Jumapili, 19 Septemba 2021

NINI CHANZO CHA MGAWANYIKO MIONGONI MWA WASABATO

 

MGAWANYIKO MIONGONI MWA WASABATO

Kumekuwepo na kutengana kwa mfululizo miongoni mwa Wakristo kwa karne  nyingi. Utengano huo, sehemu nyingine ulizaa uchungu na Mateso kwa waliojitenga, wakibanwa na wale waliokuwa wenzao hapo awali. Historia fupi ya Ukristoinaonyesha Yesu aliwachukua mitume wake na kujitenga na kanisa la WAYAHUDI, na kuanzisha kundi la Kanisa la MITUME. Sababu kubwa ya utengano huo ilikuwa ni MAPOKEO Yaliokuwa yamekumbatiwa ndani ya kanisa la Kiyahudi. Yesu alipopinga mapokeo hayoalionekana yuko kinyume cha Wazee wakongwe wa imani ya Kiyahudi (Luka 19:45-48)

Vuguvugu la UPROTESTANTI la Karne ya 16 nalo lilizaa utengano na Kanisa la KIRUMI (Roman Catholic) lililokuwa Likiendesha mambo ya Imani pamoja  na Mapokeo. Utengano huo ulizaa UPROTESTANTI, na kuzaaMataifa ya Kiprotestanti. Taifa la Marekani lilinawiri katika mambo yote kwasababu lilijitangazia Uhuru wa mambo ya Imani na kuwa Taifa la Kiprotestanti lililompa kila mtu haki yakuabudu kwa uhuru.

Karne ya 19, (1840 – 1845), vuguvugu la Waprotestanti walioamini ujumbe wa Mungu wa Malaika wa Kwanza na wa Pili ilizaa kundi la Waadventista Wasaabato. Hili ni kundi linalotakiwa kuishi kwa kulingana na Maandiko ya Biblia na Roho ya Unabii tu. Mapokeo ya viongozi au maamuzi ya Halmashauri za Kanisa yasipolingana na Maandiko, laizma pawepo na upinzani dhidi ya Mapokeo yaliyoingizwa kanisani.

Katika migawanyiko iliyokumba Ukristo, ni pale tu serikali ya wakati husika, ilipokuwa ikitumiwa na mojawapo ya makundi hayo, ndipo Serikali ilipojiingiza na kutumia nguvu zake kupigania maslahi ya kundi moja. Hali hiyo ilionekana wakati wa utengano kati ya Wakatoliki na Waprotestanti. Wakatoliki walinufaika kutumia nguvu za Serikali kujaribu kuzima kile walichokiita wao kuwa ni Uasi. Matokeo tunayafahamu  wazi hata sasa, nayo yametabiriwa kujirudia tena. Roma itashika mamlaka ya Serikali tena kama Zamani. Ufunuo 17:12-18; Ufunuo 13:3-10

Mgawanyiko Miongoni Mwa Wasabato

Kumekuwepo na migawanyiko ndani ya Waadventista Wasabato katika vipindi Mbalimbali. Hapa Tanzania tunayo Makundi Makuu Matano (5)

1.      Waadventista Wasabato wa General Conference {GC} – (Association) ndilo lenye Washiriki wengi.

2.      Wasabato Waadventista (Masalio).

3.      Wasabato Matengenezo (Reform Movement).

4.      Tanganyika Sabato.

5.      Sabato Marejeo.

Hapa tutajadili na Kuchunguza katika MAANDIKO MATAKATIFU kuhusu MISINGI ya Kanisa la Wasabato Waadventista (Masalio) na Uhalali wake Kimaandiko Matakatifu Miongoni mwa Wasabato wengine.

Kanisa hili la Wasabato Waadventista Masalio ndilo la mwisho kugawanyika  kutoka Kanisa la Waadventista Wasabato wa General Conference Mwaka 2006 hapa Nchini.

Biblia ilitabirije juu ya Mgawanyiko huo. Mafungu yafuatayo ya Biblia yanazungumzia. Mathayo 24:12 – 22,  Marko 13:14 – 23,  Luka 19:41 – 44,  2Thesalonike 2:5,
Daniel 9:27,  Luka 21:20 – 23. 
Pia Kitabu cha Roho ya Unabii Pambano Kuu UK 18 na 28.

Mafungu hayo yote yanazungumzia juu ya Chukizo la Uharibifu ambacho ni kitendo cha Kanuni za Imani na Mafundisho Mapotovu  Kushirikishwa kufanywa kuwa sehemu ya Mafundisho au Imani ya Kanisa la kweli la MUNGU. Kanuni zetu za Msingi zilizostahimili kazi kwa zaidi ya Miaka 50 iliyopita zitahesabiwa kuwa hazina maana. 1SM 204.

Hapa tutataja baadhi ya Mafundisho, Sera au Kanuni Potofu Zilizofanywa kuwa Sehemu ya Imani ya Kanisa la Waadventista Wasabato la GC, mafundisho yaliyoleta Utengano na kufanya Wasabato wa General Conference {GC}  kuondoa Utakatifu wao kama Kanisa, na Kuipa nafasi MASALIO Kujitenga nao na Kuendelea na Imani Safi ya Wasabato kama lilivyoelezwa katika Maandiko Matakatifu na Vitabu vya Kanisa hilo.

Kumbuka tunazungumzia dhambi au uasi wa kanisa, si wa mtu binafsi.

1. Kanisa kuwaruhusu Wachungaji, Wazee wa Kanisa, Mashemasi na Wahudumu wengine kunyoa Upaa huku wakihudumu patakatifu, huu ni Moto wa Kigeni. Walawi 21:5,  Isaya 15:2,  torati 14:1,  Ezekiel 44:20, SDA Bible Commentary p 238,(435), 811 (1299).   Hao ni Mfano wa Makuhani wa Mungu wa Wamisri ISIS na Baal.

2. Baadhi yaWachungaji, Wazee wa Kanisa na Washirikki kuruhusiwa kuvaa na kuhudumu na Mavazi ya Wanawake kama Vitenge, Khanga katika mtindo wa Makoti, Kaunda Suti na Mashati. Torati 22:5

3. Baadhi ya wachungaji na washiriki kujiunga na vyama vya siri (Freemason, Jesuits n.k) huku wakiendelea kuwa wahudumu kanisani. 2Wakoritho 6:14 – 16, 2SM uk 121, 127, 130 – 140.

4. Baadhi  ya Wachungaji na Washiriki kuruhusiwa kujiunga na vyama vya Siasa na Jumuiya ya watetea Haki (Wanaharakati) SACCOS na Vikundi. 2Wakoritho 6:14 – 16, GW 391 – 396,  TM p 332 – 337,  Fe 475 – 484.  Yesu hakujihusisha na Jumuiya hizi.

5. Kanisa kujiunga na Umoja na Makanisa, WCC na NCC.  Great Controvesy p 555,  2koritho 14:17 – 18.

6. Kumweka mwanamke kufanya kazi ya Upatanisho ya Kuhani, Shemasi na Mzee wa Kanisa na Kusimama Mimbarini.  CW 53 – 54,  GW 303,  EV 224 – 225,  Pastral Ministry 242,  3SM 322,   Matukio uk 54,  Ufunuo 17:12,  1Timotheo 2:8,12,   Ufunuo 14:4.

7. Kutumia nembo au alama za Freemason kwenye beji na pini za Adventure, PFC na AY.

8. Umizimu wa kuenzi wafu kwa kuwavalisha mavazi kama vile, suti, gauni, viatu, saa n.k Mwanzo 3:19,   EW uk. 262 – 265

9. Kanisa kuacha na Kuondoa Misingi ya Imani yetu iliyotufanya tuwe wasabato, kubadili nembo ya kanisa na Jina la Kanisa.  GW 307,  FE 471, 472

10. Kanisa Kutumia Bima ya Maisha

SDA  ya  GC imeshindwa na Umizimu. Limefarakana na Roho ya Unabii, halimtumikii BWANA wetu Yesu Kristo, limekubali kuingiza Bima ili kufariji Kifo cha aliyepinduka na kufa katika gari, ajali ya Meli, Ndege na Moto, huku ni kujitenga na neno la Mungu.  Bible Commentary pg. 944,   1T 549 – 551

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni