MAANA YA KANISA
(Kanisa ni nini?)
“Na juu ya
Mwamba huu nitalijenga kanisa langu. Wala milango ya kuzimu haitalishinda” Yesu
ndiye Mwamba. 1Kor 10:4 “Kwa maana
Waliunywea Mwamba wa Roho uliowafuata na
Mwamba ule ulikuwa ni Kristo”
Yesu
hakujenga jingo lolote na Kuliita Kanisa. Yesu hakutenga watu wowote
waliomwamini na kuwaita kanisa. Bali aliwaita wanafunzi wake. Yesu Kristo ndiye
Kanisa, ndiye Hekalu. Yh 2:19-21.
Ndiye pekee aliyeshinda milango ya kuzimu kama alivyosema alifufuka siku ya
tatu. Akalisimamisha hekalu la MUNGU milele. Kanisa ambalo ndiye yeye mwenyewe
likashinda umizimu, yeye ndiye ana funguo za mauti (kuzimu). Hakuna jingo
lolote liitwalo Kanisa, ambalo limefufuka na kushinda mauti. Hakuna watu
(waumini) wowote ambao wameitwa Kanisa, walioshinda mauti (umizimu). Badala ya
watu ao kushinda umizimu, wao ndio wameshindwa kabisa na umizimu. Wanaenzi wafu
kupindukia. Na wengi wanafia dhambini, bila kutubu. Matokeo yake, ni kuingia
katika hukumu ya MUNGU; moto na kibiriti Uf
20:7-9;10. Na majumba yote yaliyoitwa Makanisa yatafumuliwa kwa moto. 2Petro 3:10. Lakini Yesu ambaye ndiye
Kanisa ndiye Neno Yh 1:1
hatafumuliwa. Yeye ndiye atawafumua waongo wote na majengo yao makubwa.
Inashangaza Mkristo, Mchungaji, na kiongozi mkuu wa dini anaita majengo wanamoabudia,
na kuimba humo, eti kanisa!! Majengo amabyo yatafumuliwa na moto, kama vile
hekalu (jengo) la Yerusalemu, lilivyofumuliwa na moto. Na jiwe halikubaki juu
ya jiwe. Eti haya ndiyo kanisa la Yesu alilolijenga juu yake mwenyewe!!
Eti haya majengo ndiyo Yesu amaanishe kuwa kanisa la yesu alilolijenga juu yake
mwenyewe!! Majengo ya sasa japo yajengwe kwa vigae, mabati ya South Africa au
Kenya na madirisha makubwa ya vioo vipana, na kuta za urembo, vyumba na
waya, yatafumuliwa siku ya mwisho. Kanisa la Yesu haliwezi kufumuliwa na moto.
Leo kwa
tafasiri potovu, watu wanaita majengo yao ya ibada Kanisa, lakini si kanisa. Ni
jengo. Yesu aliacha kanisa lake, na leo linaendelea lakini hakuacha jengo
lolote kwa maana ya Kanisa. Aliacha neno lake Mt 7:24. Wanafunzi nao hawakuwa kanisa. Wala watu wote walio
mwamini. Hao walikua wanafunzi na sio Kanisa. Yesu alipoona wengine wanamwacha Yh 6:66-69, aliwauliza wanafunzi wake,
“Ninyi nanyi mwataka kuondoka”? Petro kwa niaba ya wote alijibu, “Twende kwa
nani”? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele, nasi tumesadiki, tena tumejua
yakuwa wewe ndiwe mtakatifu wa Mungu. Yh 6:68,69. Wanafunzi hawakuwa na Kanisa
lingine lenye maneno ya uzima, ila Yesu tu. Wale waliorudi nyuma wasiandamane
nae tena, Yh 6:66, walirudi jengoni
ndilo hekalu, ambalo lilifumuliwa mwaka 70AD na Warumi. Waliliacha Kanisa
ambalo ni Yesu, mwenyewe. Waliacha Kanisa waliacha hekalul la agano jipya
lililoimama milele baada ya kufufuka kwake Yh
2:19,21. Mtu anayemwacha Yesu, asisadiki maneno yake, huyu ndiye aliacha
Kanisa. KANISA NI NENO LAKE: NA NENO NI YESU. Yh1:1,14 Mt 7:24 Yh 2:19,21
Yh 1:12. “Bali waliompokea aliwapa uwezo wa
kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake” Wale waliomwamini
Yesu, hawakuwa Kanisa, bali watoto wa MUNGU. Ni makosa yatokanayo na tafsiri za
walimu wa uongo, na mafisadi 2Petro
2:1-2, wanaojifanya kuwa ndio Kanisa. Huku umizimu, udhalimu, uasi, uongo
vimekithiri miongoni mwao. Watu hawa wameyaita majumba ya kuabudia kuwa ni
makanisa hata kama ndani yake wanacheza dansi, wanaabudu sanamu, na kufuata
Sera za Mnyama kupitia Utandawazi (UTDZ). Ndivyo ilivyozoeleka. Mfano: mtu
mgeni anauliza; hili jumba (jengo) kubwa ni la nini? Jibu ni Kanisa la
Pentekoste; au la RC; au KKKT, au SDA n.k. ilivyozoeleka kwa kitu, kuitwa hivyo
siyo ukweli wa kuwa vile. Kuna tofauti kati ya kitu Fulani kuitwa vile, lakini
kisiwe vile halisi. Kuitwa na kuwa ni tofauti. To be called, and to be real,
are two different ideas. Mf huyu kijana anitwa Bongoman, lakini si Bongoman
mwenyewe, kuitwa anaitwa tu lakini hawi kama anavyoitwa. Ibrahimu alimwita
Sara, kuwa ni umbu lake; huku ni mke
wake. Hakuwa umbu lake. Kwa kosa hilo la kuita mtu, asivyo, Farao alimchukua
kuwa mke wake. Kwa huruma ya MUNGU na uwezo wake, Farao akapambana na maajabu
kwa kumchukua umbu la Ibrahimu kumbe sio umbu, bali ni mke wake. Haya ni
matokeo ya kuita kitu kwa makosa, kisivyo halisi.
Ndivyo
ilivyo leo kwa madhehebu yaitayo majengo yao ya ibada kuwa ni makanisa. Hivyo,
uongo huu, ukasababisha madhehebu mengi kuanzishwa yakijiita makanisa, lakini
bila kutoa neno la MUNGU. Isaya 8:20
“Nawaende kwa sheria na ushuhuda”, lakini bado wanahubiri watu waende humo; na
wasiojua wanajiunga na majengo tuu, yasiyo na Yesu.
Mungu ana
Kanisa moja tu, lishikalo Amri za MUNGU na Imani ya Yesu. Kama ilivyokuwa kwa
hekalu walibaki tu na nyumba yao iliyokuwa tupu bila Yesu Mt 23:8,39. Hawa waliita majengo kuwa Kanisa bila kulifuata NENO la
MUNGU, bila kuwa na Yesu, ambaye ndiye Kanisa, ndiye mlango. Wao badala ya
kuwaelekeza watu kwa Yesu na NENO lake wakawapeleka katika majengo ya ibada.
Wakawaacha waamini maneno potovu kuwa wao ndio Kanisa. Walikwea kwingineko.
Hawakuingilia Mlangoni. Walikuwa wevi na wanyang’anyi, Yn 10:1,2,8. Kwa kuwa ni majengo tu, bila Yesu, ibada zao ni za
kuimba, kucheza kupiga ngoma, vigelegele, makofi, kulia ovyo tu eti ni kushikwa
na Roho au kunena kwa lugha, kumbe ni kiuga tu, msisimko na humo si kanisa,
bali ni jumba la anasa tu (Social Hall)
Kanisa la
MUNGU ambalo ni Yesu mwenyewe, mwanadamu hawezi kuja kwa ufedhuli. Eti badala
ya kunyenyekea, kujifunza kwa utulivu, kuomba na kuungama, ila anatenda dhambi
zaidi akiwa ndani. Je akitoka nnje itakuaje? Watu wanaingia na mavazi ya aibu
kwa kuwa siyo Kanisa ni jengo tuu. Kanisa ambalo ni neno la yesu linaonya na
kufundisha hivi. Mh 5:1,2 4T uk 648 Kumb
22:55.
Je wale
waliotoka katika majengo ya ibada yao ni waasi? Kuna wajibu mawili. Ndiyo na
Hapana. Wale waliotoka humo wakaacha misingi halali, kanuni za haki na utaratibu
safi, kamazilivyoasisiwa na neno la MUNGU, wakaanzisha mafundisho mengine
potovu, kama ilivyokwisha elezwa, ni waasi. Wale walioyaacha majengo, wakazidi
kudumisha misingi yote, kanuni zote, na taratibu zote za SDA hawa ndio wamo
katika kanisa la Yesu. Kujitenga na Maasi ndani majengo sio kuacha kanisa.
Kuacha kanisa ni kuasi misingi yetu ya kanisa la waadventista wasabato. Mf.
kufanya mabaraza siku ya sabato, ni kuacha kanisa yaani NENO – Yesu. Yesu ndiye
Bwana wa Sabato, kwa hiyo umemuasi Yesu. Mwanamke kuvaa suruali ameliacha
Kanisa – Neno Kumb 22:5
Mwanamke
kutamalaki (kuhubiri) mimbarini ni kuacha Kanisani – Neno – Yesu 1Tm
2:11; 1Kor 14:34. Mwanamke ni sawa
na kondoo jike na chombo dhaifu. Hawezi
kumwakilisha Yesu Kuhani Mkuu wa huduma ya Upatanishi.
Law 16;3,5,8; 20:37. 1Pt 3:7
Wanawake wahubirio mimbarini, huku wakijua hawana sifa za utumishi
mtakatifu kwa huduma ya ukuhani (upatanisho) ni wahuni wa kiroho kabisa. Wako
nnje ya Kanisa la Yesu – SDA. Wako nnje ya NENO – Yesu.
Soma Law 21:18-21 Licha ya kuharibika kwa
kiungo hicho cha kiume, je mwanamke anacho? Maonyo mengine kwa wahudumu Ez 44:18-20. Je watavaa suruali? Je
neno litamruhusu Mwanamke kuvaa Suruali? Suruali ni vazi limpasalo Mwanaume.
Mwanamke akivaa Suruali Mimbarini, mbona ndio Babel!! (Machafuko)
Kwa hiyo,
tokeni kwake enyi watu wangu. PP166 Kabla ya kuangamizwa kwa
Sodoma, MUNGU alipeleka ujumbe kwa Lutu ajiponye nafsi yake, asitazame nyuma.
Onyo lilelile lilitolewa kwa wanafunzi, kabla Jerusalemu Haijaangamia. Lk 21:20,21
Kulikuwa
kuna kutoka, kutengana kwa makusudi kwa
makusudi na waovu, kujiponya kwa maisha ndivyo ilivyokuwa siku za Nuhu, Lutu,
na Kwa wanafunzi kabla ya Jerusalemu kuangamizwa. Na ndivyo itakavyokuwa siku
zetu hizi za Mwisho, sauti tena itasikika kwa ujumbw wa onyo, ikiwahimiza watu
wake wajitenge kutoka kwa uasi – uovu uliokithiri, lazima tujitenge na ndugu
wasio waaminifu 2Thes 3:6,7.
~MUNGU AWAFUNULIE NURU YA
UKWELI HUU AMINA~
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni