Alhamisi, 2 Agosti 2018

Sura ya 2 Mguu wa Kushoto wa Kuzimu


Sura ya 2

Mguu wa Kushoto wa Kuzimu na Mary K Baxter 


Harufu chafu iliijaza hewa. Yesu aliniambia, " Katika mguu wa kushoto wa kuzimu kuna
mashimo mengi. Shimo hili limegawanyika kwenda sehemu nyingine za kuzimu,
lakini tutatumia muda kadhaa katika mguu wa kushoto kwanza. Mambo
unayokwenda kuyaona yatakuwa nawewe daima. Ulimwengu lazima ujue juu ya
uhalisi wa kuzimu. Wenye dhambi wengi na hata baadhi ya watu Wangu hawaamini
kuwa kuzimu ni halisi. Umeteuliwa na Mimi kufunua ukweli huu kwao. Mambo yote
nitakayokueleza kuhusu kuzimu na mambo mengine nitakayokueleza ni ya kweli.
Yesu alijihihirisha kwangu kama mwanga mkali, mwangavu kuliko jua. Umbile la mtu
lilikuwa katikati ya mwanga ule. Wakati mwingine nilimuona Yesu kama mwanadamu,
lakini wakati mwingine alikuwa katika hali ya roho.
Alizungumza tena, "Mwanangu, ninaposema ni Baba amesema. Baba na Mimi ni
wamoja. Muhimu kuliko yote kumbuka upendo na kusameheana. Sasa njoo,
nifuate.
Tulipokuwa tukitembea, pepo wachafu walikuwa wanakimbia kutoka kwenye uwepo wa
Bwana. “O Mungu, O Mungu”, Nililia. “Nini zaidi?”
Kama nilivyosema awali, kuzimu nilikuwa na uelewa wangu wote. Wote walioko kuzimu
wana uelewa wao wote. Wa kwangu ulikuwa unafanya kazi kwa nguvu zote. Hofu ilitanda
kila upande, na hatari zisizoelezeka zilijificha kila mahali. Kila hatua niliyosogea ilikuwa
ilikuwa hatari zaidi kuliko iliyotangulia.
Kulikuwa na milango mfano wa madirisha madogo, ikifunguka na kufunga haraka sana juu
ya shimo. Mayowe yalijaza hewa viumbe viovu viliporuka karibu nasi, vikienda nje na juu
ya malango ya kuzimu. Mara tulikuwa mwisho wa shimo. Nilikuwa nikitetemeka kwa woga
kwa sababu ya hatari na hofu iliyotuzunguka.
Nilishukuru sana kwa ulinzi wa Yesu. Namshukuru Mungu kwa nguvu za uweza wake za
kutulinda, hata katika mashimo ya kuzimu. Hata katika ulinzi huo, nilikuwa nawaza, Sio
kwa mapenzi yangu, Baba, bali mapenzi yako yafanyike.
Niliutazama mwili wangu. Kwa mara ya kwanza niligundua kwamba nilikuwa katika hali
ya roho, na taswira yangu ilikuwa kama nilivyo.
Yesu na mimi tulichepuka kutoka kenye pango kwenda kwenye njia iliyokuwa na vipande
vya ardhi kila upande. Kulikuwa na mashimo ya moto kila mahali mpaka upeo wa macho.
8
Mashimo yalikuwa na upana wa futi nne na urefu wa futi tatu na umbo lake lilikuwa kama
bakuli. Yesu alisema,"Kuna mashimo mengi ya aina hii katika mguu wa kushoto.
Njoo, nitakuonyesha baadhi yake."
Nilisimama na Yesu kwenye njia na kuchungulia kwenye mojawapo ya mashimo. Kiberiti
kilisiribwa kwenye kuta za shimo na kiliwaka kama makaa makali ya moto. Katikati ya
shimo kulikuwa na roho iliyopotea iliyokufa na kwenda kuzimu. Moto ulianzia chini ya
shimo, ukapanda juu na kuifunika roho ile katika ndimi za moto. Mara moto hufifia, halafu
tena kwa mvumo wa sauti huenda tena kwenye roho inayoteseka katika shimo.
Nilipotazamaniliona roho iliyopotea iliyokuwa katika shimo ilikuwa imefungiwa katika
mifupa. “Bwana wangu,” nililia kwa kuona hali ile, “Huwezi kuwafungulia wakatoka?” Lo,
hali hii inasikitisha! Niliwaza, ningeliweza kuwa ndio mimi. Nilisema, “Bwana, angalia
inavyosikitisha kuona kwamba mle ndani kuna roho inayoishi.”
Nilisikia sauti ikitoka katikati ya shimo la kwanza. Niliona umbo kwa mfano wa mifupa
(skeleton) ikilia, “Yesu, nihurumie!”
"O, Bwana!" Nilisema. Ilikuwa ni sauti ya mwanamke. Nilimwangalia na kutaka kumvuta
kutoka kwenye shimo la moto. Hali yake iliniuma sana moyo.
Mifupa ya mwanamke iliyokuwa na na rangi ya zambarau na ukungu ndani ilikuwa
inazungumza na Yesu.Nilimsilikiza kwa mshangao. Nyama iliyooza ilining’inia kwa
vipande vipande kwenye mifupa yake, na ilipokuwa inaungua iliangukia chini ya shimo.
Mahali ambapo awali palikuwa na macho palikuwa mashimo matupu. Hapakuwa na
nywele.
Moto ulianza kwenye miguu yake kama moto mdogo na ukaendelea kukua ulipokuwa
unapanda kwenye mwili. Ilionekana kama mwanamke Yule aliendelea kuungua tu, hata
wakati moto umepungua sana. Kutoka ndani yake kabisa yalitoka mayowe na vilio vya
kukata tamaa.”Bwana, Bwana, nataka kutoka humu!”
Alijaribu mara nyingi kumfikia Yesu. Nilimtazama Yesu, alikuwa na huzuni kubwa katika
sura yake. Yesu aliniambia, "Mwanangu, upo hapa pamoja nami ili kuujulisha
ulimwengu kwamba malipo ya dhambi ni mauti, kwamba kuzimu ni halisi.
Nilimwangalia tena yule mwanamke, na mafunza yalikuwa yanatoka kwenye mifupa ya
skeleton yake. Hayakudhurika na moto. Yesu aliniambia, "Anafahamu na anayasikia
mafunza hayo katika mwili wake."
Mungu mhurumie!” Nililia moto ulipofikia kilele chake na ule uchomaji ulianza kwa mara
nyingine. Kilio kikubwa na kwikwi kilitigisha mwanamke-roho. Alikuwa amepotea.
9
Hapakuwa na njia ya kutokea. “Yesu, kwanini yupo hapa?” Niliuliza kwa sauti ndogo,
maana nilikuwa naogopa kwelli kweli.
Yesu aliniambia, "Njoo."
Njia tuliyokuwa tunapita ilikuwa na mizunguko, ikizunguka kwenye mashimo haya kwa
kadri ya upeo wa macho. Vilio vya wafu waishio, vikichanganyikana na mayowe, vilikuja
kwenye masikio yangu kutoka kila upande. Hakukuwa na wakati wa utulivu kuzimu.
Harufu nzito ya ya uozo wa nyama ilitapakaa hewani.
Tulifika kwenye shimo lingine. Ndani ya shimo hili, ambalo ukubwa wake ulikuwa sawa na
lile lingine, kulikuwa na skeleton nyingine. Sauti ya mwanaume ililia kutoka shimoni,
ikisema, “Bwana, nihurumie.” Ni pale tu walipozungumza ndipo nilipoweza kujua kama ni
mwanamke au mwanaume.
Vilio vikubwa vya mayowe vilitoka kwa mwanaume huyu. “Nimekosa, Yesu, nisamehe.
Nitoe humu. Nimekuwa mahali hapa pa mateso miaka mingi. Ninakusihi, nitoe.” Kilio cha
kwikwi kilitisa skeleton hii. “Tafadhali Yesu, nitoe.” Nilimtaza Yesu nikaona kwamba naye
alikuwa analia.
Bwana Yesu,mtu huyo alilia kutoka shimo la moto, “ sijateseka vya kutosha kwa
dhambi zangu? Imepita miaka arobaini tangu nilipokufa.”
Yesu alisema, "Imeandikwa, Wenye haki wataishi kwa imani!’ Wenye dharau wote na
wote wasioamini watakuwa na fungu lao katika ziwa la moto. Hukutaka kuamini
kweli. Mara nyingi watu wangu walitumwa kwako kukuonyesha njia, lakini
hukuwasikiliza. Uliwacheka na uliikataa injili. Ingawaje nilikufa msalabani kwa ajili
yako, ulinikebehi na hukutaka kutubu dhambi zako. Baba yangu alikupa fursa
nyingi za kuokolewa. Heri ungelisikiliza.” Yesu alilia.
"Najua Bwana, Najua Bwana!” Yule mtu alilia. “Lakini sasa natubu.”
"Umechelewa," Yesu alisema. "Hukumu imetolewa."
Yule mtu aliendelea, “Bwana, baadhi ya watu wangu watakuja huku, kwa maana nao
hawatatubu. Tafadhali, Bwana, niruhusu niende nikawaambie kwamba ni lazima watubu
dhambi zao wangali duniani. Sitaki waje huku.”
Yesu alisema, "Wanao wahubiri, waalimu, wazee wa kanisa-wote hao wanahubiri
injili. Vile vile wana bahati ya kuwa na njia za kisasa za mawasiliano na njia nyingine
nyingi za kujifunza kuhusu Mimi. Niliwapelekea watumishi ili waweze kuhubiriwa na
kuokoka. Kama hawaamini wanaposikia injili, basi hawatasikia hata mtu akifufuka
katika wafu.
10
Aliposikia hivi mtu yule alighadhabika sana akaanza kutukana. Maneno machafu, ya
kufuru yakatoka kwake. Nilitazama kwa mshangao nilipoona moto ukipanda kwenye
skeletoni na nyama iliyooza ikaanza kuungua na kudondoka. Ndani ya mifupa hii ya mtu,
niliona roho yake. Ilikuwa kama ukungu wa zambarau, na uliijaza mifupa yake.
Yesu alisema, "Kuzimu ni halisi, na hukumu ni halisi. Nawapenda sana , mwanangu.
Huu ni mwanzo tu wa mambo ya kutisha nitakayokuonyesha. Kuna mambo mengi
zaidi yanakuja. Uambie ulimwengu kwa niaba yangu kwamba kuzimu ni halisi,
kwamba wanaume na wanawake lazima watubu dhambi zao. Njoo, nifuate. Lazima
tusonge mbele.
Katika shimo lingine kulikuwa na mwanamke mdogo sana aliyekuwa na umri wa labda
miaka themanini. Siwezi kueleza namna nilivyojua umri wake lakini nilijua tu. Ngozi
ilitolewa kwenye mwili wake kwa moto endelevu, ilibaki mifupa tu ikiwa na roho kama
mvuke mchafu ndani yake. Niliangalia moto ulivyokuwa unamuunguza. Mara ilibaki mifupa
tu na mafunza yakizunguka ndani, ambayo moto haukuweza kuyaunguza.
"Bwana, inatisha!" Nililia. " Sijui kama naweza kuendelea, maana inavyotisha vigumu
kuamini." Kwa kadri ya upeo wa macho yangu roho zilikuwa zinaungua kwenye mashimo
ya moto.
" Mwanangu, ndio maana upo hapa." Yesu alijibu. "Nilazima ujue na uelezee ukweli
wa kuzimu. Mbingu ni hakisi! Kuzimu ni halisi! Twende, hatuna budi kusonga
mbele.
Niligeuka na kumtazama yule mwanamke. Vilio vyake vilikuwa vinasikitisha sana.
Nilipomwangalia, aliiweka mifupa ya mikono yake kama kwamba anasali. Nilishindwa
kujizuia kulia. Nilikuwa katika hali ya roho, na nilikuwa nalia. Nilijua kwamba watu wa
kuzimu walikuwa na ufahamu wa aina hii pia.
Yesu aliyajua mawazo yangu. "Ndio, mtoto," alisema, "Wanafahamu. Watu wajopo
hapa, wana ufahamu ule ule na mawazo kama walipokuwa duniani. Wanazikumbuka
familia na marafiki wao na nyakati zote walipokuwa na nafasi ya kutubu lakini
hawakutubu. Kumbukumbu iko pamoja nao wakati wote. Heri wangeliamini injili na
kutubu bila kuchelewa.
Nilimwangalia yule mwanamke kwa mara nyingine, na safari hii nilligundua kwamba ana
mguu mmoja tu. Na ilionekana kama mashimo yamechimbwa kwenye mifupa ya kiuno.
Hii ni kitu gani, Yesu?” Niliuliza.
Alisema "Mtoto, alipokuwa duniani alikuwa na kansa na alikuwa katika maumivu
makali. Upasuaji ulifanyika ili kuokoa maisha yake. Alilala akiwa mwanamke
mwenye uchungu kwa miaka mingi. Watu wangu wengi walikwenda kumuombea na
11
kumwambia kwamba naweza kumponya. Alisema, Mungu ndiye amenifanya hivi’ na
hakuweza kutubu na kuamini injili. Aliwahi hata kunijua wakati mmoja, lakini
baadaye alikuja kunichukia. Alisema kwamba hamuhitaji Mungu na hakutaka mimi
nimponye. Bado niliendelea kumbembeleza, nikitaka kumsaidia, nikitaka kumponya
na kumbariki. Alinipa kisogo na kunilaani. Alisema alikuwa hanihitaji. Roho yangu
ilimbembeleza. Hata baada ya kunipa kisogo, niliendelea kumvuta kwangu kwa
Roho wangu, lakini hakutaka kusikia. Mwishoni alikufa na kuja hapa.
Yule mwanamke alimlilia Yesu, “Bwana Yesu, tafadhali nisamehe sasa. Nasikitika
kwamba sikutubu nilipokuwa duniani. Kwa uchungu alimlilia Yesu, “Laiti ningelitubu bila
kuchelewa. Bwana, nisadie, nitoe hapa. Nitakutumikia. Nitakuwa mtu mwema. Sijateseka
vya kutosha? Kwanini nilisubiri mpaka nikachelewa? Oh, Kwanini nilisubiri mpaka Roho
wako alipochoka kushindana nami?”
Yesu alimwambia, "Ulikuwa na nafasi ya kutubu na kunitumikia.
Huzuni ilidhihirika kwenye uso wa Yesu alipoondoka mahali pale.
Yule mwanamke alivyokuwa analia, niliuliza, “Bwana kinafuata nini?”
Nilihisi hofu kila upande. Huzuni, vilio vya uchungu, na umauti vilitanda mahali pote. Yesu
na mimi tulitembea kwa huzuni hadi shimo lingine. Niliweza kosogea mbele kwa sababu
ya nguvu zake tu. Hata baada ya kitambo kirefu niliendelea kusikia vilio vya toba na
msamaha vya yule mama. Nilitamani kuwa na namna ya kumsaidia. Mkosaji, usisubiri
mpaka Roho wa Mungu anaacha kushindana na wewe.
Kwenye shimo lingine kulikuwa na mwanamke amepiga magoti, kama kwamba anatafuta
kitu. Skeletoni yake ilikuwa na matundu mengi. Mifupa yake ilikuwa inaonekana, na nguo
yake iliyokuwa imechanika ilikuwa imeshika moto. Kichwa chake hakikuwa na nywele, na
kulikuwa na mashimo tu mahali ambapo palistahili kuwa na macho. Moto mdogo ulikuwa
unawaka kuzunguka pale alipokuwa amepiga magoti, na aliparua kwa makucha pembe za
kiberiti. Moto ulishikilia kwenye mikono yake, na nyama mfu iliendelea kudondoka kama
mavi ya ng’ombe.
Kilio kikubwa kilimtikisa. “O Bwana, O Bwana,” alilia, “Nataka kutoka” Tulipozidi kuangalia
hatimaye alifika mwisho wa shimo kwa miguu yake. Nilidhani angetoka ndipo pepo kubwa
lenye mabawa makubwa yaliyoonekana kuvunjika juu na kuning’inia kwenye mabega
lilimkimbilia. Rangi yake ilikuwa zambarau nyeusi na alikuwa na minywele mwili mzima.
Macho yake yalibonyea ndani ya kichwa, na umbo lake lilikuwa kama mbweha mkubwa.
Yule pepo alimkimbilia yule mwanamke na kumsukumia kwenye shimo la moto kwa
nguvu. Niliangalia kwa mshangao alipotumbukia. Nilimsitikikia. Nilitamani kumchukua
katika mikono yangu na kumkumbatia, kumwomba Mungu amponye na kumtoa mle.
12
Yesu alitambua mawazo yangu na akasema, "Mwanangu, hukumu imekwisha
kutolewa. Mungu amesema. Hata alipokuwa mtoto nilimwita na kumuita ili
anitumikie. Alipokuwa na umri wa miaka kumi na sita, nilimwendea na kusema,
‘Nakupenda, nipe maisha yako na nifuate, kwa maana nimekuita kwa kusudi
maalum: nilimwita maisha yake yote, lakini hakutaka kusikiliza. Alisema, ‘Siku moja
nitakutumikia. Kwa sasa sina muda na wewe. Sina muda, sina muda, nina maisha
yangu ya starehe. Sina muda, sina muda wa kukutumikia Yesu. Kesho
nitakutumikia.’, Kesho haikufika, alichelewa
Yule mwanamke alimlilia Yesu, “Roho yangu iko kwenye mateso hasa. Hakuna njia ya
kutokea. Najua kwamba niliupenda ulimwengu badala ya kukupenda wewe, Bwana.
Nilitaka utajiri, sifa, na mali, na nilivipata. Niliweza kununua chochote nilichokihitaji;
nilikuwa bwana wangu mwenyewe. Wakati wangu nilikuwa mwanamke mzuri kupita wote,
mwenye kujua kuvaa kuliko wote. Nilikuwa na utajiri, sifa na mali, lakini niligundua
kwamba nisingweza kwenda navyo kaburini. O Bwana kuzimu kunatisha. Sina kupumzika
mchana na usiku. Kila wakati niko kwenye mateso na maumivu. Nisaidie Bwana,” alilia
Mwanamke alimwangalia Yesu kwa shauku na kusema, Bwana wangu mwema, laiti
ningekusikiliza. Nitajuta milele. Nilipanga kuja kukutumikia siku moja-nitakapokuwa tayari.
Nilidhani ungelikuwapo kwa ajili yangu wakati wote. Kumbe nilikosea! Nilikuwa
mmojawapo wa wanawake walikokuwa wanapendwa sana wakati wangu kwa sababu ya
urembo wangu. Najua kwamba Mungu alikuwa ananiita ili nitubu. Wakati wa maisha
yangu yote alinivuta kwa kamba za upendo, na nilidhani ningeweza kumtumia Mungu
kamanilivyokuwa nawatumia wengine. Nilidhani angekuwapo wakati wote. Ndio,
nilimtumia Mungu! Alijaribu sana kunifanya nimtumikie, ambapo wakati wote nilidhani
simuhitaji. Kumbe nilikosea! Shetani alitumia urembo wangu na fedha zangu, na mawazo
yangu yote yaligeukia kwenye nguvu ambazo angenipa. Hata hivyo Mungu aliendelea
kunivuta. Lakini niliwaza, ipo kesho na kesho kutwa. Ndipo siku moja nilipokuwa kwenye
gari dereva wangu aligonga nyumba,nikafa. Bwana, tafadhali nitoe.” Alipokuwa
anazungumza mikono yake iliyokuwa mifupa mitupu ilijaribu kumshika Yesu wakati moto
unaendelea kumchoma.
Yesu alisema, "Hukumu imetolewa."
Machozi yalimdondoka tuliposogea kwenye shimo lingine. Nilikuwa nalia ndani kwa ndani
juu ya uchungu wa kuzimu. “Bwana Mpendwa,” nililia, “mateso haya ni halisi mno. Roho
ikija huku hakuna matumaini, hakuna maisha, hakuna upendo. Kuzimu ni halisi mno.”
Hakuna namna ya kutoka, niliwaza. Lazima aungue milele kwenye moto huu.
"Muda umekwisha, "Yesu alisema. "Tutakuja tena kesho."
13
Rafiki, kama unaishi katika dhambi tafadhali tubu. Kama umezaliwa mara ya pili lakini
umempa Mungu kisogo, tubu na mrudie mara moja. Ishi vizuri na simamia kweli. Amka
kabla hujachelewa, na unaweza kuwa na Bwana milele mbinguni.
Yesu alisema tena, "Kuzimu ina mwili (kama mwili wa mwanadamu) umelala chali
katikati ya dunia. Kuzimu ina umbo kama la mwanadamu, kubwa sana na lenye
vyumba vya mateso vingi sana. Kumbuka kuwaambia watu wa dunia kwamba
kuzimu ni halisi. Mamilioni ya roho zilizopotea ziko huko, na nyingine zinakwenda
huko kila siku. Siku ya Hukumu, kifo na kuzimu vitatupwa katika ziwa la moto, hiyo
itakuwa mauti ya pili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni