika makundi makuu matatu. Nao walijishughulisha zaidi na sifa kinzani katika lugha. Sifa zao zilielemea zaidi katika ‘ukinzani wa kifonolojia kuliko ule wa kifonetiki. Mazoea ya watangulizi wao yalikuwa ni kuziainisha sauti kifonetiki, yaani kubainisha konsonanti, irabu, viyeyusho na vitambaza. Lakini wao walizigawa katika makundi mawili zile zenye ukonsonanti na zile zisizo na ukonsonanti yaani konsonanti na vokali. Wakazigawa tena sifa hizi kuu katika makundi madogomadogo manne

1.      Konsonati halisi
                                                 +konso
                                           -vokali
                                                 /p/

2.      Vokali


-konso
+voka
/a/
3.      Vitambaza


                  +konso
                  +voka
                  /l/
4.      Viyeyusho


                   -konso
                   -voka

                          /y/

SIFA PAMBANUZI ZA CHOMSKY NA HALLE
Sifa zao zilijikita zaidi katika uelekeo wa kifonetiki kuliko walivyofanya Jakobson na Halle. Katika uainishaji wao sifa pambanuzi za sauti za lugha wanazigawa katika makundi matatu.
(i)                 Sauti zenye usonoranti (dhidi ya zile zisizo na usonoranti).
(ii)               Sauti zenye uvokali (dhidi ya zisizo na uvokali).
(iii)             Sauti zenye ukonsonanti (dhidi ya zile zisizo na ukonsonanti)

(i)                 KUNDI LA SONORANTI (dhidi ya zisosonoranti)
Kwa mujibu wa Chomsky na Halle (1968:302) sauti zenye usonoranti hutolewa kwa kuiweka njia ya mkondohewa katika mkao ambao huwezesha ughunishaji wa sauti wa papo hapo, wakati zile zisizo na usonoranti (obstruenti) hutolewa kwa kuiweka njia ya mkondohewa katika mkao ambao hauwezeshi ughunishaji wa papo hapo, mfano, nazali, vitambaza, vimadende na viyeyusho.
(ii)               KUNDI LA V OKALI
Sauti zenye uvokali hutolewa kwa kuweka mkao wa mvungu  wa kinywa katika hali ambayo ubanaji wa mkondohewa hauzidi ule utumikao katika kutamka sauti [i] na [u], na wakati huohuo nyuzisauti zikiwa katika mkao ambao huwezesha ughunishaji wa papohapo.
► Sauti zenye uvokali ni : irabu na vitambaza ghuna, viyeyusho, konsonanti nazali, obstruenti, irabu zisoghuna na vitambaza visoghuna hazina uvokali.
(iii)             KUNDI LA KONSONANTI
Sauti zenye ukonsonanti hutolewa kwa uzuiaji mkali wa mkondohewa katika sehemu ya kati ya njia ya mkondohewa. Sauti zisizo na ukonsonanti hutamkwa bila kuwepo uzuiaji wa mkondohewa wa namna hiyo. Hivyo basi, sauti zenye usonoranti ni: irabu, viyeyusho, nazali, konsonanti na vilainisho. Zenye uvokali: irabu ghuna na vilainisho zenye unazali na konsonanti zisizo na unazali. Baadaye waliona istilahi ya vokali inachanganya wakaanza kutumia istilahi ya USILABI.
SABABU ZA KUCHUNGUZA SIFA BAINIFU/ PAMBANUZI
1.      Kujumuisha vitamkwa vinavyochangia sifa fulani.
2.      Kutenga makundi asilia yanayochangia mahali pa matamshi n.k. mfano, vitamkwa vya msingi vinaweza kuwekwa katika makundi asilia.
3.      Waliona kuwa kuna sifa zitumikazo katika kila lugha duniani, mfano, sifa ya ukonsonanti [+konso]. Nayo huhusisha vitamnkwa vinavyohusishwa msuguano katika utokeaji wake ambao waweza kuwa wa kubana, mwembamba au wa kimadende. Hali hii huletelea makundi kama ya: vizuio, vikwamizi, ving’ong’o, vitambaza na vimadende. Waliona pia kuna uwepo wa usilabi [+sil]. Ving’ong’o, vitambaza huwa na usilabi katika baadhi ya lugha. Waliona kwamba ni vema wabague/ watenganishe kati ya ving’ong’o na vitambaza/ vimadende.
► Sifa ya Usonoranti
Kuna ughuna wa vitamkwa kama vile vyenye usilabi na hakuna mguno kwani mkondohewa hauzuiliwi. Ukonsonanti, usilabi na usonoranti huweza kuletelea aina mbalimbali ya makundi. Vipasuo ndani, vikwamizi kwani kuna vitamkwa vina sifa ya ukonsonanti na hazina usonoranti wala usilabi.

SIFA BAINIFU/ PAMBANUZI ZIJENGAZO FONIMU ZA KISWAHILI SANIFU
Konsonanti ni aina ya vitamkwa vitokanavyo na msogeano wa kubana, mwembamba, au wa umadende wa ala za matamshi. Kifonetiki, konsonanti huainishwa kufuatana na kubanwa kabisa kwa mkondohewa katika chemba au kufuatana na kuwepo kwa upenyu mwembamba kiasi cha kuleta msuguano. Katika uchanganuzi wa kifonetiki, sifa bainifu za konsonanti huainishwa kwa kutumia sifa zote hata zile zisizo za lazima, tofauti na uchanganuzi wa kifonolojia ambapo uainishaji wa sifa bainifu huhusisha sifa zile za lazima tu nazo ni:  namna ya kutamka, mahali pa kutamkia, hali ya nyuzi sauti, mkao wa kilimi, mkao wa ulimi,  na mfumo wa mkondohewa.
A.    SIFA YA JINSI YA MATAMSHI
(i)                 Sifa ya usilabi  [+sil]
Irabu za Kiswahili zina sifa ya usilabi, ving’ong’o katika mazingira maalumu vinakuwa na sifa ya usilabi hasa katika mazingira ya kisarufi.
(ii)               Mghuno/ughuna [+ghuna]
Nyuzisauti zinapotetemeshwa sauti zitolewazo huwa na mghuno; konsonanti ghuna, vilainisho, irabu, ving’ong’o n.k.
(iii)             Ukontinuanti [kont]
Wakati wa kutolewa sauti hizi kuna kuwa na msogeano mpana au mwembamba. Mfano, vikwamizi, irabu, ving’ong’o, viyeyusho na vilainisho n.k.
(iv)             Unazali [+naz]
Wakati wa kutolewa kwa sauti hizi hewa huzuiliwa kupita mdomoni na kupitia puani, mfano, [m, n, ŋ,ň]
(v)               Utambaza [+tambaz]
Hii huhusika na vitamkwa ambavyo wakati wa kutolewa hewa huzuiliwa na kupita pembeni mwa ala sauti mfano [l]
(vi)             Stridenti
Sifa pambanuzi inayohusu sauti zitamkwazo kwa msikiko wa kelelekelele kuliko sauti nyingine. Mfano, [s], [z], [š], [ ], [f], [v], [ts]. Hutamkwa kwa kulazimisha mkondohewa kupita katika sehemu mbili kwa namna ya msuguano ambao hutoa sauti ya kukwamizwa yenye msikiko wa juu.
(vii)           Umadende [+mad]
Ni vile vitamkwa vitolewavyo wakati ala sogezi hugongagonga kwenye ala nyingine tulivu, kwa mfano [r].
2. SIFA ZA MAHALI PA MATAMSHI
(a) Ukorona [+kor]
Huhusisha vitamkwa ambavyo wakati wa kutolewa bapa/ ncha ya ulimi huhusika na kuna kuwa na msogeano wa kubana au mwembamba wa ala za matamshi, mfano, sauti za meno, ufizi, kaakaa gumu.
(b) Uanteria [+ant]
Huhusisha vitamkwa vinavyotolewa kwenye ufizi na mbele ya ufizi /t/, /d/, midomo, meno na ufizi.
© Umeno [+meno]
Huhusisha vitamkwa vitolewavyo kwenye meno mfano [th na dh]
(d)   Uglota [+glot]
Huhusisha kitamkwa kinachotolewa kwenye glota katikati ya nyuzisauti mfano [h]
3 SIFA BAINIFU ZIHUSUZO KIWILIWILI CHA ULIMI
(i)                 Ujuu [+juu]
Hii inahusu vitamkwa ambavyo wakati wa kutolewa, ulimi hunyenyuliwa juu ya chemba ya kinywa mfano, [i,u ts ny]
(ii)               Uchini [+chini]
Hii huhusisha vitamkwa ambavyo wakati wa kutolewa, ulimi unakuwa chini ya kinywa mfano [a].
(iii)             Unyuma [+nyuma]
(iv)             Hii hujihusisha na vitamkwa ambavyo hutolewa sehemu ya nyuma ya chemba ya kinywa, mfano, [u, o, k, g, ng].




SIFA BAINIFU NYINGINEZO
UWEKEVU
Katika kubainisha fonimu. Tumia sifa chache kadri iwezekanavyo bayana katika kubainisha fonimu. Mfano,
-          ughuna na usighuna
-          ukontinuanti/ uendelezi/ vifulizwa
-          uanteria
-          ukorona

/p/                                /b/                                /t/                     /d/
-gh                               +gh                              -gh                   +gh
-kont                            -kont                            -kont                -kont
+ant                             +ant                             +ant                 +ant
-kor                              -kor                              +kor                 +kor

(II) UZIADA
Kuwepo au kutokuwepo kwa sifa fulani kunatabirika kutokana na kuwepo au kutokuwepo kwa sifa nyingine. Hususani zile ambazo si muhimu kubainisha fonimu. Kwa mfano,
/i/
+sil
+juu                                                              +sil
+son                                                             +juu
-chini                                                           +son
+mbele
-nyuma
+ghuna
+kont
Sifa za ziada za /i/ ni:
+kont
-chini
-nyuma
+mbele
+ghuna

Sifa za ziada hubainishwa kwa kutumia mantiki. Na huwa si muhimu kubainisha fonimu. Sifa inaweza kubainishwa kwa kutumia uwili unaokinzana. Mfano,
+kont = [-kont]
Mwanamke                             Mwanamme
[+ke/ -me]                    [+me, -mke]
Mfano, nazali zote zina ughuna. Pia sauti ambazo ni sonoranti zina sifa ya ughuna. Mantiki inatumika kubainisha sauti zenye sifa ya uziada. Mfano, nazali haiwezi kuwa madende a kiyeyusho.


MAKUNDI ASILIA YA FONIMU ZA KISWAHILI
1.      VIPASUO/ VIZUIO
Hutamkwa kwa kuzuia kabisa mkondohewa utokao mapafuni kasha kuachiwa ghafula.
/p/                    /d/                    /b/                                /t/                     /k/
-kont                -kont                -kont                            -kont                -kont
-gh                   +gh                  +gh                              -gh                   -gh
+anteria           +ant                 +ant                             +ant                 +ant
-kor                  +kor                 -kor                              +kor                 +juu
                                                                                                                  +nyuma
2.      VIKWAMIZO/ VUKWAMIZWA/ VIKWAMIZWA
/f/                     /v/                    /th/                   /dh                   /s/        
+kont               +kont               +kont               +kont               +kont
-gh                   +gh                  -gh                   +gh                  -gh
+meno             +meno             +meno             +meno             +kor
-kor                  -kor                  +kor                 +kor                 -meno

/sh/                   /γ/                                /h/
+kont               +kont                           +kont
+kor                 +gh                              +glot
-gh                   +unyuma                     -gh
-juu                  +ujuu
-nyuma

3.      VING’ONG’O
/m/                                           /n/                    /η/                               /ny/
+nazal                                      +nazal              +nazal                          +nazal
+ant                                          +kor               -sil                               -sil
+sil                                            -sil                 +unyuma                     +juu
-kor                                                                  -kor                              -nyuma
+ghuna                                                            -ant                              +kor
+midomo                                                         +juu                             -ant

4.      VILAINISHO- Sonoranti
/l/                                 /r/
+son                            +son
+kor                             +kor
+tambaz                      +mad
+ghun                          +ghuna
-unazal                         -nazal

5. IRABU [+sil]

/i/                     /u/                    /e/                    /o/                    /a/
+sil                  +sil                  +sil                  +sil                  +sil
+juu                 +juu                 -nyuma            +nyuma           +chini
-nyuma            +nyuma           -chini               -juu                  -juu
                                                -juu                  -chini

6. VIYEYUSHO [-sil]
/w/                               /j/
-sil                               -sil
+juu                             +juu
+nyuma                       -nyuma

UMUHIMU WA SIFA BAINIFU
1.      Husaidia kugawa fonimu katika makundi asili.
2.      Husaidia kutofautisha kati ya kundi moja la fonimu asilia na jingine.
3.      Husaidia kuonesha maathiriano yanayotokea katika lugha.
4.      Hurahisisha katika uandishi wa kanuni kwani zinaandikwa kwa ufasaha na bayana.
5.      Huonesha mwenendo au tabia ya lugha Fulani kwa sababu tunaelewa baadhi ya fonimu hubadilika kutokana na muktadha wa fonimu au kimatumizi mfano, nazali ina sifa ya usilabi na isiyo na usilabi.
6.      Husaidia kuonesha muundo wa ndani wa sauti fulani.
MODULI YA 5:  KANUNI NA MICHAKATO YA KIMOFOFONOLOJIA
Ni mabadiliko yanayoonekana ya fonimu moja au mbili. Kila lugha ina mfumo wake wa kifonolojia. Hakuna lugha zinafanana idadi zake za fonimu na alofoni. Katika lugha kuna mfanano wa sifa bainifu zinazoelekeana kati ya lugha moja na nyingine kwa mfano, sifa za ujuu, ughuna n.k. Ila si katika lugha zote kwa sababu ya ufanano huo ni kwa sababu alasauti (viungosauti) vya kutolea sauti hufanana kwa binadamu wote.
Aidha, kila lugha ina mifumo yake asilia ya kifonolojia (Natural phonological processes) ijapokuwa hutofautiana.
MICHAKATO ASILIA
Ni taratibu zinazoonesha maathiriano ya sauti katika lugha nyingi duniani. Inaitwa michakato asilia kwa sababu ipo katika lugha zote duniani.
AINA ZA MICHAKATO
  1. Michakato ya kiusilimisho
  2. Michakato isiyo ya kiusilimisho

  1. MICHAKATO YA KIUSILIMISHO
Ni ile inayohusu kufanana kwa kiasi kikubwa kwa vitamkwa kutokana na ujirani (kukaribiana kwake) yaani hupata baadhi ya sifa za kipande sauti chenziye kilicho jirani. Mfano,
  1. MICHAKATO ISIYO YA KIUSILIMISHO
Ni ile inayohusu vitamkwa au sauti ambazo hazifanani kwa kiasi Fulani wakati wa mchakato.
KANUNI ZA KIFONOLOJIA
Ni maandishi rasmi yanayowakilisha michakato asilia. Kanuni hizi zimejikita katika nadharia za Morris Halle na Noam Chomsky waliobainisha muundo wan je na wa ndani wa maneno.
UMBO LA NDANI
Umbo kama lilivyo katika lugha husika ambalo haliwezi kuonesha mchakato.
UMBO LA NJE
Umbo linaloonesha lugha katika utendaji wake (uhalisia wake). Nalo linatuwezesha kujua mchakato.
  1. MICHAKATO YA KIUSILIMISHO
I.                   UNAZALISHAJI WA IRABU (Vowel nasalization)
Ni mchakato ambao irabu hupata baadhi ya sifa za nazali kutokana na yenyewe kutangamana na konsonanti ambayo ni nazali. Mfano,
/muwa/                                  [mũwa]
/nuru/                                    [nũru]
/mama/                                  [mama]
/pãn/                                      [pãn]
/pen/                                      [pẽn]
Irabu zinazotangamana na nazali nazo zinapata sifa ya unazali.
II.UTAMKIAJI PAMWE NAZALI (Homorganic nasal assimilation)
Ni usilimisho unaohusu konsonanti ambayo ni nazali kutamkiwa mahali pamoja na konsonanti inayofuatia. Mfano, mbuzi, ndama, ŋgoma.
III UKAAKAAISHAJI
Ni aina ya usilimisho ambapo konsonanti ambayo hapo awali haikuwa na sifa ya ukaakaa hupata sifa hiyo kutokana na kufuatiwa na kiyeyusho au irabu. Mfano
Ki+a+ku+l+a                                    kya:kula
Ki+etu                                              kyetu

IV.  UYEYUSHAJI
Ni sauti isiyo kiyeyusho inaathiriwa na kuwa kiyeyusho, sauti mbili zinapokutana inatokea sauti moja mfano, irabu zinapotokea katika mazingira Fulani hubadilika na kuwa kiyeyusho. Mfano,
Mu+eupe                                mweupe
Mu+ana                                  mwana
Mu+alimu                              mwalimu
V. MVUTANO WA IRABU/ MUUNGANO WA SAUTI
Sauti mbili hukutana au kuungana hasa irabu ya juu na chini na kupata irabu ya kati. Mfano,
Ma+ino                                  meno
Ma+iko                                  meko
Ma+ini                                   maini
Ma+iti                                    maiti
Hakuna mabadiliko yanayotokea katika mjumuisho wa fonimu.
KANUNI YA KONSONANTI KUATHIRI NAZALI
Mazinrira fulani ya utamkaji konsonanti huathiri nazali iwe inafanana na konsonanti inayofuatia.
Mfano,
M+buzi                                              mbuzi
N+dugu                                             ndugu
N+goma                                             ngoma
N+gombe                                           ŋng’ombe
Konsonanti inayofuatia nazali ndiyo inayoathiri nazali.
NAZALI KUATHIRI KONSONANTI
Yaani nazali ndiyo inayoathiri konsonanti ili konsonanti hiyo ifanane na nazali, mfano,
U+limi                                    ulimi
N+limi                                    ndimi
U+refu                                    urefu
N+defu                                   ndefu
Katamba anasema kuwa mchakato huu ni uimarishaji wa sauti karibu kuna sauti ambazo ni ndefu.

TANGAMANO LA IRABU
Ni usilimisho baina ya irabu na irabu, yaani huathiriana kiasi kwamba hulazimika kufanana. Kufanana, kupeana sifa zinazofanana. Kwa mfano,
Paka                                        pakia
Pika                                                   pikia
Soma                                                 somea
Tupa                                                  tupia
sema                                                  semea

Mofimu ya utendea hubadilika kutokana na irabu inayofuatia mzizi wa neno. Irabu a,i na u] mofimu yake ya utendea ni /i/
Irabu [e,o] mofimu yake ya utendea ni [e].
MICHAKATO ISOUSILIMISHO
A.UDONDOSHAJI
Kitamkwa ambacho awali kilikuwa katika neno kinaondoshwa au kinaangushwa. Mfano
Mu+tu/                                   /mutu/- [mtu]
Mu+toto                                 /mutoto/- [mto]         
Udondoshaji sio katika irabu tu bali hata konsonanti hudondoshwa.
Waliokuja                                             walokuja
Amekwishakula                                   ameshakula
I am going                                            I’m going
I have no food                                     I’ve no food

B.UCHOPEKAJI
Uingizaji wa sauti ambazo hazikuwepo katika neno. Mfano
Kiarabu                                    Kiswahili
Aql                                           akili
Saqf                                          sakafu
Bakhat                                      bahati
C. TABDILI
Ni mchakato ambao kwao sauti mbili zilizo jirani hubadilishana nafasi. Mfano
Nga+wa+reng+a+o = ngwaareengao ‘wanachukua’
Nga+wa+jo+reng+a = ngwaajoreenga = ‘watachukua’
Nga+wa+reng+a = ngwaajoreenga = wanachukua
Ka+wa+tsi+reng+a = ‘hawachukui’






VIARUDHI/ VIPAMBASAUTI
Hizi ni sifa ambazo huambatishwa katika vitamkwa na kuleta maana. Sifa hizi huambatana na vitamkwa asilia kama vile: silabi, neon, kirai na sentensi (vipashio ambavyo ni vikubwa kuliko foni na vinatumika katika mfumo wa lugha). Viarudhi hujumuisha jiografia ya mzungumzaji.
►KIIMBO
Ni upandaji na ushukaji wa mawimbi ya sauti katika usemaji. Kutokana na kiimbo tunaweza kumtambua mzungumzaji kama anauliza swali, ombi, amri, maelezo, kejeli au mshangao.
AINA ZA VIIMBO
(i)                 Kiimbo cha maelezo kwa mfano, Mtoto anakula
(ii)               Kiimbo cha kuuliza kwa mfano, Mtoto anakula?
(iii)             Kiimbo cha kuamuru kwa mfano, Nenda nje
(iv)             Kiimbo cha mshangao kwa mfano, khaa! Mtoto anakula
(v)               Kiimbo cha kejeli, Mtoto anakula

KIDATU
Hii ni sifa ya kiarudhi ambayo hubainishwa na kupanda na kushuka (mpandoshuko) kwa kiwango cha sauti. Kidatu hudokeza maana ya msemaji (kwa msikilizaji). Hali hii hutokana na kasi ya msepetuko wa nyuzi za sauti ndani ya koromeo.
AINA ZA KIDATU
(i)                 Kidatu cha juu
(ii)               Kidatu cha kati
(iii)             Kidatu cha chini
Kwa ujumla kidatu ni kiwango cha juu, cha kati au cha chini katika usemaji.
►LAFUDHI
Ni tofauti ya mzunguzaji kutokana na mazingira na jiografia aliyotoka mzawa wa lugha. Lafudhi huonesha lugha yake ya kwanza.
Mpare neno supu ►thupu
Mnyakyusa chai ► kyai
Mmkonde ► Athumani Achumani
MKAZO
Ni msisitizo / utamkaji wa silabi au neon kwa kutumia nguvu nyingi, hali ambayo huifanya silabi au neno hilo kusikika kuliko silabi nyingine katika neno husika au neno katika tungo.
AINA ZA MKAZO
(i)                 Mkazo mkuu
Huifanya silabi husika kusikika Zaidi kuliko silabi nyingine katika neno, kirai, kishazi au sentensi. Alama ᾽ ndiyo hutumika kuwalikisha mkazo huu.
(ii)               Mkazo wa kawaida
Hauna msikiko mkubwa kama mkazo mkuu ῝ ni alama itumikayo katika unukuzi wake.
Mkazo unaweza kutokea mwanzoni, katikati au mwishoni mwa neno. Kila lugha huwa na utaratibu wa uwekaji wa mkazo. Katika lugha ya Kiswahili mkazo huwekwa katika silabi ya pili kutoka mwisho wa neno.
WAKAA
Ni muda unaotumika katika utamkaji wa fonimu fulani. Wakaa unaweza kuwa mfupi, kawaida na mrefu. Wakaa mrefu huonyeshwa kwa nukta mbili.
Mfano, paa► pa:

TONI
Mgullu (1999) anasema toni ni kiwango cha kidatu pamoja na mabadiliko yake ambayo hutokea wakati mtu anapotamka silabi au maneno. Katika lugha za toni (tonal languages) mabadiliko ya toni hubadili maana za maneno. Hata hivyo ikumbukwe kwamba si kila lugha ina toni, lugha ya Kiswahili kwa mfano na Kinyakyusa (hazina) toni bali zina mkazo. Ni sifa inayowakilisha kiwango pambanuzi cha kidatu cha silabi katika neno au sentensi na ambayo huweza kubadilisha maana ya neno au sentensi hiyo kisemantiki au kisarufi. Tunaweza kupata aina mbalimbali za toni kutokana na utamkaji.
Toni huweza kuwa ya kupanda (rising tone), ya kushuka (falling tone), ya kupanda shuka (rise-fall) na kushuka panda (fall-rise). Wanasimu wengi husema kwamba hapo kale lugha zote za Kibantu, Kiswahili kikiwemo, zilikuwa na toni lakini kutokana na mabadiliko na nyakati ndipo zingine zimepoteza toni hizo. Hili linaonekana katika Kiswahili kwa maneno: barabara na barabara
AINA ZA TONI
Kmsingi kuna aina kuu mbili za toni, yaani toni za kisarufi na toni za kileksika.
(i)                 TONI ZA KISARUFI
Hizi ni zile ambazo zinapotumika katika maneno hazina athari yoyote katika maana bali hufanya kazi za kisarufi kuonyesha aina ya tendo, nyakati n.k. Mifano mizuri ya toni za aina hii ni zile za lugha ya Kiruri
Okutema                                     kata
Okutemera                                  katia
Okutemeranira                            katiana
KISAFWA
Alya                                            anakula
Álya                                            amekula
(ii)               TONI ZA KILEKSIKA
Hizi ni zile ambazo zinapotumika katika maneno hubadili maana ya maneno. Hii ni kusema kwamba neno lile lile huweza kuwa na maana tofauti tofauti kutokana na tofauti ya toni.
KISAFWA
Gula                                            nunua
Gula                                            subiri
Shila                                           kile
Shila                                           nenda/ondoka
Lila                                             lile
Lila                                             lia

SILABI
Ni dhana ya kifonolojia ambayo huwakilisha umbo la matamshi ambapo sauti moja au zaidi hutamkwa kwa mara moja kama fungu moja.
Silabi ni kipashio cha kifonolojia ambacho ni kikubwa kuliko fonimu lakini kidogo kuliko neno katika mfumo wa darajia.
AINA ZA SILABI
1. SILABI HURU/WAZI
Ni silabi ambazo mara nyingi huishia na irabu. Msikiko wake ni mkiubwa.
  1. SILABI FUNGE
Ni silabi ambazo huishia na konsonanti. Msikiko wake ni hafifu. Aghalabu irabu huchukuliwa kama kilele cha silabi. Aidha, irabu ni vitamkwa ambavyo vikitolewa hakuwi na mzuio wa hewa.
NAMNA YA KUWAKILISHA MUUNDO WA SILABI
Kuna wananadharia wanaosema kuwa silabi inaweza kuwasilishwa kwa namna mbalimbali. Pike na Pike (1943) wanasema kuwa muundo wa silabi una matawi na darajia. Baadhi ya wanataaluma wanaona kuwa silabi ina mwanzo na kilele. Wengine hudai kuwa silabi ina upeo na ukingo/mpaka/margin (sehemu ya mwanzo au ya mwisho wa silabi. Kuna wanazuoni wengine kama vile Halle, Harris na Vernaud wanasema kuwa silabi ina vitamkwa vinavyobeba sifa bainifu. Aidha, silabi zenye matawi na darajia zina tia.
Katamba (1996:176) anasema kuwa suala la kuainisha silabi kwa vigezo huru na funge ni la kimapokeo ama kijadi. Hivyo basi tunatakiwa kuangalia silabi husika kama ni nzito au nyepesi.
SILABI NZITO
Ni ile silabi ambayo upeo wake una tawi linalogawanyika.
Kwa mfano;


$lah$

                                                                            6

Mwanzo wa silabi                                                                       upeo wa silabi ah
l
                                                                        Kiini cha silabi                        ukingo wa silabi
                                                                               a                                                     h

SILABI NYEPESI
Ni ile silabi ambayo upeo wake haugawanyiki kwa mfano ba, ma da ,fa ja n.k.
                                                                                    6

                                       Mwanzo wa silabi                            upeo wa silabi
                                                   M                                               a

Mwanzo wa silabi ndio una msukumo wa matamshi. Hivyo basi silabi ma ni huru ni ni nyepesi kwani haina tawi linalogawanyika.
Kila lugha ina muundo wake wa silabi kulingana na idadi ya fonimu zilizopo.
MUUNDO WA SILABI HURU ZA KISWAHILI
  1. Muundo wa irabu pekee kwa mfano katika ua, oa, au
  2. Muundo wa nazali pekee kwa mfano katika mganga, mtoto, mdogo
  3. Muundo wa konsonanti na irabu kwa mfano katika kaka, dada, debe, baba, raha
  4. Muundo wa konsonanti konsonanti na irabu kwa mfano
(a)    Kipasuo+kiyeyusho+irabu kwa mfano, pweke
(b)   Kikwamizo+kiyeyusho+irabu kwa mfano, swaga
(c)    King’ong’o|+kiyeyusho+irabu kwa mfano. Mwaka
(d)   Kikwamizo+kipasuo+irabu kwa mfano spika
(e)    Kipasuo+kiyeyusho+irabu kwa mfano, bweka
  1. Konsonanti konsonanti kiyeyusho na irabu kwa mfano;
(a)    Nazali+kipasuo+kiyeyusho+irabu kwa mfano pingwa
(b)    Nazali +kipasuo+ kiyeyusho+irabu kwa mfano pandwa, undwa
(c)    Nazali+ kikwamizo+kiyeyusho+irabu kwa mfano chinjwa
MUUNDO WA SILABI FUNGE
Aina hizi za silabi haziishii na irabu. Pia huwa hazisikiki na huweza kutokea mwanzoni, katikati au mwishoni mwa neno
MWANZONI MWA NENO
1.      Silabi zenye ukingo /l/ kwa mfano
Alfajiri, almasi, halmashauri, hulka n.k.
2.      Silabi zenye ukingo /s/ kwa mfano
Askari, askofu, desturi, mustarehe, rasmi, hospital, taslimu, wastani n.k.
3.      Silabi zenye ukingo /k/ kwa mfano
Daktari, bakshishi, iktisadi, takribani, aksante, maksai, muktadha, nuksi, nukta n.k.
4.      Silabi zenye ukiongo /r/ kwa mfano
Ardhi, karne n.k.
5.      Silabi zenye ukingo /n/ kwa mfano
Ankra
6.      Silabi zenye ukingo /m/ kwa mfano
Hamsini, mamsapu, alhamudullilah, hamsa n.k.
7.      Silabi zenye ukingo /p/ kwa mfano
Aprili, kaptula, kapteni
8.      Silabi zenye ukingo /b/ kwa mfano
Biblia, kabla, rabsha n.k.
9.      Silabi zenye ukingo /j/ kwa mfano;
Majhununi
SILABI ZENYE UKINGO ZINAZOTOKEA KATIKATI YA NENO
Kwa mfano, mfalme, daftari, eropleni n.k.
SILABI ZENYE UKINGO ZINAZOTOKEA MWISHONI MWA NENO
Kwa mfano jehanam, inshallah n.k.
Kwa ujumla maneno mengi yanayotumia silabi funge mengi ni ya kukopa.
DHIMA YA SILABI
-          Silabi ni kipashio cha msingi ambacho kina dhima ya kifonotaktiki (kanuni ambayo inamruhusu mzungumzaji kutumia mfuatano unaokubalika na kumkataza mfuatano usiokubalika. Kwa mfano, katika Kiswahili hakuna silabi inayoundwa kwa mfuatano kappa. Hivyo basi, muundo wa silabi hutusaidia kujua mfuatano sahihi kulingana na lugha husika.
-          Silabi inatumika kama mawanda ya kanuni za kifonolojia.
-          Silabi ni kama muundo wa kipande sauti changamano. Silabi hupambanua/hudhibiti mfuatano wa sifa thabiti.
-          Silabi ni kipashio ambacho hutumika kuunda vipashio vikubwa zaidi katika taaluma ya fonolojia kama vile toni, shada/mkazo. Pia inatumika kubainisha maana ya kifonolojia, kwa mfano, katika lugha ya Kiswahili tunaweka mkazo katika silabi ya pili kutoka mwisho wa neno.
SIFA MAJUMUI ZA LUGHA KATIKA FONOLOJIA
Madhumuni makubwa ya fonolojia ni kuweka wazi baadhi ya sifa majumui zinazojitokeza katika lugha asilia. Hii inatokana na ukweli kwamba kuna tofauti za wazi zinazojitokeza katika fonolojia ya mifumo mbalimbali ya lugha asilia, bado kuna sifa fulani ambazo zinaelekea kuchangiwa na lugha zote. Sifa zinazoelekea kuchangiwa na lugha zote asilia ndizo zinazoitwa sifa majumui za lugha.
AINA ZA SIFA MAJUMUI ZA LUGHA
(a)   SIFA MAJUMUI HALISI ZA LUGHA
Hizi ni zile sifa za kiisimu ambazo ni za kawaida katika lugha zote za binadamu. Kwa mfano, lugha zote za binadamu huwa na irabu na konsonanti katika orodha ya sauti zake; ingawa idadi ya irabu na konsonanti hizo huweza kutofautiana toka lugha moja hadi lugha nyingine. Vilevile, lugha zote asilia zina silabi, ingawa muundo wa silabi unaweza kutofautiana toka lugha moja hadi lugha nyingine; katika lugha zote asilia irabu na konsonanti hupangiliwa katika silabi.
(b)   SIFA MAJUMUI PANA ZA LUGHA
Hizi ni zile sifa ambazo hupatikana katika lugha nyingi, ingawa sio zote. Kwa mfano, wanaisimu wengi hukubaliana kwamba lugha nyingi za binadamu huwa zina angalau irabu tano. Pamoja na huo ukweli kuna ukweli mwingine kwamba kuna baadhi ya lugha chache ambazo zina irabu saba au zaidi, na kuna lugha nyingine zenye irabu tatu.
(c)    SIFA MAJUMUI TABIRIFU ZA LUGHA
Hizi ni zile sifa ambazo kuwapo kwa sifa moja ya msingi huashiria kuwepo kwa sifa nyingine ambayo inahusiana na hiyo sifa ya msingi. Kwa mfano ikiwa katika lugha kuna tonijuu basi kutakuwa na tonichini pia.


Maoni 209 :

  1. Ahsante. Nukuu zipo vizuri tafadhali naomba mnitumitumie kupitia email yangu hiyo

    JibuFuta
  2. hunguhabibu@gmail.com

    JibuFuta
  3. Kazi nyuri kabisa.naomba unitumie kazi hii ya fonetiki na fonolojia kwenye email yangu...
    mosesnyukuri01@gmail.com

    JibuFuta
  4. Shukrani kwa kazi nzuri Mgaya,naomba ukaweze kunitumia kazi hii kwa edwinkemboik@yahoo.com

    JibuFuta
    Majibu
    1. Hongera kwa kazi nzuri Mgaya, ila nlikua naomba Kama kuna kazi umeanzaa inayohusu jedwali la fonolojia katika lugha ya kijita kifonetiki naomba nitumie kupitia maigapeter4@gmail.com

      Futa
  5. Ahsante kwa uchapisho,naomba kupata Nazi hii tafadhali kwenye email yangu,ntashukuru.

    JibuFuta
  6. elizabethakinyi519@gmail.com

    JibuFuta
  7. elizabethakinyi519@gmail.com

    JibuFuta
  8. nashukuru kwa hiyo kazi njema

    JibuFuta
  9. Naomba kujua uhusiao uliopo baina ya isimu na taaluma nyinginezo

    JibuFuta
  10. Nashukuru nimefaidika sana

    JibuFuta
  11. Mmechambua vzur kwan mada inaeleweka

    JibuFuta
  12. Kazi nzuri maombi ya kunitumia
    emamaskot@gmail.com

    JibuFuta
  13. Kazi nzuri maombi ya kunitumia
    emamaskot@gmail.com

    JibuFuta
  14. Ipo vizuri sana naomba nitumie kwenye email sgwamenyo@gmail.com

    JibuFuta
  15. Asante Daktari kwa kazi nzuri

    JibuFuta
  16. Ni kazi nzuri sana,, naomba unitumie

    JibuFuta
  17. Nawezaje kuzipakua kwa mfumo wa pdf?

    JibuFuta
  18. Kazi iko pouwaa Ila mifano mmenyima

    JibuFuta
  19. Kaz nzur sana mwalimu wangu pendo naomb nitumie kweny email yangu mwalyegob@gmail.com

    JibuFuta
  20. Kitabu hicho kameandikwa na nani msaada

    JibuFuta
  21. Nashukuru nimefaidikaaaaaaaaaaaaa sanaaaaaa

    JibuFuta
  22. Iko vizuri sana naomba nitumiwe kwenye enail sgwamenyo@gmail.com

    JibuFuta
  23. Ingiza maoni yako...Kazi nzuri sana ya fonolojia ya kiswahili

    JibuFuta
  24. Nukuu zipo vizuri sana zimenisaidia Sana katika usomaji

    JibuFuta
  25. Asante kwa uchapishaji naomba kupata nakala hii kwa (email) yangu

    JibuFuta
  26. Asante kwa uchapishaji naomba kupata nakala hii kwa (email)yangu

    JibuFuta
  27. Naomba nakala hii kwenye email yangu, Nazi nzuri

    JibuFuta
  28. Nitumie madam

    Pslaa745@gmail.com

    Or

    Peteralbini24@gmail.com

    JibuFuta
  29. Uko vizuri madam jmn,ntumieee

    JibuFuta
  30. Nimependa hongera Sana Zaid ya sana

    JibuFuta
  31. Naomba unitumie email Lucylucykikoso@gmail

    JibuFuta
  32. Naomba matini ya hii kazi ikiwezekana pamoja na ya mofu,alomofu na mofimu
    Email:geoffreyomache@gmail.com

    JibuFuta
  33. Dah! Kazi nzuri naomba unitumie kwenye email ,dominicusanna@gmail.com

    JibuFuta
  34. halafu matini hii naomba unitumie kwenye email:malekelaamani@gmail.com

    JibuFuta
  35. vyema sana. nitumie kwenye mail yangu tafadhali ochiengbrian345@gmai.com

    JibuFuta
  36. Kazi nzuri Sana kiukweli unatusaidia kupata maarifa ya kutosha juu ya hili Somo, Mungu akubariki

    JibuFuta
  37. Kazi nzuri sana,, kwa hakika nitakushukuru sana naomba unitumie matini hii kwa Email yangu, emmanuellawei2@gmail.com

    JibuFuta
  38. Ni kazi nzuri sana yenye mpangilio unaosomeka na kueleweka.

    JibuFuta
  39. Hiki kitabu naweza kukipa wapi nipo Arusha.

    JibuFuta
  40. Vizur Sana kazi nzuri hii,,naweza kupata matiniyake tafadhali

    JibuFuta
  41. hamis Magwe@gmail.com

    JibuFuta
  42. Kazi safi nitumei
    kipkorirfrankline3@gmail.com

    JibuFuta
  43. Kazi nzurii mungu akupe wepesi katika majukumu yako

    JibuFuta
  44. Kazi nzuri nimefahamu mengi

    JibuFuta
  45. Kazi nzuri sana,naomba unitumie kwa email yngu ka pdf

    JibuFuta
  46. Hii ni kazi Nzuri sana hongera kwako nitumie kwenye barua Pepe tafadhali purityjepchumba2000@gmail.com

    JibuFuta
  47. Kazi kuntu! Naweza kupata makala haya

    JibuFuta
    Majibu
    1. Sharon Achieng,nahitaji nalala hii,ntaipata vipi?

      Futa
  48. The best article 👌👌..napenda kazi yako..naomba unitumie hii yote tafadhali.. daviskiptoo600@gmail.com

    JibuFuta
  49. Naomba kujua uhusiano uliopo baina ya fonetiki na fonolojia

    JibuFuta
  50. Kaz ni nzur sana nimeipend, nashaur ungeweka na makosa ya kifonolojia

    JibuFuta
  51. Kiukweli hili ni chapisho bora linaloweza kumsaidia mtu kujifunza fonolojia na fonetiki kwa ujumla. Nimependa na nashukuru

    JibuFuta
  52. Mme eleza vizuri lakini kwanini msinge weka tofauti bainifu mojakwamoja kwenye mlolongo unaoeleweka

    JibuFuta
  53. Kaka kazi nzuri sana, naomba nisaidie kupata dhana ya mvutano wa irabu!

    JibuFuta
  54. Nisaidie dhana ya mvutano wa irabu! Ntumie kwa email 👉 www.ayubumpiluka@gmail.com

    JibuFuta
    Majibu
    1. Na mm pia nahitaji

      Kwa email hii sanjodaud@gmail.com

      Futa
  55. Kazi nzuri kabisaa...nimefurahia...hongera

    JibuFuta
  56. Hongera kwa kazi nzuri,, tushirikiane katika kukikuza kiswahil chetu

    JibuFuta
  57. Jamani naomba kutumiwa uhusiano uliopo kati ya fonetiki na fonolojia

    JibuFuta
    Majibu
    1. Fonolojia inachota sauti katika fonetiki kisha kuzichambua kwa umahususi kulingana na lg husika.

      Ili kuzielewa sauti za kifonetiki na kuzipa maana ni sharti uhusishe fonolojia

      Matawi haya yote yanashirikiana katika uchunguzi wa sauti za lg ya mwanadamu.

      Futa
  58. Kaz nzur,pia ningeomba kujua fonetik na fonolojia znahusina vp na kukamlshana vp?

    JibuFuta
  59. Kaz nzur sana Mungu akubariki

    JibuFuta
  60. Hakika kazi ninzuri sana naomba unitumie naimi
    lwigadima24@gmail.com

    JibuFuta
  61. Kazi nzuri Sana mwalimu wangu.

    JibuFuta
  62. Kazi Nauru,naomba nitumie Kwa henryambale1992@gmail.com

    JibuFuta
  63. Kongole kwako kwa kazi nzuri. Kizuri hakikosi kasoro, ongeza ufafanuzi wa taarifa za wataalamu wa simu

    JibuFuta
  64. Hii kazi kwa kweli no nzuri naomba unitumie katika
    email yangu (abdullafathia7@gmail.com.

    JibuFuta
  65. Kazi nzuri mno mpendwa mungu akubariki

    JibuFuta
  66. Kazi nzuri Sana,kongole .naomba kutumiwa kazi hii
    sophynanjila@gmail.com

    JibuFuta
  67. Imeeleweka sana mimi binafsi sijaona mapungufu ata kama yapo ni kidogo ila inaeleweka

    JibuFuta
  68. Heko mkuu wangu, zidi kutufahamisha zaidi juu ya isimu kama taaluma na uhusiano wake na taaluma nyingine nitashukuru

    JibuFuta
  69. Nazi safi sana,,,can you sent me via email please

    JibuFuta
  70. Kazi nzr,na pongez kwa mwl husika bila ingefaa cn kama ningetumiwa

    JibuFuta
  71. Umeiva mlm naomba unitumie antidiusjames1999@gmail.com

    JibuFuta
  72. Habari mkuu, naomba kujua fonolojia ya kihaya tu

    JibuFuta
  73. Heko ,Kazi safi

    Naomba mnitumie nakala hii kwenye nakala yangu ya maenapeter331@gmail.com

    JibuFuta
  74. Naomba jibu kwa swali hili...jadili utumikizi wa taaluma ya fonolojia katika isimu pedagojia

    JibuFuta
  75. Umetusaidia sana mkuu 🙏🙏🙏

    JibuFuta
  76. Inapendeza, iko vizuri

    JibuFuta
  77. Kongole.kazi njema.imetufaidi hasaa mimi

    JibuFuta
  78. Taja sifa zizazofananisha fonetiki na fonolojia

    JibuFuta
  79. Honger docta kwa kazi nzuri

    JibuFuta
  80. Shukrani sana somo limenoga

    JibuFuta
  81. Somo lilo vizuri ila sijaona marejeleo

    JibuFuta
  82. Kazi nzuri sana hiyo naomba unitumie kwenye email yangu hii ndalahwadepow@gmail.com

    JibuFuta
  83. Zile kanuni za kifonolojia tisaidie kuongeza hapo mwalimu

    JibuFuta
  84. Umenitoa kwenye Giza nene mwalimu asante Sana kwa kuniangazia nuru

    JibuFuta
  85. Umenitoa kwenye Giza nene mwalimu asante kwa somo lililonipa Nuru Tena

    JibuFuta
  86. Asantee sana umenisaidia vp naweza nikadowload hizi nukuu?

    JibuFuta
  87. Ahsante kwa kutupatia chakula hiki Cha ubongo,, ila utusaidie na marejereo yake

    JibuFuta
  88. Andika na marejereo itakuwa vyema zaidi

    JibuFuta
  89. Naomba kutumiwa nalala hii kwenye email, achiengsharon2003@gmail.com tafadhali

    JibuFuta
  90. Naomba kujua tofauti kati ya toni na mkazo

    JibuFuta
  91. hongera na pi kama mtu anahitaji zaidi kazi zako mbali na huku tutakupatia wapi docta

    JibuFuta
  92. Kazi nzuri sana,,, naomba kupata nakala halisi ya kazi hii,,, pia ushauri wangu jitahidi uweke katika nakala ngumu- hard copy ili watu waipate Kwa urahisi. Mungu akubariki Sana,, naitwa Joseph Sabas kapinga nipo hapa chuo kikuu Cha katoliki Cha Ruaha (RUCU)

    JibuFuta
  93. Shukrani kazi nzuri sana

    JibuFuta
  94. Lucas naomba unipe tofauti Kati ya fonetiki na fonolojia ukiangazia katika uainishaji wa sauti zake

    JibuFuta
  95. Asante Sana hakika endelea kukomboa kizazi, mungu hakupe AFYA njema kila wakati.

    JibuFuta
  96. Naomba unitumie mwanahawaomari49@gmail.com

    JibuFuta
  97. Heko ndugu,japo ningeomba unieleze umuhimu wa sauti (foni),katika fasiri ya lugha.
    agukoerick@gmail.com

    JibuFuta
  98. kazi nzuri sanaaaaaa

    JibuFuta
  99. Ongera kwa kazi yako nzuri naomba unitumie izi notes kwa hii Gmail account (julieekas15@gmail.com) shukrani

    JibuFuta
  100. Hongera kwa maelezo mufti. kutumia kazi hii nimeweza kusaidika katika kuufunya mjarabu wangu wa shahada ya ualimu. Shukrani

    JibuFuta
  101. Sijawahi kupata kazi iliyopangwa kwa umakinifu kama hii.
    Nimetosheka yaani.
    Kongole

    JibuFuta
  102. Naomba unisaidie na nakala ya foni za lugha na vigezo vya huainishaji wa foni

    JibuFuta
  103. Asante dakatari
    Nimejifunza Sanaa
    Ila napenda kujua phonological sequence za kiswahili kwa maana ya wepesi wa matamshi na cognitive sequence as well
    Mmfano mtoto hawezi tembea kabla hajaweza kukaza shingo, kukaza,kutambaa, kusimama na kutembea
    Je kwenye lugha yeti ya kiswahili sequence ya kujifunza sauti za kiswahili ipoje
    Tmfano kama nataka nimfundishe mtoto mdogo kabisa au mtoto mwenye ulemavu wa akili AmBAe ulewa ni kidogo kabisa naazia na herufi gani kwa maana ya wepesi wa matamshi na pia akili
    Nitafurahi ukiweza nijibu @rayahamad85@gmail.com

    JibuFuta
  104. Kazi nzuri sana

    JibuFuta
  105. Kazi safi kwelikweli

    JibuFuta
  106. Hongera sana Kwa maelezo mufti,Kasi yenu imefana sana

    JibuFuta
  107. Kazi nzuri ila jaribu kuweka na marejeleo yake na kama unayo naomba nitumie kwa email hii antidiustrazias@gmail.com

    JibuFuta
  108. Hongera ...umenisaidia sana

    JibuFuta
  109. Hongera kwa njema kazi naomba nitumie hii kazi kwa email hii plz kibonaclever123@gmail.com

    JibuFuta
  110. Lwerera mwanaisimu29 Novemba 2022, 19:22

    Shukrani zilizoje kwako

    JibuFuta
  111. Naomba unitumie kwa mtandao lwereravaizal@gmail.com tafadhali kwa lengo la kuboresha kiswahili lugha ashirafu🙏

    JibuFuta
  112. Asante sana Kwa SOMO zuri, nami naomba unitumie kwenye email yangu, johnemanuel600@gmail.com

    JibuFuta
  113. Kazi njema sana

    JibuFuta
  114. Shukran sana.tafadhali naomba unitumie kwenye email yangu.ngudemasanja22@gmail.com

    JibuFuta
  115. Kazi nzur lakini marejeleo hatuyaoni ni vyema ukaandika

    JibuFuta
  116. Naomba nitumie notice hizo kwenye email make nmezipenda ni nzuri sana

    JibuFuta
  117. Nimeziependa naomba na mim nitumie kwa email

    JibuFuta
  118. Kazi powaaaa

    JibuFuta
  119. Kongole kazi Safi sana

    JibuFuta
  120. Naomba nitumie Kwa email amosnguda@gmail.com

    JibuFuta
  121. Naomba unitumie makala haya kwenye email valevugu415@gmail.com tafadhali 🙏🙏

    JibuFuta
  122. Kazi safi sana kiongozi. Naomba tafathali unitumie kwa joshuasmumo@gmail.com' nitashukuru sana

    JibuFuta
  123. Kazi safi sana kiongozi. Naomba tafathali unitumie kwa ' joshuasmumo@gmail.com ' nitashukuru mno

    JibuFuta
  124. Kari safi mno

    JibuFuta
  125. Kazi nzuri.....lakini hakuna marejeleo

    JibuFuta
  126. Nimezipenda sana

    JibuFuta
  127. Kazi nzuri sana

    JibuFuta
  128. Pongezi kwa kazi nzuri na iliyo bora zaidi

    JibuFuta
  129. Naomba nitumie kwenye email yangu rahelsigala@gmail.com

    JibuFuta
  130. Naomba marejeleo

    JibuFuta
  131. Kazi nzuri sana

    JibuFuta
  132. HERBERT MASINDE1 Desemba 2023, 06:36

    NINASHUKURU SANA DAKTARI,NIMEFAIDIKA SANA

    JibuFuta
  133. Shukran za dhati ziwafikie wataalam bora

    JibuFuta
  134. Nimependa chapisho hili naomba kutumiwa kwa njia ya email yangu hiyo ngelomungulu55@gmail.com

    JibuFuta
  135. Naomba kujua tofauti baina ya fonolojia ya vitamkwa na fonolojia arudhi?

    JibuFuta
  136. Kwalanda N William kAZI njema kabisa shukran kabisa hongera

    JibuFuta
  137. Kazi njema hii

    JibuFuta
  138. Kazi nzuri kazi imetulia na inaeleweka, naomba unisaidie hii kazi kwa kutuma kwa email yangu thelezakatale@gmail.com

    JibuFuta
  139. Lazi nzuri sana hongera

    JibuFuta
  140. Shukrani nukuu nzuri

    JibuFuta
  141. Kazi nzuri sana tafadhari nitumie bonkehahara2000@gmail.com

    JibuFuta
  142. Naomba nukuu yake Yan hizi notes anitumie

    JibuFuta
  143. Kazi nzurii ya kupendeza mawazoo na akili ya mswahili.shukran sana

    JibuFuta
  144. Kazi nzuri kwa sisi wageni wa haya mambo

    JibuFuta