Ijumaa, 3 Agosti 2018

Sura ya 3 Mguu wa Kulia wa Kuzimu


Sura ya 3

Mguu wa Kulia wa Kuzimu na Mary K Baxter 

Sikuweza kulala wala kula tangu nilipotoka kuzimu usiku uliopita. Kila siku kumbukumbu
za kuzimu zilinijia. Nilipofumba macho; nilichokiona ni kuzimu tu. Masikio yangu
hayakuweza kuzuia nisisikie kelele za waliolaaniwa. Mambo niliyoyaona kuzimu yalinijia
mara kwa mara kama kwamba nilikuwa naangalia kipindi cha televisheni. Kila siku
nilikuwa kuzimu, na kila siku nilikuwa natafuta namna ya kuueleza ulimwengu juu ya
mambo haya ya kutisha.
Yesu alinitokea tena na kusema, "Leo tunakwenda ndani ya mguu wa kushoto wa
kuzimu, mwanangu. Usiogope, maana nakupenda na nipo pamoja nawe."
Uso wa Bwana ulikuwa na masikitiko, na macho yake yalijaa upole na upendo. Ingawaje
waliokuwa kuzimu walikuwa wamepotea milele, nilijua kwamba bado alikuwa anawapenda
na angewapenda milele.
"Mwanangu," Alisema, "Mungu, Baba yetu, alimpa kila mmoja wetu utashi ili
kuchagua kumtumikia Yeye au Shetani. Unajua, Mungu hakuumba kuzimu kwa ajili
ya watu wake. Shetani anawadanganya watu wengi wamfuate, lakini kuzimu
kulitengenezwa kwa ajili ya Shetani na malaika zake. Sio mapenzi yangu, wala
mapenzi ya Baba yangu, kwamba mtu yeyote apoteeMachozi ya huruma yalitiririka
kwenye uso wa Yesu.
Alianza kusema tena, "Kumbuka maneno yangu katika siku za mbele
nitakapokuonyesha kuzimu. Ninayo mamlaka yote mbinguni na duniani. Sasa, mara
nyingine itakuwa kama nimekuacha, lakini sitakuacha. Kuna wakati tutaonekana na
14
nguvu za giza, na wakati mwingine hazitatuona. Kokote tutakakokwenda, uwe na
amani na usiogope kunifuata."
Tulikwenda pamoja. Nilimfuata kwa karibu nikilia. Kwa siku kadhaa nilikuwa nalia, na
sikuweza kabisa kuuondoa uwepo wa kuzimu ambao wakati wote ulikuwa mbele yangu.
Zaidi nililia ndani kwa ndani. Roho yangu ilikuwa na majonzi sana.
Tulifika kwenye mguu wa kulia wa kuzimu. Nilipotazama mbele niliona njia iliyokuwa kavu
na imeungua. Vilio viliijaza hewa chafu, na harufu ya mauti ilikuwa kila mahali. Mara
nyingine harufu ilikuwa mbaya kiasi cha kunifanya nijisikie kutapika. Kila mahali palikuwa
giza isipokuwa mwanga uliokuwa unatoka kwa Kristo na mashimo ya moto, ambayo
yalijaa kila mahali kwa kadri ya upeo wa macho.
Mara, mapepo ya kila aina yalianza kutupita. Vipepo vilitumulika vilipotupita. Mapepo ya
kila ukubwa na umbile yalianza kusemezana. Mbele yetu, pepo kubwa lilikuwa linatoa
amri kwa mapepo madogo. Tulisimama kusikiliza, na Yesu alisema, "Vile vile kuna jeshi
lisiloonekana hapa la nguvu za giza- kama vile mapepo ya magonjwa."
"Nenda!" Pepo kubwa liliviagiza vipepo vidogo. “Kafanye mambo mengi maovu. Vunja
familia. Washawishi Wakrsto dhaifu, na fundisha uongo na wapotoshe watu wengi kadri
mtakavyoweza. Mtapata dhawabu yenu mtakaporejea. Kumbuka, jihadharini na wale
waliompokea Yesu kuwa Mwokozi wao. Wana uwezo wa kuwafukuza. Nendeni sasa
ulimwenguni pote. Ninao wengi kule na bado nitawapeleka na wengine. Kumbuka, sisi ni
watumishi wa mfalme wa giza na nguvu za anga.”
Baada ya hapo, nguvu za giza zilianza kutoka chini na kuruka juu hadi nje ya kuzimu.
Milango juu ya mguu wa kulia wa kuzimu ilifunguka na kufungwa kwa kasi sana
kuziruhusu hizo nguvu za giza kutoka nje. Zingine zilipanda juu na kutokea kwenye pango
tuliloingilia.
Nitajitahidi kuelezea maumbile ya viumbe hivi. Aliyekuwa anazungumza alikuwa na umbo
kubwa sana dubu mkubwa, rangi ya kikahawia, alikuwa na kichwa kama popo na macho
yaliingia ndani sana ya uso wenye minywele. Mikono yenye minywele ilining’inia pembeni,
na meno yalijitokeza kwenye nywele za uso wake.
Mwingine alikuwa mdogo kama nyani akiwa na mikono mirefu sana na nywele mwili
mzima. Uso wake ulikuwa mdogo, na alikuwa na pua iliyochongoka. Sikuona macho juu
ya mwili wake mahali popote.
Mwingine tena alikuwa na kichwa kikubwa, masikio makubwa na mkia mrefu, na mwingine
alikuwa mkubwa kama farasi na ngozi laini. Maumbile ya mapepo haya mabaya yalinitia
kichefuchefu. Kila nilikotazama kulikuwa na mapepo.
15
Kubwa kushinda yote ya mapepo haya yalikuwa yanapokea amri moja kwa moja kutoka
kwa Shetani, ndivyo Bwana alivyoniambia.
Yesu na mimi tulitembea kwenye njia hadi tulipofika kwenye shimo lingine. Vilio vya
maumivu, sauti za masikitiko zisizosahaulika, zilisikika kila mahali. Bwana wangu, nini
zaidi? Niliwaza.
Tulitembea kuvipita baadhi ya viumbe hivi vibaya, ambavyo havikuelekea kutuona, na
kusimama kwenye shimo lingine la moto na kiberiti. Katika shimo hili kulikuwa na mtu
mwenye umbile kubwa. Nilimsikia akihubiri injili. Nilimtazama Yesu kwa mshangao
nikisubiri jibu, maana wakati wote aliyajua mawazo yangu.. Alisema, " Alipokuwa
duniani mtu huyu alikuwa mhubiri wa injili. Wakati fulani alisema kweli na
kunitumikia."
NiIishangaa, mtu huyu alikuwa anatafuta nini kuzimu? Alikuwa na kimo cha futi sita, na
mifupa yake ilikuwa michafu, kijivu, kama jiwe la kaburi. Vipande vya nguo vilimnin’ginia
bado. Nilishangaa kwanini moto haukuunguza vipande hivi vya nguo. Nyama iliyokuwa
inaungua ilikuwa inamning’inia, na kichwa kilionekana kuwaka moto. Harufu mbaya ilitoka
kwake.
Nilimwona amenyosha mikono yake kama kwamba ameshika kitabu na alianza kusoma
Maandiko kutoka kitabu kisochokuwepo. Nilikumbuka tena Yesu alivyokuwa ameniambia.
Yesu alisema, "Kuzimu unakuwa na ufahamu wako wote, na unakuwa mkubwa zaidi.
" Yule mtu alisoma Andiko hadi Andiko, na nilidhani ilikuwa vizuri. Yesu alimwambia yule
mtu kwa upendo mwingi katika sauti yake, “Amani, tulia." Mara moja mtu yule aliacha
kusema, aligeuka taratibu kumwangalia Yesu.
Niliona roho ya mtu ndani ya mifupa hii. Alimwambia Bwana, "Bwana, sasa nitahubiri kweli
kwa watu. Sasa, Bwana, niko tayari kwenda na kuwaambia wengine kuhusu mahali hapa.
Najua kwamba nilipokuwa duniani nilikuwa siamini kwamba kuna kuzimu, wala sikuamini
kwamba ungerudi tena. Ndivyo watu walivyotaka kusikia, sikutetea kweli. Najua kwamba
sikumpenda yeyote wa rangi au asili tofauti na mimi, na nilisababisha watu wengi
kujitenga nawe. Nalitengeneza taratibu zangu mwenyewe kuhusu mbingu na kuhusu
jambo gani ni sahihi na lipi si sahihi. Najua kwamba niliwapotosha wengi, na nilisababisha
wengi kujikwaa kwa Neno lako Takatifu, na nilichukua fedha kutoka watu fukara. Lakini,
Bwana, nitoe humu nami nitajirekebisha. Sitachukua tena fedha za kanisa. Nimetubu
tayari. Nitawapenda watu wa kila aina na kila rangi.
Yesu alisema, "Sio tu kwamba ulipindisha na kutoa tafsiri ya uongo ya Neno la
Mungu, Bali ulidanganya kwamba hujui ukweli. Mimi mwenyewe nilikutembelea na
kujaribu kukugeuza, lakini hukutaka kusikia. Ulikwenda njia yako mwenyewe, na
ubaya ulikuwa ndio bwana wako. Uliijua kweli, lakini hukutaka, lakini hukutaka
16
kutubu na kunigeukia. Nilikuwepo pale wakati wote. Nilikusubiri. Nilitaka utubu
lakini hukutaka.
Masikitiko yalikuwa kwenye sura ya Yesu. Nilijua kwamba mtu huyu angelisikia wito wa
Mwokozi, asingekuwa hapa sasa. O nyie watu, tafadhali sikilizeni.
Yesu alisema tena na mkosaji “Ulipaswa kusema kweli, na ungewageuza wengi
kwenye haki kwa Neno la Mungu, ambalo linasema kwamba wote wasioamini
sehemu yao ni katika ziwa linalowaka kwa moto na kiberiti. Uliijua njia ya msalaba.
Uliijua njia ya haki. Ulijua kusema kweli. Lakini Shetani alijaza uongo kwenye moyo
wako, na ukaingia katika dhambi. Ulistahili kutubu kwa moyo wa kweeli, sio nusu
nusu. Neno langu ni kweli. Halisemi uongo.Baada ya kusikia hayo, mtu yule
alinyosha mkono kwa Yesu kwa hasira, akaanza kumlaani.
Kwa huzuni, mimi na Yesu tuliondo kuelekea shimo lingine. Mhubiri aliyeanguka
aliendelea kulaani na kumkasirikia Yesu. Tulipokuwa tunapita kwenye mashimo ya moto,
mikono ya wapotevu ilinyooshwa kutka kumfikia Yesu, na kwa sauti ya kubembeleza
waliita na kuomba rehema.
Mifupa ya mikono yao na miguu yao ilikuwa na rangi ya majivu meusi kutokana na
kuungua- hakuna nyama yenye damu, hakuna viungo, ni mauti tu na kifo. Nilikuwa nalia
ndani kwa ndani,O dunia, tubu. Usipotubu utakuja hapa. Acha kabla hujachelewa.
Tulisimama tena kwenye shimo lingine. Nilisikia huzuni mno kwa ajili yao wote kiasi cha
kwamba nilijiona dhaifu katika mwili hata kusimama wima ilikuwa vigumu. Kilio cha kwikwi
kilinitisa. “Yesu, naumia sana ndani.” Nilisema.
Kutoka ndani ya shimo sauti ya mwanamke ilisema na Yesu. Alisimama katikati ya moto,
na ulimfunika mwili mzima. Mwili wake ulijaa mafunza na nyama mfu. Moto ulipokuwa
unawaka kumzunguka, alinyosha mikono yake kwa Yesu akilia. “Nitoe humu. Sasa
nitakupa moyo wangu, Yesu. Nitawaeleza wengine habari za msamaha wako.
Nitakushuhudia. Nakusihi, tafadhali nitoe”
Yesu alisema, "Neno langu ni kweli linasema kwamba watu wote lazima watubu na
kuziacha dhambi zao na kuniomba niingie katika maisha yao kama wanataka
kukwepa kuja hapa. Katika damu yangu kuna ondoleo la dhambi. Mimi ni
mwaminifu na wa kweli ni nitawasamehe wote wanaokuja kwangu. Sitawatupa nje.
Aligeuka, alimwangalia mwanamke na kusema, "Ungelinisikiliza na kuja kwangu na
kutubu, ningelikusamehe.”
Yule mwanamke aliuliza, Bwana, hakuna njia nyingine ya kutoka hapa?”
17
Yesu alimjibu kwa upole sana. “Mwanamke,” alisema, ulipewa nafasi nyingi za kutubu,
lakini roho yako sugu haikutaka. Ulilijua Neno langu kwamba waongo sehemu yao
ni katika ziwa la moto
Yesu alinigeukia na kusema, "Mwanamke huyu alikuwa na matendo ya dhambi na
wanaume wengi, na alisababisha nyumba nyingi kuvunjika. Pamoja na hayo yote
niliendelea kumpenda. Nilikwenda kwake sio kwa kumhukumu bali kwa ukombozi.
Niliwatuma kwake watumishi wangu wengi ili atubu na kuacha njia zake mbaya,
lakini hakutaka. Alipokuwa mwanamama kijana, nilimwita, lakini aliendelea kufanya
maovu. Alifanya maovu mengi, bado ningelimsamehe kama angelikuja
kwangu.Shetani alimwingia, akawa na uchungu na hakuweza kuwasamehe
wengine. Alikwenda kanisani ili tu kuwatafuta wanaume. Aliwapata na kuwanasa.
Angelinijia, dhambi zake zingelitakaswa zote kwa damu yangu. Upande mmoja
alitaka kunitumikia, lakini huwezi kumtumikia Mungu na Shetani kwa wakati mmoja.
Kila mmoja lazima aamue nani atakayemtumikia."
"Bwana,” Nililia, “nipe nguvu za kuendelea” Nilikuwa natetemeka tangu kichwa hadi miguu
kwa sababu ya mateso ya kuzimu.
Yesu aliniambia, “Amani, tulia
"Nisaidie, Bwana” Nililia. Shetani hataki tujue ukweli kuhusu kuzimu. Nilikuwa sijawahi
kufikiria kwamba kuzimu kungekuwa namna hii. Mpendwa Yesu, haya yataisha lini?”
"Mwanangu,” Yesu alijibu, “Baba peke yake ndiye anayejua mwisho utakavyokuwa.
Alisema nami tena na kuniambia, “Amani, tulia.Nguvu nyingi zilinijia.
Yesu na mimi tulitembelea mashimo mbalimbali. Nilitamani kumvuta kutoka kwenye
shimo la moto kila mtu tuliyemkuta na kumkimbiza kwenye miguu ya Yesu. Nililia ndani
kwa ndani. Niliwaza: sitaki watoto wangu waje huku.
Hatimaye, Yesu alinigeukia na kuniambia, “Mwanangu, tutakwenda nyumbani kwako
sasa. Kesho usiku tutarudi tena kwenye sehemu hii ya kuzimu.
Niliporudi nyumbani nililia na kulia. Wakati wa mchana picha ya kuzimu na mateso ya
watu wa kule ilinijia. Nilimwambia kila mtu niliyekutana naye mchana habari za kuzimu.
Niliwaambia kwamba mateso ya kuzimu hatasimuliki, ni vigumu kuamini.
Mnaosoma kitabu hiki, nawasihi, tafadhali, tubu dhambi zenu. Mwite Yesu na mwambie
akuokoe. Mwite leo. Usingoje mpaka kesho. Kesho huenda isifike. Muda unakwisha
haraka. Piga magoti usamehewe dhambi zako. Mpendane. Kwa ajili ya Yesu, iweni
wapole na msameheane.
18
Kama umemkasirikia mtu msamehe. Hakuna hasira iliyo na uzito wa kutosha kukupeleka
kuzimu. Uwe mtu wa kusamehe kama Kristo alivyotusamehe dhambi zetu. Yesu ana
uwezo wa kuvumiliana nasi tukiwa na moyo wa toba na atafanya damu yake isafishe
dhambi zote. Wapende watoto wako, na wapende jirani zako kama unavyojipenda
mwenyewe.
Bwana wa makanisa anasema, "Tubu nawe utaokolewa!"

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni