Maandiko
SOMO LA 11
Alama Ya Mnyama
Tafadhali wasiliana na Kanisa la Waadventista
Wasabato
lililo karibu nawe, au tuandikie kwa anwani
hii:
Kibidula Bible Studies
P.O. Box 17
Mafinga/Iringa
Tanzania
Printed by:
Light Bearers Ministry
USA
•
Moja kati ya maonyo yenye lugha kali
kabisa katika Biblia
linapatikana
katika Kitabu cha Ufunuo.
Katika onyo hilo
Mungu anaelezea adhabu
watakayopata wale
watakaopokea alama ya mnyama.
“Mtu awaye
yote akimsujudu huyo mnyama
na sanamu
yake, na kuipokea chapa
(alama) katika kipaji
cha uso wake, au katika mkono
wake, yeye naye
atakunywa katika mvinyo ya
ghadhabu ya Mungu
iliyotengenezwa, pasipo
kuchanganywa na maji.”
Ufu. 14:9-10.
Ukisoma fungu la 12 linasema, “Hapa ndipo
penye
subira ya watakatifu,” hao wazishikao Amri za
Mungu, na
Imani ya Yesu.” Hapa tunayaona makundi mawili
ya watu
katika siku za mwisho. Wale wenye alama
(muhuri) ya
Mungu, ndio wale wazishikao Amri za Mungu, na
Imani ya
Yesu, na wengine ni wale wenye alama ya
mnyama, ndio wale
waliokubaliana na hila za Ibilisi.
Lakini kama mtu hajui alama ya mnyama ni ipi,
bila
shaka ataishia kuwa nayo hata bila kujua kuwa
anayo. Je, una
uhakika kuwa unaweza kuitambua alama ya
mnyama? Bila
hivyo maisha yako yako hatarini.
Somo hili linaweza kufunua ukweli dhidi ya
mambo
ambayo umekuwa ukiyaamini na kuyapenda sana
tangu
utoto. Lakini kwa kuwa Mungu katika upendo
wake
anatutumia ujumbe huu maalum, ni vyema
kuupokea na
kufuata ushauri wake.
“Heri asomaye na wao wayasikiao maneno ya
unabii
huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo; kwa
maana wakati u
karibu.” Ufu. 1:3.
1. Kwa kuwa tunataka
kujifunza juu ya Alama ya Mnyama,
mnyama mwenyewe ni kitu
gani?
“Wanyama hao wakubwa walio wanne ni wafalme
wanne
watakaotokea duniani.” Dan. 7:17.
Katika unabii mnyama anawakilisha ufalme,
serikali
au taasisi yenye mamlaka.
2. Mnyama anayeelezewa
katika Ufunuo 13 ana sifa zipi?
“Kisha nikaona mnyama akitoka katika bahari,
mwenye
pembe kumi, na vichwa saba, na juu ya pembe
zake
ana vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina
ya
makufuru. Na yule joka akampa nguvu zake na
kiti
chake cha enzi na uwezo mwingi. Nikaona
kimoja cha
vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la
mauti, na
pigo lake la mauti likapona. Dunia yote
ikamstaajabia
mnyama yule. Wakamsujudu yule joka kwa sababu
alimpa huyo mnyama uwezo wake; nao
wakamsujudu
yule mnyama, wakisema, Ni nani afananaye na
mnyama
huyu? Tena ni nani awezaye kufanya vita naye?
“Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu,
ya makufuru. Akapewa uwezo wa kufanya kazi yake
miezi arobaini na miwili. Akafunua kinywa
chake
amtukane Mungu, na kulitukana jina lake; na
maskani
yake, nao wakaao mbinguni. Tena akapewa
kufanya
vita na watakatifu na kuwashinda, akapewa
uwezo juu
ya kila kabila na jamaa na lugha na taifa. Na
watu wote
wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye
jina lake
halikuandikwa katika Kitabu cha Uzima cha
Mwana-
Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya
dunia.
“Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na
akili, na
aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni
hesabu ya
kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita,
sitini na sita.”
Ufu. 13:18.
Mnyama huyu anaonekana wazi kuwa ni taasisi
ya
kidini inayopingana na Mungu. Ni taasisi
inayotaka
kusujudiwa au kuabudiwa. Hebu tuziangalie
alama nane
za kuweza kuitambua taasisi hii.
A. Inapokea mamlaka yake toka kwa Joka
(fungu la 2).
Joka hapa anawakilisha Shetani (Ufu.
12:3,4,9),
lakini Shetani alifanya kazi yake kwa njia ya
ufalme
wa Roma. Mfalme wa Kiroma Herode alijaribu
kumwua Yesu kwa kuua watoto wa Bethlehemu
(Mt. 2:16-18). Hivyo Joka anamaanisha pia
ufalme
wa kipagani wa Roma.
Kuna taasisi moja tu ya kidini iliyopokea
kiti cha
enzi na mamlaka toka Ufalme wa Roma. Historia
inatueleza wazi kuwa taasisi hiyo ni Kanisa
la Roma.
“Kanisa la Roma lilijiingiza mahali pa Ufalme
wa Roma na kuuendeleza. Papa ni mrithi wa
Kaisari.” Bila shaka alama ya kwanza inahusu
Mamlaka ya Papa.
B. Ni ufalme ulioenea dunia nzima (fungu la
3,7).
Hakuna anayeweza kubisha kuwa mamlaka ya papa
ilienea dunia nzima katika karne za kati.
Alama hii
tena inahusu Mamlaka ya Papa.
C. Ingedumisha uwezo wake kwa miezi 42.
Miezi 42 ni sawa na siku 30 x 42 = 1260.
Katika
unabii siku moja ni sawa na mwaka mmoja
(Eze. 4:6). Uwezo wa Mamlaka ya Papa ulifikia
kilele mwaka 538 B.K. kutokana na barua ya
Mfalme Justinian iliyomtambua askofu wa Roma
kama mkuu wa makanisa yote. Hata hivyo, uwezo
wa Mamlaka ya Papa ulikomeshwa mwaka 1798
ambapo Jemadari wa Kifaransa, Berthier,
aliingia
Roma na kumteka Papa. Kuanzia mwaka 538 B.K.
hadi mwaka 1798 ni miaka 1260 kamili.
Onyo hili ni pamoja na:
(a) Msujudieni Muumbaji (fungu la 7).
Maana yake ni kuishika ishara au alama ya
uumbaji
wake, yaani, Sabato yake.
(b) Msipokee Alama ya Mnyama (fungu la 9-10).
Maana yake usiikubali wala kuipokea ishara ya
bandia ya utakatifu wa Jumapili.
Ni Mungu anayetupa maonyo haya. Shetani, adui
wa
Mungu anataka nimtii kwa kushika alama yake.
Yesu,
Mwokoziwangu anataka nimtii kwa
kuiadhimishaishara au
alama yake.
Je, sasa umeelewa kwamba mtu ye yote
Akiipokea Alama
ya Mnyama atapotea?
Yesu anabisha kwenye mlango wa moyo wako.
Anasubiri
jibu toka kwako. Je, utaamua kuipokea ishara
yake tukufu
kama ushahidi kwamba umempokea yeye kama
Bwana na
Mwokozi wako.
Uamuzi Wangu:
inaendelea kutoka nyuma
D. Ni taasisi yenye kufanya makufuru (fungu la
5,6).
Biblia inaelezea kuwa makufuru ni kudai kuwa
yeye
ni Mungu, na kudai kuwa ana uwezo wa kusamehe
dhambi (Yn 10:33; Luka 5:21).
Mamlaka ya Papa tena inayo alama hii, kwani
inadai kuwa mapadre wanaweza kusamehe dhambi.
Angalia jinsi Katekisimu moja inavyosema:
Swali: Je, Padre husamehe kabisa dhambi, au
huwa
anatangaza tu kwamba zimeondolewa?
Jibu: Padre husamehe kabisa dhambi kwa uwezo
aliopewa na Yesu Kristo.
Pia mamlaka hii hudai kuwa Mungu. Hii hapa
ni baadhi ya kauli zake: (1) “Wewe ni Mungu
mwingine hapa duniani.” (2) “Papa siyo
mwakilishi
wa Yesu Kristo tu, lakini ni Yesu Kristo
mwenyewe
aliyefichwa katika mwili.”
E. Ni taasisi iliyopata Jeraha la Mauti, kisha
likapona, na “dunia nzima ikamstaajabia”
(fungu la 3).
Mamlaka ya Papa ilipata pigo la mauti mwaka
1798 Papa alipotekwa na Jemadari Berthier na
kufia uhamishoni. Ulaya yote ilidhani kuwa
huo
ulikuwa mwisho wa Mamlaka ya Papa. Lakini
leo hii kila mtu anatambua kuwa Mamlaka ya
Papa ndiyo yenye ushawishi na mvuto kuliko
zote
duniani. Jeraha la mauti lilipona pale
Kiongozi wa
Italia (Musolini) alipomrudishia Papa Mamlaka
ya Kiserikali na kuunda Taifa la Vatikani
mwaka
1929. Leo hii mamilioni wanaiangalia Mamlaka
ya
Papa kama tumaini pekee la umoja, upendo,
amani
na uungwana. Hivyo tena Mamlaka ya Papa inayo
alama hii.
F. Ina namba ya siri 666. Ufunuo 13:17-18
inatuambia tuihesabu hesabu ya mnyama maana
ni hesabu ya kibinadamu.
Zingatia kuwa baadhi ya herufi za Kirumi
hutumika
pia kama namba. Hivyo basi, hesabu ya jina la
mtu ni jumla ya herufi zote zilizo katika
jina lake
zinazotumika kama namba.
Binadamu tunayemfikiria kila tunapozungumza
juu ya Mamlaka ya Papa ni Papa mwenyewe. Moja
kati ya majina rasmi ya Papa ni “MWAKILISHI
WA MWANA WA MUNGU” kwa Kirumi ni
‘VICARIUS FILII DEI’. Kitabu cha Ufunuo
kinasema kuwa jumla ya namba za Kirumi katika
jina lake ni 666. Hebu tuone.
V 5 F 0 D 500 112
I 1 I 1 E 0 53
C 100 L 50 I 1 501
A 0 I 1 501 666
R 0 I 1
I 1 53
U 5
S 0
112
Hivyo Mamlaka ya Papa inayo alama hii tena.
G. Ni Taasisi au Mamlaka ya Kidini.
Inajihusisha na mambo ya kiroho. Neno “kusujudia”
limetumika mara 4 katika Ufunuo 13. Sura hii
inahusu ibada ya bandia. Hii ni alama
nyingine
inayoonekana katika Mamlaka ya Upapa.
H. Itafanya vita na kuwatesa Wakristo (fungu la
7).
Historia inaonyesha wazi kuwa Mamlaka ya Papa
ilitesa na kuangamiza Wakristo, hasa katika
kilele
cha utawala wake katika karne za kati.
Wanahistoria
wengi wanasema zaidi ya watu milioni hamsini
waliuawa kwa ajili ya imani zao katika
kipindi
cha dhiki kuu. Kanisa lilidhani kuwa lilikuwa
linamsaidia Mungu kuondoa “uzushi.” Lakini
ukweli
unabaki pale pale kwamba lilitesa na
kuangamiza.
Mamlaka ya Papa tena inayo alama hii.
Zingatia: Wapo Wakristo wengi wa Kikatoliki
ambao ni wema, waaminifu na wenye upendo,
wanaomtumikia Yesu, na Yesu anawahesabu kuwa
ni
watu wake.
Papa Yohana Paulo II mwenyewe anaonekana
kuwa mtu mchangamfu, mwenye huruma, mwenye
kupenda mapatano, na jasiri anayempenda
Mungu.
Hili sio somo la kuwasuta rafiki zetu,
Wakristo
wa Kikatoliki. Hili ni shambulio dhidi ya
Ibilisi
aliyesababisha yote haya. Hata hivyo ni kweli
kwamba Mungu mwenyewe ndiye aliyetuambia
kuwa Taasisi hii ina alama ambayo hatupaswi
kuipokea. Waprotestanti waaminifu, Wakatoliki,
Wayahudi, na wasiokuwa katika kanisa lo lote,
wanapaswa kuijua alama hii ili wasiipokee.
Tunamshukuru Mungu kwa kuifunua mipango
mibovu ya Shetani ya kutuangamiza sisi sote.
Ili tuijue alama hii ya Mamlaka ya Papa, ni
lazima kwanza tuijue Alama ya Mungu.
3. Je, Mungu naye anayo
alama?
“Nikaona malaika mwingine, akipanda kutoka
maawio
ya jua, mwenye muhuri ya Mungu aliye hai;…
Akisema, Msiidhuru nchi, wala bahari, wala
miti, hata
tutakapokwisha kuwatia muhuri watumwa wa Mungu
wetu juu ya vipaji vya nyuso zao.” Ufu.
7:2,3. “BWANA
akamwambia, Pita kati ya mji, kati ya
Yerusalemu, ukatie
alama katika vipaji vya nyuso vya watu
wanaougua na
kulia kwa sababu ya machukizo yote
yanayofanyika kati
yake… Waueni kabisa, mzee, na kijana, na
msichana,
na watoto wachanga, na wanawake; lakini
msimkaribie
mtu ye yote mwenye hiyo alama; tena anzeni
katika
patakatifu pangu.” Eze. 9:4,6.
Mungu anayo alama kwa ajili ya watu wake.
4. Je, tunaweza kuijua alama
hiyo kwa uhakika?
“Tena naliwapa Sabato zangu, ziwe ishara kati
ya mimi
na wao, wapate kujua ya kuwa mimi, BWANA,
ndimi
niwatakasaye… Zitakaseni Sabato zangu; nazo
zitakuwa
ishara kati ya mimi na ninyi, mpate kujua ya
kuwa mimi
ndimi BWANA, Mungu wenu.” Eze. 20:12,20.
Kwa uhakika kabisa. Mungu ameweka Sabato ili
iwe ishara ya watu wanaomtambua kwamba yeye
ndiye
Muumbaji na kwamba yeye ndiye anayewatakasa
watu
wake (angalia pia Yer. 10:10-16).
5. Biblia inasema kuwa
Mamlaka ya Papa ingeazimu kufanya
jambo gani?
“Naye ataazimu kubadili majira na Sheria.”
Dan. 7:25.
Kubadili majira (muda) na Sheria. Mamlaka ya
Papa inajigamba yenyewe kuwa ilifanya jambvo
hilo.
Hebu angalia mahojiano haya yaliyo katika
Katekisimu
ya Waumini ya Mafundisho ya Kikatoliki,
katika ukurasa
wa 50.
Swali: Siku ya Sabato ni ipi?
Jibu: Siku ya Sabato ni Jumamosi.
Swali: Kwa nini tunaiadhimisha Jumapili
badala ya
Jumamosi?
Jibu: Tunaadhimisha Jumapili badala ya
Jumamosi
kwa sababu Kanisa Katoliki lilihamisha
utakatifu wa siku
hiyo kutoka Jumamosi kwenda Jumapili.”
Mtu mmoja aliposoma mahojiano haya
alishangaa,
naye akidhani kuwa wachapaji walikuwa
wamekosea,
alimwandikia James Cardinal Gibbons wa
Baltimore
na kumwuliza kama kweli kanisa lilibadili
siku ya
Ibada kutoka Jumamosi kwenda Jumapili
Kadinali
alijibu: “Ndiyo, Kanisa Katoliki linadai kuwa
badiliko
hilo lilikuwa ni tendo lake. Na tendo hilo ni
ALAMA
ya uwezo wake wa kikanisa na mamlaka yake
katika
masuala ya kidini.”
Angalia pia mahojiano haya katika Katekisimu
ya
Mafundisho iliyoandikwa na Stephen Keenan.
Swali: Je, unayo njia nyingine ya
kuthibitisha kuwa
kanisa lina uwezo wa kuweka sikukuu?
Jibu: “Kama lisingekuwa na uwezo kama huo,
lisingeweza kufanya jambo ambalo hata
wanadini wa
leo wanalikubali. Lisingeweza kuweka
maadhimisho
ya Jumapili, siku ya kwanza ya juma, badala
ya
maadhimisho ya Jumamosi, siku ya saba ya
juma,
mabadiliko ambayo hayakutokana na Maandiko.”
Mamlaka ya Papa hapa inauliza swali. Hapa
kuna
swali maarufu ambalo Mamlaka ya Papa imekuwa
ikiwauliza mara kwa mara Waprotestanti, na
cha
kushangaza Waprotestanti wamekuwa hawalijibu:
“Mtaniambia kuwa Jumamosi ilikuwa Sabato ya
Wayahudi. Lakini Sabato ya Wakristo
ilibadilishwa
kwenda Jumapili. Ilibadilishwa! Lakini na
nani? Ni nani
aliye na mamlaka ya kubadili amri dhahiri ya
Mungu
Mwenyezi? Mungu anaposema, “Ishike siku ya
saba
uitakase,” ni nani anayeweza kusema, hapana.
Unaweza
kufanya kazi na kushughulika na mambo yote ya
kidunia
katika siku ya saba, lakini uishike na
kuitakasa siku ya
kwanza badala yake? Hili ni swali muhimu
ambalo sijui
namna mnavyoweza kulijibu. Ninyi ni
Waprotestanti
na mnadai kuwa mnafuata Biblia, tena Biblia
peke yake,
na bado katika suala muhimu kama la
kuadhimisha
siku moja kati ya saba mnakwenda kinyume na
andiko
la Biblia na kuweka siku nyingine badala ya
ile ambayo
Mungu ameamuru. Amri ya kushika siku ya saba
ni
moja kati ya Amri kumi. Mnaamini kuwa zile
nyingine
tisa zinapaswa kushikwa, ni nani aliyewapa
ruhusa ya
kuichezea ile ya nne? Kama kweli mnashikilia
msimamo
wenu, kama kweli mnataka kufuata Biblia, tena
Biblia
peke yake, mnapaswa kutuonyesha sehemu katika
Agano
Jipya ambapo amri ya nne imebadilishwa.
(Nukuu
kutoka, Library of Christian Doctrine. Burns
and Oates,
uk. 3-4., London.)
Mamlaka ya Papa inadai kuwa ilibadili siku ya
Ibada
toka Jumamosi kwenda Jumapili na kwamba
Jumapili
au kushika Jumapili ni Alama ya Mamlaka na
Uwezo
wake. Alama au Ishara ya uwezo wa Mungu wa
kuumba
na kutakasa ni Sabato au kushika Sabato, na
Ishara au
Alama ya uwezo wa mnyama ni Jumapili.
6. Je, kuna wakati ambapo
watu watalazimishwa kupokea Alama
ya Mnyama?
“Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na
matajiri
kwa maskini, na walio huru kwa watumwa,
watiwe
chapa katika mkono wao wa kuume, au katika
vipaji
vya nyuso zao; tena kwamba mtu awaye yote
asiweze
kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile,
yaani, jina
la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.” Ufu.
13:16,17.
Biblia inasema wazi kwamba watu watawekewa
vikwazo vya kiuchumi na hata kuuawa
wasipoipokea
Alama ya Mnyama.
7. Nifanye nini sasa ili
nisiipokee alama hiyo?
Ufunuo 14:9-11 inaonya juu ya Alama ya
Mnyama;
fungu la 12 linaelezea jinsi watakatifu
watakavyofanya
ili kuepuka alama hiyo. Watashika Amri za
Mungu na
kuwa na Imani ya Yesu. Bwana asifiwe, ni
imani ya Yesu
inayofanya mwujiza kwa watu wanaoshika amri.
Ujumbe wa Onyo la Mwisho toka kwa Mungu
(Ufu. 14:6-12).
inaendelea mbele
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni